Mbunge kuishi nyumba ya kupanga ni halali kwenye jimbo lake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge kuishi nyumba ya kupanga ni halali kwenye jimbo lake?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by zamlock, Jan 1, 2011.

 1. z

  zamlock JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mfano mbunge wa tarime kapanga na makazi yake yako dar es salaam je inakuaje muda wake wote ameishi dar alafu apate ubunge tarime, ni kitu gani huwa kinatokea kwa wananchi wanao amua kumpa kura mtu ambaye wanajua kabisa akishapata uongozi anarudi kwenye makazi yake ambako amezoea na kwa shughuli zake zote
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sheria na kanuni za uchaguzi zinaruhusu mbunge kuwa na makazi nje ya jimbo
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Agree with you, its so obvious the chap is not convinced that is the resident of that place. So, how would you expect him to know your problems deep down if he considered himself on the transit.

  People wake up
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  sawa sijakata juu ya hlo lakin kumfahamu mtu kuwa anashida lazima uwe naye karibu na kubaini matatizo yake haswa kwa wananchi ni vyema ukawa nao karibu na kubaini matatizo yao ili uweze kuwatatilia hilo linajulikana
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wapo wengi! mbunge wa babati, igunga, singida mjini, n.k
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mbona balozi wa nchi ana makazi nje ya nchi yake na anatoa huduma na kupeleka maendeleo nchini mwake? it works like that
   
 7. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  miss kuna tofauti kubwa katika kufananisha kwako.balozi kazi yake ni kuangalia maslahi ya taifa lake katika nchi husika na kushughulikia wananchi wa nchi yake katika nchi anayofanya kazi.lakini mbunge anachaguliwa kuyawakilisha matatizo ya wananchi katika sehemu husika hasa bungeni, kama kazi yake ndo hiyo akikaa nje ya jimbo lake atayajuaje matatizo ya wananchi wake?
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sasa ndugu, mfano tujiulize; balozi akikaa nje ya nchi yake atajuaje maslahi ya nchi yake? mi naona tofauti ya kazi hizo mbili iko kwenye contents tu, lakini they all work in similar manner. ingawa kwa balozi kupewa makazi huko nje anakoishi ni stahili kwa mbunge is presumed kwamba due to geographical convenince anaweza kufanya maneuvre ya mahali pa kuishi na kutekeleza vyema wajibu wake kwa wapiga kura wake
   
 9. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  kazi ya balozi ni kukaa nje ya nchi yake na kutekeleza wajibu wake huo nje ya hiyo nchi yake.hata majukumu yake ni yale yanayohusiana na hiyo nchi alikotumwa ndo maana hata siku moja balozi wa marekani tz hawezi kukaa marekani lazima akae tz ili atimize wajibu wake vizuri.miss huku iringa mbunge aliyopita kapigwa chini kwa ajiri hiyo yaani alikuwa hapati muda wa kuwasikiliza wananchi wake coz hakai iringa.
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  asante kwa mchango wako huo ndugu yangu kwa kukmuelewesha
   
 11. z

  zamlock JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mfano mbunge wa babati ambaye alikuwa tarime mh chambiri naweza sema nimemkubali kwa sababu amekwenda pale muda mrefu sana na akawafanyia mambo makubwa sana wakazi wa pale kabla awajampa ubunge na amejenga na makazi yake kahamishia pale na anayajua matatizo ya pale lakini wengine wanakuja kuchukua uongozi alafu wanarudi jijini kula kuku
   
 12. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Balozi anawakilisha nchi yake ugenini hivyo lazima akae huko ugenini anakowakilisha lakini kule anapotoka lazima ana makazi ya kudumu.Ingekuwa ajabu balozi kuwakilisha nchi ugenini wakati yeye akiwa katulia nchini kwake manake jukumu lake kubwa ni kuiwakilisha nchi ugenini.Wananchi waishio ugenini wakitaka kuwasilisha matatizo yao wanaenda kwa balozi ambaye anaishi huko. Mbunge anapokuwa hana makazi ya kudumu jimboni kwake na wakati jukumu lake kubwa ni kuwawakilisha wananchi bungeni then anawawakilisha vipi wananchi wa jimboni kwake? Wananchi wa jimboni kwake ambao ndio wanaomtuma bungeni wamtafute wapi pindi wanapohitaji kuwasilisha matatizo yao bungeni? Wamfuate Dar(mfano)? Au ni sawa hata akiishi Nairobi au Lagos kwa kuwa tu ana uwezo wa kuja mara moja moja katika jimbo lake kwa kufikia hotelini au kwenye nyumba ya kukodi?
   
 13. m

  mzambia JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona dr nchimbi kwetu huku songea baada ya kutaka kugombea ubunge ndo alinunua nyumba ili aonekane anakaa mateka lkn kabla ya hapo hata songea alikuwa hapajui

  ndo si haswa hizo.
   
 14. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  issue co sheria au kanuni zinasemaje_kinachozungumzwa hapa ni kwamba utambuz wa masuala yanayoikabili jamii yake utategemea kuambiwa tu wakat angekuwa akiish jimbon angekuwa na ufahamu mkubwa_actually wa kulaumiawa co wananch bali sihasa za nch yetu_hao ni wale walioletwa kwa kushikwa mikono na wakubwa otherwise wasingekuwa na ujasiri huo_mfano ni mbunge wa shinyanga pia, wakat wa kampen ndo amepanga nyumba shy_na amepelekea machafuko makubwa lkn vigogo wakalazimisha_so he is there for interest of big potatoes
   
 15. P

  Percival JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,566
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Bila shaka ni galoni la mapuya ndio lifanyalo hao wananchi kumchagua mtu wasiemjua au wanajua hatakua na maslahi kwao. Pamoja na demokrasia kusonga mbele ni muhimu kwa wapiga kura pia kuelemika na kufahamu nini wanakitaka kutoka kwa viongozi wao.
   
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  :bump:ki ukweeli sijawahi on posts zako zenye maana hata siku 1?balozi akichguliwa ofisi yake si lazima iwe katika nchi aliyochaguliwa?
  swaali? ofisi ya mbunge wa mara ipo dar es salaam,hebu fungua ubongo wako na ujaribu kutwist kwa kutumia koreo na bisbis
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  miss Judy,unajua kweli JD ya balozi au umeamua kutupa mfano tu! Unajua kuwa baloz na mwanasiasa hata hawaendani kimalengo? Politician Vs Diplomat? Nadhani inabidi tukubali kuwa mwakilishi wa wananchi/mbunge anabidi awe kwenye kundi ilo la wananchi ili aelewe anachoenda kusema unlike diplomat anayetumwa hata kwa mawasiliano ya email au hata kwa fax vitu gani akapresent hata bila kujua vinaimpact gani au vinalenga nini. Lastly bora na wewe umekumbuka kuwa balozi anaishi sehemu ya kazi ilipo,hawezi kuwa balozi wa Kenya amepelekwa China lakini makazi yake akayaweka South africa! Atakaa sehemu husika,kwa mfano wako kama mbunge angekaa Dodoma nahisi swali letu lingekuwa vinginevyo,lakini akae dar for what?Nakushukuru Judith!
   
 18. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kwa mfumo wa sasa wa bongo, sioni kama hiyo ni issue. At the end of the day ili mradi ana-deliver kwa kuwatumikia wananchi wake na kuleta maendeleo. Kukaa huko kijijini na kunywa nao kimpumu kila siku inaweza kuwa sio suluhisho la kuonekana ni mbunge mzuri na kuwatumikia anaowawakilisha.

  Wapo wabunge ambao nawajua, hawakai ktk majimbo yao lakini wana coordinate vizuri shughuli za maendeleo ya maeneo yao, na kutatua kero za wapiga kura wao. Kumbuka siasa za bongo ni fitna na ushap wa kufuatilia mambo yako. Ukitegemea kuishi huko Kufakunoga, ambako simu ni zile za kukoroga, na ipo moja tu kwa DC, ndiyo huwe unawasiliana na wizara, idara n.k ktk kufuatilia mambo ya jimbo lako, hakuna kitakachofanyika kwa wakati.

  Kujua matatizo ya wananchi wako, ktk inji yetu wala sio lazima uishi hapo jimboni.
   
 19. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Kind of contradictions katika comment yako.Kama simu ni moja na hali za wananchi ni duni na yeye hawezi kuishi katika hali hiyo na hawezi kuibadilisha... huoni tayari mbunge ameshindwa jukumu la kuwaletea wananchi wake maendeleo? ikiwepo mawasiliano na miundombinu!.Awaachie wanaoweza kukaa huko na kuondoa hali umasikini kwa kufanya kazi bega kwa bega na waliomchagua.Kwanini asigombee jimbo lenye simu kila kona ili awasiliane vizuri na wizara? Kama angekuwa anaishi huko jimboni kwake lazima hayo matatizo yangemgusa pia na angetafuta solution right away.
   
 20. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  ....Sio contradiction yoyote kwa sababu sio kosa la mbunge kuwepo kwa simu moja ya kukoroga. Unaongelea "hewa" ...Awaachie wanaoweza kukaa huko na kuondoa hali umasikini kwa kufanya kazi bega kwa bega na waliomchagua.Kwanini asigombee jimbo lenye simu kila kona ili awasiliane vizuri na wizara? Kama angekuwa anaishi huko jimboni kwake lazima hayo matatizo yangemgusa pia na angetafuta solution right away.

  ...Ndiyo shida ya umasikini na ndg yake umbumbumbu..... maana hata priority hatuzijui na badala ya kuangalia mambo ya msingi tunaanza kuhangaikia mambo ya nani anaishi wapi ect. Kazi gani hizo za bega kwa bega au paja kwa paja ambazo unategemea hao masikini wazifanye ili kuleta hayo maendeleo ?

  Binafsi hata kama mbunge anakaa nje ya inji, i dont care kama wajibu wake anautekeleza. I care about the end product- period na sio anaishi wapi ect.

  Na kwa mfumo huu wa sasa ambapo mawaziri na baadhi ya watendaji wakubwa wanatokana na hao hao wabunge, unategemea waziri wa maji awe anaishi Mfaranyaki (au mkuu wa mkoa dodoma awe anaishi Masasi), wakati serikali kuu ipo DSM ?. Na utawezaje kulazimisha wengine waishi majimboni, na wengine no say kwa sababu ni mawaziri au wana dhamana flan ?
   
Loading...