FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 733
Tutawakimbiza sana mwaka huuu. Wakipika sisi tunamwaga. Wakimwaga Ugali sisi tunamwaga Mboga!
Mimi nilidhani kuna issue kubwa kumbe ni haya ? Mbona haya yaliusha sema na wana JF mmoja siku za nyuma .Anyway Mbowe kama anapata huu ujumbe ajibu mwenyewe .Mimi nitamtafuta na kumpa ila najua kesha pata maana si mvivu wa kusomana kuandika.Lakini hawa wana Chadema si waende kwenye Public Domain na kuweka kwenye magazeti ? Spinning zingine bwana .
Mimi nilidhani kuna issue kubwa kumbe ni haya ? Mbona haya yaliusha sema na wana JF mmoja siku za nyuma .Anyway Mbowe kama anapata huu ujumbe ajibu mwenyewe .Mimi nitamtafuta na kumpa ila najua kesha pata maana si mvivu wa kusomana kuandika.Lakini hawa wana Chadema si waende kwenye Public Domain na kuweka kwenye magazeti ? Spinning zingine bwana .
ukishalog in hapa au kwenye mtandao wowote, mtu yeyote mwenye utaalamu anaweza kujua location yako na kama unatumia computer yako binafsi anaweza kujua hata id yako.
Nilijua tu chanzo kitajulikana na hoja itaweza kujadilika. Now we can move on! Si nilikwambia I wont delete this thread? Ndiyo sababu hii
BAAB KUBWA !! m-zecodemy Mbowe bana ! yaani mtafute kutumia ile ze comedy style, mkimbize kwenye gari asiposimama ita polisi !
Subject: Hatima Yetu: Tuchukue Hatua
Nakupa pole kwani nadhani kazi unayo mwaka huu,
umeanza vizuri kwa kujiandikia makala na kujitumia kwa anuani ya Wana Mabadiliko Chadema chademampya@gmail.com, ukasahau kujua kuwa umewatumia ujumbe wako hafifu wasomi, wasomi wanaojua kwamba yeyoye yule aweza kufungua email address na kujipa jina lolote atakado ikiwa tuu jina hilo halijaaza kutumika na mtumiaji mmwingine.
dada Mwamvita ukasahau pia kuwa, watu makini husoma na kuamini makala toka kwenye anuani ya kueleweka kama ujumbe kuhusu ufisadi wa BOT toka kwa Slaa na Tundu Lissu au barua toka kwa Butiku. ukasahau kuwa utapuuzwa kama zile shutuma kwa Dr Slaa eti zimeandikwa na Zitto na Mbowe, hazikuwa nguvu na hata makala hii imeshajifia kabla haijasambaa, siyo kama ilivyo kwa barua ya Butiku
ukasahau pia kuwa chadema haipo madarakani, haina dora, hivyo mwandishi makini yeyote asingeweza kuficha jina maana kama anavyosema kuwa ana nzuri na ana ushahidi kwa nini ajifiche? anamuogopa nani? Mbowe? kwani mbowe anamiliki polisi? mbona Dr Slaa hawaogopi Mafisadi?
mwisho ukasahau kuwa ujumbe wa kwenye internet huonesha vituo na anuani zilizohusika, kwa mail yako wewe ulikuwa wa kwanza kuipata na haioneshi anuani za wegine waliopata awali, yaani mwandishi mwenye nia njema ya kukichenga chadema anapeleka hoja CCM, kituko, yaani mwandishi alikutumia wewe peke yako na wewe ukaanza kusambaza, ungelikuwa makini zaidi ungetafuta zile address za kichama za chadema.net halafu ukatuma ujumb ukitokea huko.
pia hukujua kuwa wana chadema wana anuani rasmi za (name)@ chadema.net.
mimi nadhani unapaswa kumsaidia Baba yako ( Mzee Yusuph Makamba katibu mkuu wa CCM) kujibu makomora yanayotumwa usoni kwake na siyo kupiga porojo kama wazee wengine wa CCM, wewe ni kijana unayeamina falsafa ya maisha bora kwa KILA mtanzania sijui mnaelewa maana ya KILA MTANZANIA?
Achana na unafiki etii ooh zito na Mnyika wanajenga chama... kwani chama chako? wewe si kiongozi wa umoja wa vijana CCM, endelea kumsaidia baba yako kukijenga chama chenu hasa wakati huu muhimu wa uchaguzi wa ndani.
eti ooh mbowe anadaiwa, nani kakwambia madeni ni dhambi? Tanzania inadaiwa, itakuwa mtanzania?kama kweli anadaiwa basi anadaiwa kwa vile hayumo kwenye orodha ya mafisadi, angekuwemo asingedaiwa kwani angetumia fungu toka BOT kulipa wadeni wake. madeni ni kawaida kwa mfanya biashara.
Hoja kwamba alipewa hongo ya milioni 6 ma Mo wa METL ni upuuzi kwani haingii akilini mtu anayemiliki gazeti linaloingiza kiasi zaidi ya hicho kwa siku akubali kuhongwa 6millions. tunachojua sisi wapinzani ni kwamba kama ingekuwa rahisi kwa mbowe kuhongwa leo hii ngekuwa amerudi CCM kama ilivyo kwa Zitto, Slaa, Mnyika, Rwakatare, Maalim Sefu, Duni nk. miiba mikali ambayo Mzee makamba na kamati zake hawalali
Hoja ya ufuska wa Mbowe ni upuuzi wa kisiasa, kila mtu anamjua mbowe kuwa ni mtu makini, mwenye mvuto, au umegeuka Dr Lilian? kama Mbowe aliwahi kubaka basi nenda mahakamani kamshitaki, utakuja kufungwa kwa kutoa hoja usizokuwa na ushahidi kisa umetumwa na CCM
Huwezi kukiokoa chama kwa habari nyepesi nyepesi
eti ooh hatuwezi kuongozwa na raisi mwenye kilabu cha pombe, Mbona unakuwa mshamba? Club Billcanaz haiwezi kumzuia mtu kuwa raisi, hoja kuwa kuna machangudoa pale nje ipeleke kwa Kandoro au ungempa mzee Makamba kwani yeye ndiye wa kuwashughulikia. mbowe hajaandika bango pale kuwa club ya machangudoa
kama mtaangalia jamaa wanatuvutia kule kwenye picha kusema wataweka after every one hour ili hapa watu wapuuzie, jamani kumbukeni kuna kiporo hapa !
Lazima tukimalize,
ZEGE HALILALI !!