Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Siyo kila kiongozi ana akili. Siyo kila kiongozi ana busara. Siyo kila kiongozi ni mwadilifu.
Kiongozi anaweza kuwa mwenye akili, hekima na mwadilifu. Pia mnaweza kuwa na kiongozi mwongo, hana busara, fisadi, mnafiki na mropokaji.
Kwa sasa tuna viongozi wengi wanafiki, waongo, na sifa nyingi mbaya. Kutokana na uwezo wao wa uongozi kuwa mdogo, kwa sababu wanajuu hawana uwezo, wanachokifanya, wakati wote ni kumpa Mh. Rais rushwa ya sifa, wakijua kwa kufanya hivyo watampumbaza asiyaone mapungufu yao.
Viongozi hao, wapo tayari kutoa hata sifa za kejeli kwa Rais. Unapompa mtu sifa ambayo unajua kabisa ni ya uwongo, hiyo ni kumkejeli huyo unayemsifia na unamfanya hana akili ya kutambua kuwa hiyo sifa unayompa ni ya uwongo.
Wengi wenye akili na wanaotamani nchi hii iongozwe na watu wenye akili timamu, walionyoka kwa kauli na matendo, walio wakweli wa nafsi na wenye dhamira njema kwa Taifa lao, mara nyingi wamesikika wakiilalamikia hii tabia ya hovyo, ya kumsifia Rais hata kwa mambo ambayo wala hayafanyiki kwa sababu Rais. Kuna wakati ni jitihada tu wahusika, mapenzi ya Mungu, kodi na kujitoa kwa wananchi wenyewe.
Kuthibitisha tuna viongozi wengi wa hovyo, hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amewajibu wanaohoji tabia ya hovyo ya uchawa ya baadhi ya viongozi, eti yeye hawezi kumsifia Mbowe, atamsifia Rais! Hakika huyu ni miongoni mwa viongozi wanaodhihirisha kuwa ni wa hovyo, na aliyekosa hata ile akili ya kawaida ambayo kiongozi anastahili kuwa nayo.
Hivi kuna mtu yeyote ambaye yeye Chalamila anaweza kumtaja kwa ushabidi kuwa alisema Rais asisifiwe kwa mambo ambayo ni kejeli, na kwa hayo mambo asifiwe Mbowe au mtu mwingine yeyote?
Hii nchi, kwa aina ya viongozi wa namna hii, tunaua matumaini na ndoto za wananchi wa Taifa hili. Siku zote kiongozi ambaye anaonekana hovyo kwa machache tunayoyajua, uwezekano mkubwa atakuwa hovyo hata kwa mengi tusiyoyajua.
Siku zote kazi ya kiongozi ni kuwa mbele, na anaowaongoza wanatakiwa kuwa nyuma yake, na yeye akiwaongoza kuwapeleka kwenye maono sahihi. Viongozi hawa wanafiki, wanawaongoza wananchi kuelekea kwenye unafiki, na hivyo kulijenga Taifa la watu wanafiki, waongo, wapiga porojo na mafisadi, kama walivyo wao viongozi.
Kiongozi apongezwe kwa kufanya vema, aonywe na kukosolewa anapotenda hovyo, aondolewe na afurushwe anapoonekana amedhamiria kulipotosha Taifa au jamii.