Mbunge atamka Waadilifu lakini JK Rais wetu hayumo

Posted Date::4/23/2008
Mbunge aliambia Bunge viongozi waadilifu serikalini ni Dk Shein, Pinda
Na Muhibu Said, Dodoma

SIKU moja baada Mbunge wa Vunjo), Aloyce Kimaro (CCM), kumtuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe, Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuhusika katika ufisadi wakati wa ununuzi wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwanji(CCM), naye ameibuka na kuishambulia serikali bungeni, akisema imejaa mafisadi kasoro viongozi wawili.


Lwanji ambaye alikuwa akichangia Muswada wa Umeme wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007 uliopitishwa baada ya mjadala mkali Bungeni, mjini hapa juzi jioni, alisema haoni kiongozi mwingine muadilifu aliyebaki isipokuwa Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Pia alimtaja Waziri Mkuu Mstaafu, Rashid Kawawa katika orodha ya waadilifu.


Alisema hivi sasa idadi ya mafisadi imekuwa ikiongezeka kila kukicha na kwamba njia pekee ni kwa viongozi mafisadi kukataa uteuzi na kuongeza kuwa ni aibu kuona viongozi wengi wanajitumbukiza katika vitendo vya ufisadi,

ambao alisema ni mwelekeo mbaya.


�Kila kukicha idadi ya viongozi mafisadi inaongezeka, viongozi waadilifu wanapungua kila siku. Mimi nadhani kama ukiteuliwa na Rais na kuona una madudu ni heri umweleze Rais kwamba nafasi hiyo huiwezi,� alisema Lwanji na kuongeza:


�Wanapoandikwa kwenye magazeti wanalalamika�hivi unataka uandikwe kwa mazuri tu?� alihoji.


Akiuzungumzia muswada huo, Lwanji alisema wawekezaji katika sekta ya umeme watakaokuja nchini, wengi wao ni wabovu na kwamba wanakuja kuvuna.


�Wengi wao ni reject (waliokataliwa)na kwa bahati mbaya wakija hapa wanakutana na viongozi wa ten percent (asilimia kumi),� alisema.


Lwanji aliitumia nafasi hiyo kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Kojani, Haroub Othman aliyoitoa Jumatatu wiki hii kuwa kuna umuhimu wa kuunda timu maalum ya Bunge ya kushughulikia mafisadi.


Wakati huo huo, Muswada wa Sheria ya Umeme ya Mwaka 2007, juzi jioni ulipitishwa na wabunge baada ya mjadala mkali.


Kilichomwokoa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja hadi Muswada huo ukapita, ni Kanuni za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kuupinga vikali.


Wabunge waliombana Ngeleja kutoa maelezo ya ziada ni Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP). Wengine, ni Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango (CCM), Mbunge wa Ludewa, Prof Raphael Mwalyosi (CCM) na Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga (CCM).

Huwezi kusema Pinda ni msafi wakati hana miezi mitatu ofisini.tathmini Mwisho wa mchezo, Mkapa alikuwa waziri kwa muda mrefu kama Muadilifu hadi kuaminiwa na Mwalimu na alipofika anapopataka kaonesha yeye ni nani.ni mapema mno kumsifu.
 
Back
Top Bottom