Mbunge wa Jimbo la Makete, akichangia katika Bunge la 13, Mkutano wa Pili, Kikao cha 6, ameeleza kuwepo kwa mifuko ya vijana katika wizara mbalimbali licha ya kuwepo kwa Wizara rasmi ya Vijana. Amesema kuna zaidi ya mifuko 70 katika wizara tofauti inayopokea fedha kwa ajili ya vijana.
Amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mfuko mmoja wa vijana ili kurahisisha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha hizo, akibainisha kuwa ripoti zinaonyesha serikali imekopesha zaidi ya Shilingi trilioni 3.5 kupitia mifuko hiyo, lakini bado vijana wanalalamikia ukosefu wa ajira.