Kero ya Maji Kandiya Haitanishinda - Mbunge Lekaita wa Kiteto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

KERO YA MAJI KANDIYA HAITANISHINDA - MBUNGE EDWARD LEKAITA

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita amewaambia wananchi wa tawi la Kandiya Kitongoji cha Kona kuwa changamoto ya Maji waliyonayo haitamshinda kuitatua na ameahidi kushirikiana na RUWASA kutatua changamoto hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita amewataka viongozi wote wa Kitongoji cha Kona, Kijiji cha Kijungu, Kata ya Kijungu kuhakikisha wanatatua migogoro ya Mashamba, Malisho na Mapalio ili uwe mfano mzuri kwa maeneo mengine.

Mwenyekiti wa Kijiji kwa kushirikiana na Kitongoji cha Kona, Kijiji cha Kijungu, Kata ya Kijungu wamepitisha na wamemuomba Mbunge Edward Ole Lekaita afuatilie TAMISEMI maombi ya wananchi ya muda mrefu kwani wameomba Kandiya kuwa Kitongoji tangu mwaka 2003.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kijungu amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita kwa kutekeleza Miradi iliyopo kwenye Ilani hivyo kuwaheshimisha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ujumla.

Nao wananchi wa Loosikito wamempa Mhe. Edward Ole Lekaita zawadi ya Kiti cha Asili kama Ishara ya Baraka katika uongozi wake na kumuombea dua. Pia, wamemzawadia Vazi la heshima la kimasai kama ishara ya Upendo baada ya kufika kwao kwa mara ya kwanza.

Aidha, Mhe. Edward Ole Lekaita ameambatana na Diwani wa Kata ya Loolera na kutembelea Josho na kukagua Maendeleo ya Ukarabati huku Mbunge akiwataka wananchi kulinda vyanzo vya Maji vilivyopo na vitakavyoanzishwa.

Mhe. Edward Ole Lekaita akiwa na Diwani wa Kata ya Loolera na viongozi mbalimbali wa Kata wamekagua ujenzi wa Madarasa kwa nguvu za Wananchi ambapo amewapongeza wananchi na kuwachangia Mifuko 70 ya Saruji.

WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.50.26(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.25.jpeg
    1.1 MB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.50.24.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.50.24.jpeg
    1 MB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.25.jpeg
    1.1 MB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.23.jpeg
    844.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-21 at 11.49.22.jpeg
    547.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Video 2023-08-22 at 06.51.58.mp4
    68.3 MB
Back
Top Bottom