Mbunge Edward Lekaita Akabidhi Ambulance Hospitali Ya Wilaya Ya Kiteto na mifuko 900 ya saruji katika kata za Jimbo la Kiteto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoa wa Manyara, Mhe. Edward Ole Lekaita amekabidhi Ambulance đźš‘ mpya kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto na kuwataka kulitunza ili liwanufaishe.

Vilevile, Mhe. Edward Ole Lekaita amekabidhi Mifuko 900 ya Saruji kwa Kata ya Bwawani (Mifuko 50), AMCOS Matui (Mifuko 100), Kata ya Sunya (Mifuko 265), Kata ya Partimbo (150), Kata ya Njoro (Mifuko 35), Kata ya Kibaya (Mifuko 35), Kata ya Kaloleni (Mifuko 20), Kata ya Engusero (Mifuko 70).

Pia, Kata ya Sunya iliyopokea Mifuko 265 ya Saruji imepelekwa Zahanati ya Olgira (15), Lobosoit (50), Ndilali (50), Shule Shikizi Natushu (50), Shule ya Msingi Mbikasi (50) na Shule ya Msingi Chang'ombe (50)

Mifuko ya Saruji aliyokabidhi Mhe. Edward Ole Lekaita ni kutokana na ahadi aliyoahidi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kiteto wakati akifanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amezungumza na viongozi na kusikiliza kero zilizopo.

WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.21.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.27.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.27(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.43.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.57.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.58.05(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.56.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.51(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.49(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.49.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.46(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-01 at 16.52.45.jpeg
 
Back
Top Bottom