Mbunge Shonza - Miaka Miwili ya Rais Samia Madarakani Imeleta Maendeleo Makubwa katika Jimbo la Mbozi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
"Wengine wakasema Chama Cha Mapinduzi kitakoma kwasababu Rais ameruhusu mikutano ya hadhara. Mimi nasema, miongoni mwa watu ambao wamekula hasara na tamko la Rais kuruhusu mikutano ya hadhara ni vyama vya upinzani" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sisi Chama Cha Mapinduzi ndiyo tunaotekeleza Ilani, sisi tunayo mengi ya kuja kuongea. Hatuji kwenu kuomba kura au kufanya kampeni. Mlituchagua mwaka 2020, tunapokuja tunasema tuliahidi haya na Tumefanya haya, tumefikia hapa, haya bado, haya yapo kwenye utekelezaji. Hiyo ndiyo kazi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Changamoto kubwa ya Wanawake wa Mkoa wa Songwe, Jimbo la Mbozi, hususani Mlowo ni suala la Maji. Hatusemi Serikali imemaliza Changamoto ya Maji lakini tunaona na kuthamini jitihada za Serikali za kuhakikisha tunamaliza Changamoto ya Maji" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais alisema ajenda yake namba moja ni kumtua Mama Ndoo kichwani. Alivyoingia madarakani akasema bado ajenda yake ipo palepale. Tumeendelea kumuona Waziri wa Maji, Aweso, amekuja mara nyingi Jimbo la Mbozi kuzindua miradi ya Maji" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tulishawahi kuwa na Mbunge Jimbo la Mbozi, kazi yake Bungeni ilikuwa ni matusi tu; kumtukana Rais, kutukana Mawaziri, kutukana Wabunge. Mtu unayemtukana unategemea akuletee Maji, Barabara. Bungeni Mbunge aliyekuwa anaongoza kwa matusi alikuwa anatoka kwenye Jimbo la Mbozi, ndiyo maana kwa miaka mitano Jimbo la Mbozi halikuwa na maendeleo" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tumepata Rais mchapa kazi, tumepata Rais ambaye ndani ya Miaka Miwili aliyokaa madarakani amefanya mambo makubwa sana Majimbo yote ya Mkoa wa Songwe. Tulikuwa na changamoto ya madarasa na Shule, ilifika kipindi watoto wanatoka umbali mrefu wanavuka Barabara kwenda kufuata Shule" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tulipoteza watoto wengi maana walipovuka Barabara wengi walikuwa wanagongwa na magari na Bajaji. Rais wetu ni Rais wa wanyonge alipoingia madarakani ndani ya Miaka Miwili kwenye Jimbo la Mbozi tumepata zaidi ya Bilioni 4 ambapo hizo zote zimekwenda kwenye Mashule" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Wazazi bado wanaendelea kulalamika kwamba Serikali iondoe Ada kwenye Vyuo vya Kati, Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan, tun Rais ambaye ni msikivu. Kwenye simu yangu nina meseji zaidi ya 200 ya Wazazi wa Mkoa wa Songwe, wanasema Shonza tusemee huko Bungeni, Rais aondoe Ada kwenye Vyuo vya Kati na sisi Wabunge kazi yetu ni kusema na tumekuwa tukisema pale Bungeni" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Rais wetu ni msikivu, anayewajali watanzania, akasema hapana, kama nimeweza kufuta Ada kidato cha kwanza mpaka cha Sita, sitaweza kushindwa kufuta Ada kwenye Vyuo vya Kati. Bajeti iliyomalizika Julai 2023, Rais kupitia Wizara ya Elimu ametoa tamko la kuondoa Ada kwenye Vyuo vya Kati" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe.






 
Back
Top Bottom