Mbunge atamka Waadilifu lakini JK Rais wetu hayumo

mmmh simba akilowana hawi paka jamani, kama kundi la marafiki zako ni simba sizani kama we utakuwa ni ng'ombe...minachoamini anatulia timing ili atupige kisha arudi zake wawi akachokoe chaza.
 
Huyu Dr Shein ni mfano mwingine wa matumizi mabaya ya rasilimali za taifa letu. Ana elimu kubwa sana huyu jamaa, PhD katika molecular biology. Nchi zilizoendelea vichwa kama hivi ndio viliwekwa maabara vikazalisha haya maajabu mnayosikia ya GMO's, cloned organisms, genetic engineering nk. Kuna masikhara makubwa ya aina mbili nimesikia kuhusu Dr Shein, la kwanza nilisikia alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Muhimbili pale) kusomea udaktari wa binadamu, lakini "wanoko" wa enzi hizo ambao nasikia bado wapo wakam-"disco" mwaka wa kwanza tu! Mwaka uliofuata ndio akapata scholarship akaenda nje ambako aliunga nondo juu ya nondo hadi aliporudi na hiyo PhD ya molecular biology. Masikhara ya aina ya pili ni kazi aliyopewa aliporudi, akaajiriwa kwenye Wizara ya Afya Zanzibar kama pathologist (ninavyojua pathologists ni watu kama Prof Shaba ambao huwa wanafanya uchunguzi wa maiti, postmortems na mambo kama hayo)! Baadaye akaingia kwenye tume ya kudhibiti UKIMWI Zanzibar. Yaani hakufanya kazi aliyosomea hata siku moja! Sasa najiuliza madude magumu namna hiyo aliyasoma ya nini, bora angejiunga tu huku kwenye "ungwini"! Baadae akaingia kwenye siasa na sasa ni makamu wa rais, na kina GT hapa wanamkejeli na mkasi, ati ndio kifaa chake cha kazi! Jamani, alikuwa "genius" huyu msimuone hivi na utulivu wake, ni "maakili" yamejazana kichwani humo yamekosa matumizi!
 
ccm sasa wameanza kuamka, muungwana wameshindwa kumuweka kwenye kundi la waadilifu ee....sawa sawa.
hata huyo pinda tuna wasi wasi nae kuwa hali iwapo itatulia kidogo tu atachota vijisenti vyake na yeye.
shein is a totale bore, kuiba ki hivyo hawezi, shy amemsema kuwa kawaachia wanawe wawe na uraia wa uingereza.....hao wanawe waloachiwa are they under 18?
 
Wewe Shy una uhakika gani kwamba huyu mbunge hana wanao muunga mkono?Ok sawa vyovyote vile lakini ujumbe umefika na sasa hivi huyo mjomba yako Ben anakosa usingizi,sasa nimegundua kuwa wewe ni mtu unae toka ktk jamii ya mafisadi
 
Wewe Shy una uhakika gani kwamba huyu mbunge hana wanao muunga mkono?Ok sawa vyovyote vile lakini ujumbe umefika na sasa hivi huyo mjomba yako Ben anakosa usingizi,sasa nimegundua kuwa wewe ni mtu unaetoka ktk jamii ya mafisadi
 
Posted Date::4/23/2008
Mbunge aliambia Bunge viongozi waadilifu serikalini ni Dk Shein, Pinda
Na Muhibu Said, Dodoma

SIKU moja baada Mbunge wa Vunjo), Aloyce Kimaro (CCM), kumtuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe, Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuhusika katika ufisadi wakati wa ununuzi wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwanji(CCM), naye ameibuka na kuishambulia serikali bungeni, akisema imejaa mafisadi kasoro viongozi wawili.


Lwanji ambaye alikuwa akichangia Muswada wa Umeme wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007 uliopitishwa baada ya mjadala mkali Bungeni, mjini hapa juzi jioni, alisema haoni kiongozi mwingine muadilifu aliyebaki isipokuwa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Pia alimtaja Waziri Mkuu Mstaafu, Rashid Kawawa katika orodha ya waadilifu.


Alisema hivi sasa idadi ya mafisadi imekuwa ikiongezeka kila kukicha na kwamba njia pekee ni kwa viongozi mafisadi kukataa uteuzi na kuongeza kuwa ni aibu kuona viongozi wengi wanajitumbukiza katika vitendo vya ufisadi,

ambao alisema ni mwelekeo mbaya.


�Kila kukicha idadi ya viongozi mafisadi inaongezeka, viongozi waadilifu wanapungua kila siku. Mimi nadhani kama ukiteuliwa na Rais na kuona una madudu ni heri umweleze Rais kwamba nafasi hiyo huiwezi,� alisema Lwanji na kuongeza:


�Wanapoandikwa kwenye magazeti wanalalamika�hivi unataka uandikwe kwa mazuri tu?� alihoji.


Akiuzungumzia muswada huo, Lwanji alisema wawekezaji katika sekta ya umeme watakaokuja nchini, wengi wao ni wabovu na kwamba wanakuja kuvuna.


�Wengi wao ni reject (waliokataliwa)na kwa bahati mbaya wakija hapa wanakutana na viongozi wa ten percent (asilimia kumi),� alisema.


Lwanji aliitumia nafasi hiyo kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Kojani, Haroub Othman aliyoitoa Jumatatu wiki hii kuwa kuna umuhimu wa kuunda timu maalum ya Bunge ya kushughulikia mafisadi.


Wakati huo huo, Muswada wa Sheria ya Umeme ya Mwaka 2007, juzi jioni ulipitishwa na wabunge baada ya mjadala mkali.


Kilichomwokoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja hadi Muswada huo ukapita, ni Kanuni za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kuupinga vikali.


Wabunge waliombana Ngeleja kutoa maelezo ya ziada ni Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP). Wengine, ni Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango (CCM), Mbunge wa Ludewa, Prof Raphael Mwalyosi (CCM) na Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga (CCM).


Na ndiyo maana kuna "kufaulu" na "kushindwa"
 
Hayo ni mawazo ya Mheshmiwa Mbunge na havimfanyi Muungwana kuwa fisadi.

Mimi naamini Muungwana ni safi!
 
huyu muungwana ni as msafi as they come.Tukumbuke tu kuwa JK alibambikiwa huyu na kina Mkapa ndio kabakishwa kupiga mikasi tu.Huyu akienda mikoani hufikia kwenye state lodges,hata Arusha yeye hufikia Ikulu ndogo wakati JK huwa Ngurdoto au kule mbugani kwa matajiri
 
Hayo ni mawazo ya Mheshmiwa Mbunge na havimfanyi Muungwana kuwa fisadi.

Mimi naamini Muungwana ni safi!

Muungwana ni msafi???? Msafi hawezi kukaa na waliochafuka muda wote na yeye asipakae matope.

Huenda sio mwizi kama akina Mkapa, lakini pia sio msafi.
 
Mimi naamini Muungwana ni safi!

Mkuu FD,

Heshima mbele, muungwana bado ni safi, lakini pia huwezi kufumbia macho the political fact hapa kwamba Lowassa, Msabaha, Karamagi, Mkapa, Yona, Chenge, marafiki zake wa karibu tena sana, ni proven mafisadi tena big time, unajua kuanzia Mwalimu mpaka Yesu hakuwa na marafiki kama hawa!
 
Mi naomba mungu hiki kizazi cha wana-CCM wa sasa afanye replacement hakuna mwenye afadhari hao mnaoona wako kimya na kuwasifia nao wanatafunia ndani ya shuka wote wezi na ndio maana hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake...Sijui ni balaa gani limeikumba Tz???
 
Hata mimi binafsi namuona JK kama mtu safi. Ila wajibu wetu ni kuendelea kusimamia harakati zake zisipungue speed maana naye anabanwa sana na mafisadi hao.

Tusimkatishe sana tamaa, kwani katika awamu zote tatu zilizo mtangulia mimba za Mafisadi zilitungwa awamu ya kwanza wakati Azimio la Arusha linatungwa.

Awamu ya pili Mafisadi yakazaliwa kila limoja likawa na mchezo wa kwake, yakaanza chekechekea na kumaliza chuo kikuu.

Awamu ya tatu Mafisadi yameanza kazi katika Wizara na Idara mbalimbali. Hapo ndipo tulipoona ujanja wa panya kuuma na kupuliza. Tunachokiona sasa ni harakati za mafisadi yale yale toka awamu ya tatu.

Awamu ya nne mafisadi yanagombana baada ya kuzidiana mali ambapo sasa siri zinafichuka ni kama vile "cannibalism" ambayo huwakumba kuku na kuanza kuuwana wenyewe kwa kudonoana. Ila tushukuru kwamba mambo haya yametokea kwani kama si hali hii ya kuumbuana kwa viongozi hawa wala tusingejua kuna hali kama hiyo ya UFISADI. Mh Rais kuzitembelea wizara kuliibua baadhi ya mambo hadi yakaweza kuanza kuibuka kama tunavyoyaona.
 
Rais awe safi alafu achague au arithi viongozi wachafu?

Mwenyekiti wa chama cha kijani aliyeshindwa kuwafuta uanachama mafisadi wa richmond na EPA leo yeye ni safi?

Hainingii akilini
 
GT,

..muache Mzee wetu Sheikh Idiris Abdul Wakil Nombe.

..Yule Mzee alikuwa poa sana ila Wazanzibari watu wagumu mno.
 
Kadiri mkuu wa kaya anavyoendelea kuwakumbatia mafisadi tunafika sehemu tunaquestion uadirifu wake maana haiwezekani mawaziri wake, makatibu wakuu wake, gavana wote mafisadi wa hali ya juu halafu yeye hasiwachukulie hatua, hata kama anafuata sheria bado watu kama EL, RA Karamavi na wengine alitakiwa kukaa nao mbali maana ni majambazi wa nchi yetu.
 
Huyo Mbunge Amezungumza Kwa Utashi Wake Na Hakuna Mtu Wowote Anayemuunga Mkono Kwa Msemo Wake Huo Yeye Ana Sema Tu

Kama Kweli Shein Angakuwa Msafi Basi Asingeruhusu Watoto Wake Wengi Kuwa Na Uraia Wa Uingereza Huyo Mbunge Anajua Kweli Hili Suala ?

Shein Sio Mzalendo

Khe!! Shy shy wee!!!. Kuna kitu kinaitwa HAKI ZA BINAADAMU. Hivyo wewe unataraji huyo Mzee awazuwie Haki zao za Kibinaadamu watoto wake ambao wameshapindukia umri wa miaka 21. Uko sayari gani wewe-Shy shy (au ndio unaona haya)?
 
Huyo Mbunge Amezungumza Kwa Utashi Wake Na Hakuna Mtu Wowote Anayemuunga Mkono Kwa Msemo Wake Huo Yeye Ana Sema Tu

Kama Kweli Shein Angakuwa Msafi Basi Asingeruhusu Watoto Wake Wengi Kuwa Na Uraia Wa Uingereza Huyo Mbunge Anajua Kweli Hili Suala ?

Shein Sio Mzalendo

Hapa Shy nakuomba utoe vigezo utetee hoja yako hii.

Useme ana watoto wangapi na wepi wana uraia wa UK.
 
Back
Top Bottom