Elections 2010 Mbunge kuishi nyumba ya kupanga ni halali kwenye jimbo lake?

HAWA NDIO WATANGANYIKA BONGO LA-LA-LA A LA AAAAAAAA!! YAANI MBUNGE WAO AKISHACHAGULIWA WATAMWONA TENA WAKATI WA UCHAGUZI AU WAKATI AMESIKIA KIONGOZI WA SERIKALI ANATEMBELEA JIMBONI MWAKE NDIO UTAMWONA ANAJISHEBEDUA KUWA KARIBUKARIBU! HII INATIA SHAKA KAMA KWELI WANANCHI WENGI WATANZANIA HUWA WANAJUA WANACHOKIFANYA WAKATI WA KIPIGA KURA!
>>> Mfano mtu kama huyu Mbunge wa Tarime sijui anaitwa '' Nyambari Nyagwine''....Anaishi Dar es saalaam ni lini atajua matatizo ya wana TARIME? .....Ndo maana sishangai kusoma habari zake kwenye gazeti la Mwananchi la leo 03/01/2011 Anakutana na wajumbe wa CCM kawe kuwauliza kwa nini Jimbo la KAWE Limechukuliwa na wapinzani (Chadema) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! JE HAYA NDO WANA TARIME WALIYOMTUMA??????????????? Watu kama hawa 2015 waogopwe kama UKoma......
 
Tuache unafiki hapa hebu tuwe wakweli, ni wabunge wangapi bila kujali wanatoka chama gani wana nyumba kwenye majimbo yapo ya uchaguzi?
 
Wewe KIlembwe kweli!!! Tatizo lako unasahau kuwa wabunge wengi ni wa CHAMA chako hivyo unavyozungumzia wabunge wangapi basi ulitakiwa ujue kuwa Wabunge wengi wa chama chako hawana nia ya dhati ndio maana wengi wao hawana nyumba majimboni mwao! Kwa taarifa yako si dhambi mbunge kuwa na nyumba DAR au mbali na Jimbo lake! Ila Walau awe na nyumba Jimboni kwake na muda mwingi autumie jimboni kwake. Kwa taarifa yako zaidi ya 75% ya Wabunge wa CDM walioshinda majimbo yao wanakaa Sehemu husika ukilinganisha na chama chako!
 
Mimi nafiriki mbunge anapaswa kupimwa kwa namna anavyotekeleza au atakavyotekeleza ahadi zake kwa wananchi na si kwa kuwa au kutokuwa na nyumba jimboni,kwani hili halitowasaidia wananchi mwisho wa siku!!!
 
mbona balozi wa nchi ana makazi nje ya nchi yake na anatoa huduma na kupeleka maendeleo nchini mwake? it works like that

miss hapo si kweli. balazi huko ANAKOPELEKWA huwa anaenda kupanga tu na ndiyo maana aliye mpeleka huko (TO LIE ON HIS BEHALF (PRESIDENT) ABOUT HIS GOVERNMENT AND COUNTRY) akishajua kuwa jamaa ameshaishiwa uongo, anamrudisha home au kumbadilishia pango kwa kumpeleka nchi nyingine to lie for his/her head of state and government.
 
mfano mbunge wa tarime kapanga na makazi yake yako dar es salaam je inakuaje muda wake wote ameishi dar alafu apate ubunge tarime, ni kitu gani huwa kinatokea kwa wananchi wanao amua kumpa kura mtu ambaye wanajua kabisa akishapata uongozi anarudi kwenye makazi yake ambako amezoea na kwa shughuli zake zote
Na inakuwaje mbunge wa sehemu fulani apewe ukuu wa mkoa mahala pengine...........??? Au hata huyo waziri mkuu
 
Mimi nafiriki mbunge anapaswa kupimwa kwa namna anavyotekeleza au atakavyotekeleza ahadi zake kwa wananchi na si kwa kuwa au kutokuwa na nyumba jimboni,kwani hili halitowasaidia wananchi mwisho wa siku!!!

nyumba yako mwenyewe ya kuishi ni muhimu jimboni mwako. tusidanganyane hapa.
 
....Sio contradiction yoyote kwa sababu sio kosa la mbunge kuwepo kwa simu moja ya kukoroga. Unaongelea "hewa" ...Awaachie wanaoweza kukaa huko na kuondoa hali umasikini kwa kufanya kazi bega kwa bega na waliomchagua.Kwanini asigombee jimbo lenye simu kila kona ili awasiliane vizuri na wizara? Kama angekuwa anaishi huko jimboni kwake lazima hayo matatizo yangemgusa pia na angetafuta solution right away.

...Ndiyo shida ya umasikini na ndg yake umbumbumbu..... maana hata priority hatuzijui na badala ya kuangalia mambo ya msingi tunaanza kuhangaikia mambo ya nani anaishi wapi ect. Kazi gani hizo za bega kwa bega au paja kwa paja ambazo unategemea hao masikini wazifanye ili kuleta hayo maendeleo ?

Binafsi hata kama mbunge anakaa nje ya inji, i dont care kama wajibu wake anautekeleza. I care about the end product- period na sio anaishi wapi ect.

Na kwa mfumo huu wa sasa ambapo mawaziri na baadhi ya watendaji wakubwa wanatokana na hao hao wabunge, unategemea waziri wa maji awe anaishi Mfaranyaki (au mkuu wa mkoa dodoma awe anaishi Masasi), wakati serikali kuu ipo DSM ?. Na utawezaje kulazimisha wengine waishi majimboni, na wengine no say kwa sababu ni mawaziri au wana dhamana flan ?

Una elimu gani Mfuluto manake unaongea kama kibaraka anayewakilisha kila anachoambiwa? Wewe ni masikini wa akili na uko radhi kutetea system mbovu ili mradi maisha yanasonga.Si ajabu ni mmoja wa wale wanaoridhika na vitenge, kofia na pilau na kutetea upupu eti you care about end product..what a looser! Mambo ya msingi ni pamoja na mbunge kuwa karibu na wananchi wake bila hivyo maendeleo ya kweli hayapo.We are trying to analyse how the MP's can be effective and how can this happen if he/she live far away from his/her constituency? Kufanya kazi bega kwa bega nina maana ya kuzunguka maeneo ya jimbo,kukagua miradi, na kuwasikiliza wananchi but as what all short minded folks like you umekurupuka na kejeli za paja kwa paja (sign of ignorance! and probably iliteracy! and lets be frank you really didnt know what i meant? thats pity).Hoja sio kulazimisha bali tuangalie moral and ethics...Wajibu hautekelezeki kirahisi unapokuwa mbali na eneo lako la kazi.Mifano michache ya wanaotekeleza wajibu haitoshi kufuta ukweli wa wengi walioshindwa kutekeleza wajibu. Wake up..
 
Ukosefu wa maendeleo kwenye majimbo mengi kwa hakika huchangiwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kutokujua shida za kweli majimboni kwao.

Watajuaje na wao wanaishi Dar es Salaam?
 
Wewe KIlembwe kweli!!! Tatizo lako unasahau kuwa wabunge wengi ni wa CHAMA chako hivyo unavyozungumzia wabunge wangapi basi ulitakiwa ujue kuwa Wabunge wengi wa chama chako hawana nia ya dhati ndio maana wengi wao hawana nyumba majimboni mwao! Kwa taarifa yako si dhambi mbunge kuwa na nyumba DAR au mbali na Jimbo lake! Ila Walau awe na nyumba Jimboni kwake na muda mwingi autumie jimboni kwake. Kwa taarifa yako zaidi ya 75% ya Wabunge wa CDM walioshinda majimbo yao wanakaa Sehemu husika ukilinganisha na chama chako!

Kaka Mageuzi, kwanza hebu tuweke records sawa, mimi si mwanachama wala shabiki wa Chama Cha Muungwana kama hivyo ndivyo ulifikiri kwa vile tu nimesema sio wabunge wote wenye nyumba kwenye majimbo yao ya uchaguzi, ona wewe mwenywe umesema zaidi ya 75% ya wabunge wa CDM wana nyumba kwenye majimbo yao ya uchaguzi why not 100% si umeona hayo ni mapungufu! Mimi nafikiri suala lisiwe kuwa na nyumba, nikiwa na maana ya mbunge kumiliki nyumba katika jimbo la uchaguzi, suala ni anuani, je mbunge ana address ya uhakika katika jimbo lake, na maana yangu hapa ni kuwa hata kama ana nyumba ya kupanga mradi tu wapiga kura wake wanajua kuwa tukimtaka mbunge basi tunaenda mahali fulani hapa jimboni tunampata. Zitto Kabwe wakati anachaguliwa kwa mara ya kwanza kule Kigoma alikuwa anaishi kwenye nyumba ya wazazi wake, huwezi sema ile ni nyumba yake ila ni anuani yake hilo ndio muhimu. kutumia muda mwingi jimboni si lazima uwe na nyumba hapo, ni wabunge wangapi wana nyumba katika majimbo ya uchaguzi na kila siku tunawasikia na kuwaona Dar na sehemu zingine za miji mikubwa? mfano wachaceh tu, Shibuda (CDM), Mrema ((TLP), hamd rashid, chenge, EL RA, Sitta, Mbowe, Zitto, Cheyo, wote hawa wanaishi Dar je wanawakilisha majimbo gani dar? na wote hawa wana nyumba kwenye majimbo yao!
 
bora hao wa tarime walizaliwa huko......mbona morogoro,singida , rukwa, tabora wanawahusudu waasia (akina rostamu)kwenye ubunge km vile ni wazawa kuliko hata watoto wao ambao serikali ya kikwete inawakamua kwa kuwasomesha kwa ghjarama kubwa lakini bado wanabaki kusujudia rangi................wana watoto wengi tu wanaoweza kuwasaidia na wanaojhua vema matatizo yao lakini wanajidharau wenyewe........waache hao wa tarime nk walienda kupata maarifa na wanarudi na jipya sudhani km kuna shida hapo.....ni sawa tu na mtz kwenda kutafuta maarifa ng'ambo baada ya miaka mingi anakuja tunampa uongozi sembuse dar-tarime?
 
Hizi nafasi za kugombea huwa hazitabiriki, hivyo mtu yeyote anaweza kuwa anaisha nje ya mkoa aliozaliwa na hii kwa vyovyote itamlazimisha apange au ajenge nyumba kama watu wengine wote wanavyofanya wanapokuwa mbali na sehemu walipozaliwa, sasa inatokea uchaguzi umefika akajitokeza na kwa bahati akichaguliwa, hakutakuwa na jinsi zaidi ya mbunge huyo kupanga kama hakuwa ameweza kujenga eneo alilogombea. Kumbuka kuwa kwa mujibu wa katiba mtu yeyote anahaki ya kugombea jimbo lolote bila kujali rangi, kabila n.k hivyo kwa kigezo hicho usitegemee kuwa kila mbunge atakuwa na makazi yake binafsi jimboni kwake.
 
Hapo sasa tunaona mabadiliko ya katiba hayakwepeki kabisa iwapo tunahitaji maendeleo ya kweli katika Tanzania yetu,kwani hilo la wabunge kuwepo nje ya majimbo yao kimakazi ni case ambayo pia inatokea tunapochanganya watendaji wa serikali na wanasiasa...Anangalia mawaziri wote ambao basically wanatokana na wabunge waliochaguliwa kuwawakilisha wananchi wao bungeni..inawezekana initially alikuwa anamakazi yake Jimboni lakini baada ya kuzawadiwa Wizara, Jimboni kuonekana kwake inabaki History hivyo huyu mtu hawezi kuwa current na matatizo ya watu wake .....Hivyo ama kwa hakika inabidi Katiba tunayoililia ni muhimu ikatenganisha WanasiHasa na Watendaji wa serikali.
 
HAWA NDIO WATANGANYIKA BONGO LA-LA-LA A LA AAAAAAAA!! YAANI MBUNGE WAO AKISHACHAGULIWA WATAMWONA TENA WAKATI WA UCHAGUZI AU WAKATI AMESIKIA KIONGOZI WA SERIKALI ANATEMBELEA JIMBONI MWAKE NDIO UTAMWONA ANAJISHEBEDUA KUWA KARIBUKARIBU! HII INATIA SHAKA KAMA KWELI WANANCHI WENGI WATANZANIA HUWA WANAJUA WANACHOKIFANYA WAKATI WA KIPIGA KURA!
>>> Mfano mtu kama huyu Mbunge wa Tarime sijui anaitwa '' Nyambari Nyagwine''....Anaishi Dar es saalaam ni lini atajua matatizo ya wana TARIME? .....Ndo maana sishangai kusoma habari zake kwenye gazeti la Mwananchi la leo 03/01/2011 Anakutana na wajumbe wa CCM kawe kuwauliza kwa nini Jimbo la KAWE Limechukuliwa na wapinzani (Chadema) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! JE HAYA NDO WANA TARIME WALIYOMTUMA??????????????? Watu kama hawa 2015 waogopwe kama UKoma......

huyu mbunge wa tarime walichakachua kura lakini alikuwa atakiwi kwa wanatarime
 
huyu mbunge wa tarime walichakachua kura lakini alikuwa atakiwi kwa wanatarime

Pia ni bingwa wa kuchakachua elimu through vijitabu vyake vya maswali na majibu ya mitihani ya sekondari.Wanafunzi wa sekondari hawasomi vitabu bali wanasoma hivyo vichapisho na matokeo yake ndio generation hiyo ya kukariri.
 
bora hao wa tarime walizaliwa huko......mbona morogoro,singida , rukwa, tabora wanawahusudu waasia (akina rostamu)kwenye ubunge km vile ni wazawa kuliko hata watoto wao ambao serikali ya kikwete inawakamua kwa kuwasomesha kwa ghjarama kubwa lakini bado wanabaki kusujudia rangi................wana watoto wengi tu wanaoweza kuwasaidia na wanaojhua vema matatizo yao lakini wanajidharau wenyewe........waache hao wa tarime nk walienda kupata maarifa na wanarudi na jipya sudhani km kuna shida hapo.....ni sawa tu na mtz kwenda kutafuta maarifa ng'ambo baada ya miaka mingi anakuja tunampa uongozi sembuse dar-tarime?

Man are you sure with you dimensions? Refer to the main point please!
 
Back
Top Bottom