Mbunge atamka Waadilifu lakini JK Rais wetu hayumo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge atamka Waadilifu lakini JK Rais wetu hayumo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Apr 23, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Posted Date::4/23/2008
  Mbunge aliambia Bunge viongozi waadilifu serikalini ni Dk Shein, Pinda
  Na Muhibu Said, Dodoma

  SIKU moja baada Mbunge wa Vunjo), Aloyce Kimaro (CCM), kumtuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe, Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuhusika katika ufisadi wakati wa ununuzi wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwanji(CCM), naye ameibuka na kuishambulia serikali bungeni, akisema imejaa mafisadi kasoro viongozi wawili.


  Lwanji ambaye alikuwa akichangia Muswada wa Umeme wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007 uliopitishwa baada ya mjadala mkali Bungeni, mjini hapa juzi jioni, alisema haoni kiongozi mwingine muadilifu aliyebaki isipokuwa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Pia alimtaja Waziri Mkuu Mstaafu, Rashid Kawawa katika orodha ya waadilifu.


  Alisema hivi sasa idadi ya mafisadi imekuwa ikiongezeka kila kukicha na kwamba njia pekee ni kwa viongozi mafisadi kukataa uteuzi na kuongeza kuwa ni aibu kuona viongozi wengi wanajitumbukiza katika vitendo vya ufisadi,

  ambao alisema ni mwelekeo mbaya.


  �Kila kukicha idadi ya viongozi mafisadi inaongezeka, viongozi waadilifu wanapungua kila siku. Mimi nadhani kama ukiteuliwa na Rais na kuona una madudu ni heri umweleze Rais kwamba nafasi hiyo huiwezi,� alisema Lwanji na kuongeza:


  �Wanapoandikwa kwenye magazeti wanalalamika�hivi unataka uandikwe kwa mazuri tu?� alihoji.


  Akiuzungumzia muswada huo, Lwanji alisema wawekezaji katika sekta ya umeme watakaokuja nchini, wengi wao ni wabovu na kwamba wanakuja kuvuna.


  �Wengi wao ni reject (waliokataliwa)na kwa bahati mbaya wakija hapa wanakutana na viongozi wa ten percent (asilimia kumi),� alisema.


  Lwanji aliitumia nafasi hiyo kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Kojani, Haroub Othman aliyoitoa Jumatatu wiki hii kuwa kuna umuhimu wa kuunda timu maalum ya Bunge ya kushughulikia mafisadi.


  Wakati huo huo, Muswada wa Sheria ya Umeme ya Mwaka 2007, juzi jioni ulipitishwa na wabunge baada ya mjadala mkali.


  Kilichomwokoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja hadi Muswada huo ukapita, ni Kanuni za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kuupinga vikali.


  Wabunge waliombana Ngeleja kutoa maelezo ya ziada ni Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP). Wengine, ni Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango (CCM), Mbunge wa Ludewa, Prof Raphael Mwalyosi (CCM) na Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga (CCM).
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kampuni iliyosimamishwa mkataba wa baggage handling airport za South Africa inakuja Tanzania.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kumbe hata CCM wenyewe wanajua kwamba Shein ndiye pekee msafi na Mkuu wa Kaya ni wale wale ?
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hata huyo Shein usafi wake ni debatable,

  Kama anaweza kukaa na mafisadi meza moja bila kuyasema naye ni wale wale tu, labda mseme jamaa muoga tu.

  Ndiyo hao hao kina Mkapa wenye nidhamu ya woga, alivyokuwa foreign alikuwa anarudisha fungu serikalini, kuja kuwa rais kalamba mgodi mzima bei chee bila collateral!

  Huyo Pinda naye kauli zake zinatuacha hoi, tunasahau kuwa ili kuwa kiongozi mzuri ni zaidi ya kuwa safi, inabidi uwe na uwezo wa kuongoza.Pinda hana uwezo na hata kama akiwa msafi kama theluji mpya uongozi wake utakuwa mwekundu kama bendera.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi bado nataka tamko la akina Mtu wa Pwani , Kada na kundi lake.Hivi kada yuko hapa ? Mpuuzi shy naye anaweza kuja hapa longo longo zake .
   
 6. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2008
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  take five mp huyu!! time will tell for sure
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wanaanza kuamka ama wamesha jua CCM itawatema so wanajenga mazingira ya kuingia Upinzani ili wakafe nao huko ?By the wau JK hapendi challenge naamini Makamba lazima awaite na kuwapa onyo ama spika mwenyewe .
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  kwa mtu anayepewa mikasi kuna uwezekano gani wa yeye kuwa fisadi?
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huyo Mbunge Amezungumza Kwa Utashi Wake Na Hakuna Mtu Wowote Anayemuunga Mkono Kwa Msemo Wake Huo Yeye Ana Sema Tu

  Kama Kweli Shein Angakuwa Msafi Basi Asingeruhusu Watoto Wake Wengi Kuwa Na Uraia Wa Uingereza Huyo Mbunge Anajua Kweli Hili Suala ?

  Shein Sio Mzalendo
   
 10. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hakuna mtu safi ccm,labda anna kilango!!! na marehemu wetu wapendwa kolimba,nyerere,amina chifupa,ngoja nikwambie wewe ccm,watu safi uhai wao ni mdogo sana kuishi,kwani watasema ukweli na watateketezwa kwa nguvu za giza na mafisadi.........hivi unajua mafisadi wengi hawamuogopi hata mungu wao,kwa hiyo kutoa roho ya mtu kwao ni kitu kidogo sana.....
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lunyungu Pls Usiwe Una Niita Mpuuzi Naomba Usiwe Unanidhalilisha Kumbuka Sijawahi Kutamka Neno Hata Moja Au Tusi Hata Moja Dhidi Yako

  Kwa Ufupi Nimeenda Kituo Cha Polisi Na Hakuna Mtu Kama Wewe Aliyeonekana Pale Wala Kwenda Kuulizia Suala Lako

  Tafadhali Wacha Kusema Uwongo Katika Jukwaa Hili Heshimu Maadili
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Lakini imeandikwa hata yule ambae hakupatikana na doa alikula na wezi watoza ushuru.

  Alitembea kati yao lakini hakufanyika mmoja wao!


  BILLAL KAFICHWA WAPI? KIKWETE MTOE TUMSULUBU!
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hii Ni Nchi Ya Amani , Mshikamano Na Upendo Hakuna Kuhukumiana Kila Kitu Kinatasemehewa Kila Kitu Kitasahaulika Na Utaendelea Kuishi Maisha Ya Amani , Uhuru Na Upendo Leo Kesho Na Hata Milele
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Hivi kwa Shein na kutumia ile ofisi yake ya makamu wa rais, je hakuna mambo ya maana anayoweza kufanya zaidi ya kufungua majengo na mikutano?

  Ndio tunahitaji viongozi waadilifu lakini pia wawe innovative na wenye ueleo na ambao wako tayari kukumbatia mabadiliko. Kuwa mwaminifu pekee haitoshi kabisa.

  Binafsi ningetaka Shein atumie huo muda wake kufanya mambo ya maana zaidi kwa jamii.

  Ila kuna mkuu mmoja aliniambia Shein mvivu hasa, sijui kama ni kweli.

  Kwa uadilifu nampa tano lakini ajitahidi na kwenye mengine.
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  RATIBA YA SHENI:

  Saa 10.10 alfajiri anamka

  Saa kumi 11 anaswali swala ya alfajiri

  saa 11: 30 alfajiri anavuta uradi mpaka saa 12

  Saa 12:00 anapata staftahi (kama hajafunga siku hiyo)

  saa 12:30 huyooo ofisini kwa JK au kama JK hayupo basi ofisini kwake...pale anakta magazeti yote yakotayari

  saa 1 asubuhi anasoma magazeti huku computer iko on..siku hizi kaacha kusoma magazeti kwanza

  TANGU MUANZE KUMSEMA NA MIKASI,AMEKUWA OBSESSED NA MA SNITCH WA JF...na inasemkana kuwa PC yake imefanyiwa setting ya JF/SIASA ndio homepage

  Kusoma JF siasa na kucatch up na posters wa ULAYA NA USA inachukua minimum 1 hr

  baada ya hapo anapitia magazeti

  saa 2:30 huyooo anavuta droo yake na kuchukua kitendea kazi chake


  [​IMG]

  safari kwenda ubungo kufungua jengo au tawi la kituo cha mama na mwana

  atafanya na khutba na kukagua nyama huku na kule hii itampeleka peleka mpaka saa 6:30 mchana

  saa 6:45 huyoooanaingia msikiti ulio karibu anaswali sala ya adhuhuri..mle ataka kaa 1 hour

  akitoka hapo atanda kule ofisini lakini mchana huwa hali mpaka bibie ampikie hiyvo wapishi wake hawapati tabu sana naye huyu

  atapitia tena JF kama kawaida yake kwani niye ni addict kama mimi na wewe humu

  atapokea wageni mara nyingi ni wazungu waliomsomesha au wale wazungu wa SCANDINAVIA ambao wanamjua kuwa yeye hana khiyana...


  saa 9:30 mchana atapata mijisimu toka kwa akina Kingunge na wengine wakimpa ushauri au wakimtaka atoe matamko kuhusu UFISADI lakini wapi...

  10 kamili anaswali ofisini mpaka saa 10:30

  baada ya hapo wanakuja akina ENGINEER MOHAMMED na akina LUNYUNGU etio wanataka dili ya tenda ya kumodernise DIA ...kisa MO ni mtu wa kutoka visiwa vidogo vidogo mwenzie na of course LUNYUNGU ni mtoto wa KIJAMAA toka BARA..dakika 30 za mwanzo SHEIN anonyesha yuko so enthusiastic na whoe idea...na anawajibu hivi:

  HEBU NJOONI hapa zungukeni nikuonyesheni kitu kwenye hii computer:

  shein anatype http://www.ctb.go.tz/

  kisha nawaambia "nyie mmekaa nchi za nje lakini internet hamuijui..ingieni hapa mtaona tenda zote zilizotangazwa na mu BID kama watu wengine...mkikosa mnaweza kujaribu tena hivyo hivyo..."

  LUNYUNGU anaona hapa kushakuwa na miyeyusho hivyo anajribu kuaga...ENGINEER MOHAMMED anajaribu kuomba appointment ya nyumbani.....na kama kawaida yake SHEIN alivyo hana khiyana anmkubalia appointment jioni


  ENGINEER MO anaondoka na mwenzie KUNYUNGU huku wakiwa na splitting minds kuwa bora wangeenda kumona CHENGE au hata SAMUEL SITTA au MUSTAFA MKULLO mambo yao yangenyooka kwani wangeulizwa 10% na tenda wangeipata...lakini MO anasema NO SWEAT jioni nitaenda nyumbani kwa SHIEN...kisa eti wapemba wanajuana kwa Vilemba


  saa 2 kamili usiku Engineer MO keshafika na keshapewa misosi ya DRAFTI(unajua tena wenzetu wa visiwani ndio wenyewe kwa kupika)...SHEIN huyo anamchukuwa anamswalisha sala ya ISHA ...na baada ya hapo ENGINEER MO anaulizia tena ile tanda...na kama kawaida yake SHEIN anamletea hadithi ndefuuuu kuanzia ile tenda ya MODE-NI ZESHENI- ya bandari ya UNGUJA mpaka ule mradi wa MTOTO KWA MTOTO kule PAJE NDAME..vyoote vilienda kwa tenda

  ENG Mo anaona keshayeyushwa anaaga ...shein anamwambia atarudishwa nyumbani...

  Huyo ndio MAKAMU WA RAIS WETU MOHAMMED ALI SHEIN...ni BOARER wa kutupwa WABUNGE na MAWAZIRI MAFISADI hawampendi na CCM nao wanaomona ni boara awe hivyo hivyo kwani hawasumbui

   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi ni big fan wa Dr Shein na ningetulia kidogo kama ningemuona akipewa nchi kuiongoza wakati huu wa kipindi cha mpito mpaka huo uchaguzi mkuu ujao!

  Asante GT
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0

  SHEIN NI UPDATE VERSION YA MZEE IDRISSA ABDUL WAKIL
  [​IMG]
  aka BABU


  tofauti ni kuwa SHEIN ni MNOKO...asiyependa makuu
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Weye GT,

  Wewe mwendawazimu kweli kweli! Sasa Mzee wetu wa Mikasi kakukosea nini tena? Yaani nimecheka mpaka ule unga wa mkate wa Sakramenti nimeuharibu!
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Babu au Mzee Kibogoyo?
   
 20. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee poa kabisa, hawezi kubadili mfumo mzima lakini hata mtu wa kawaida anaona alivyojitenga nao.
   
Loading...