Mbunge Atupele Mwakibete amshukuru Rais Samia, asema Busokelo Sekta ya Afya Wamepiga Hatua Nzuri Sana

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Namshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeniteua tarehe 08 Januari, 2022 kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi. Alituheshimisha sana Vijana, alituheshimisha sana wana Busokelo na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla. Ninaamini nilifanya kazi kwa Weledi, Uaminifu na nina hakika bado nitaendelea kukitumikia Chama changu, nchi yangu na Jimbo la Busokelo kwa wananchi wangu" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Kuna miradi mingi ambayo Mheshimiwa Rais ametuletea katika Jimbo la Busokelo na Mkoa wa Mbeya. Mwaka wa fedha 2022-2023 kwa fedha tu za maendeleo ni zaidi ya Shilingi 6,537,520,843 zimekuja Busokelo. Mkisikia Barabara, Maji, Vituo vya Afya, Zahanati zimeletwa fedha hizi kupitia Mwigulu Lameck Nchemba" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Tumepata kuanzia Julai 2023 mpaka Septemba 2023 Shilingi Bilioni 2,310,548,905 zimekuja ndani ya Halmashauri ya Busokelo. Ndiyo Zahanati 8 mpya zimejengwa na Zahanati 3 zimekarabatiwa, kwa ujumla Zahanati 11. Vituo vya Afya 4, Hospitali ya Wilaya imeshaanza kufanya huduma za upasuaji na zimegharimu zaidi ya Bilioni 2.8, katika sekta ya Afya Tumefanya vizuri sana" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Katika ujenzi wa jengo la Halmashauri tumepata fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 6,387,469,120. Jengo hili litaendelea kutumika lina vyumba 205, ni jengo la kisasa ambalo katika Halmashauri zote nchini halipo, lipo Busokelo tu" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Shule za Msingi 62 zimekarabatiwa, Sekondari 21, Barabara inayoenda Ipelele - Kitulo - Njombe Kilomita 9. Waziri wa Ujenzi naamini utasema neno ili Barabara hii waiweke katika kiwango ambacho itapitika wakati wote. Wananchi walikuwa wanasafiri Kilomita 150 kwenda Ikonda, sasa watatumia Kilomita 9, ni kwasababu ya juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Kipaumbele cha kwanza Busokelo ni barabara, Kipaumbele namba pili ni Lami, Kipaumbele namba tatu ni Lami ndiyo hitaji letu kubwa kwa sasa Busokelo" - Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo

"Ndugu zetu wakifariki Bonde la Mwakareli tunalazimika kuwazika siku hiyo hiyo kwasababu hatuna Mochwari ya kuhifadhia maiti. Tunaomba Mochwari ijengwe, wodi za watoto na wodi za Wazazi zijengwe katika kituo cha Afya Mwakareli pamoja na kumalizia vituo vya Afya vya Isange, Mpata, Lupigi, Lufilo, Nkaba, Kisegese, Kambasegela. Wananchi wamejitahidi kujenga, sasa ni maboma, wanahitaji nguvu ya ziada ya Serikali ili vikamilike" -Atupele Mwakibete, Mbunge wa Jimbo la Busokelo.


 
Back
Top Bottom