Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,898
- 942
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Ileje Kata ya Ibaba kwa lengo la kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero za wananchi na kuwapa mrejesho wananchi kuhusu utendaji kazi wa Serikali.
Katika ziara yake, Mhe. Juliana Shonza aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka TANESCO, RUWASA ili wajionee wao wenyewe kutoka kwa wananchi changamoto wanazopitia na kutoa majibu sahihi.
Mhe. Juliana Shonza alimtaka afisa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Songwe kueleza kwanini Watu wanalala giza wakati Rais Samia Suluhu ameshatoa maagizo kwani Mmeweka alama lakini hakuna nguzo wala hakuna umeme. Mna mpango gani?
Vilevile, Mhe. Juliana Shonza alimuomba Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe kuzungumza kuhusu maji kwani haiwezekani wananchi wakakosa maji kwasababu ya kukosa Pampu tu.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza akizungumza na Wanawake wa UWT Ileje amepongeza ujenzi wa Ofisi za Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Ibaba
Aidha, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefurahishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 na kusema kuwa wao kama viongozi wanatembea vifua mbele. Miaka ya nyuma CCM Tunduma tulinyanyasika sana, hata kuvaa nguo ya CCM ilikuwa ni mwiko.
"Kuna muda najiuliza hivi Rais Samia hizi fedha zote anayatoa wapi, kwasababu hakuna Jimbo au Kata ambayo utaenda usikutane na miradi ya Shule. Mbozi kuna shule ya msingi imejengwa, tumesema iitwe Mama Samia, utajua ni Chuo lakini ni shule ya msingi ya kisasa" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe
Mhe. Juliana Daniel Shonza amemshukuru Diwani wa Kata ya Ibaba usimamizi mzuri wa ujenzi wa barabara kwani barabara zinapitika tofauti na Mwanzoni Barabara zilikuwa hazipitiki kirahisi.