Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Jamani msi-complicate mambo, 'consultant is someone who advises people on a particular subject (Tazama Cambridge Dictionary). Sasa Mnyika kuwa consultant hakuna cha ajabu. Mimi nilikuwa consultant wa shirika la kijerumani kwa miaka kadhaa kwenye mambo ya vijana kabla sijawa hata na degree. Sifa kubwa walionipea hiyo kazi ni kwamba nilikuwa na uzoefu na taasisi za vijana, period. Ndio shida yetu wa TZ tunapenda kuangalia zaidi makaratasi dhidi ya uwezo, uzoefu; ndio hivyo inabidi watu wapenda degree za short cut.

Mtalii aka chinga neno consultant lisikutishe mwanangu, lete hoja zingine, naona ile ya family business watu haoo wamenywea; ahsante sana kwa kutuelewa, karibu mjiunge na CHADEMA tujenge demokrasia Tanzania.
 
Hizii mada zilipungua makali na utamu baada ya kuchanganywa. Kuna zilizokuwa zinaenda kisomi sana mpaka unaenjoy .. na nyingine zilikuwa za kimtaani mtaani lakini tukijifunza mengi humo humo along the way.

Anyway, nna swali langu naliuliza mara ya tatu na ya mwisho.. mara mbili limekuwa ignored.

Nauliza hivi: Utaratibu rasmi wa Chadema katika kupata wabunge wa kuteuliwa uko vipi? Je utaratibu huo ndio uliotumika 2000, 2005 na utakaotumika 2010?

Yaani je huwa zinapigwa kura.. au ni maamuzi tu ya kijikamati au watu fulani?

Sababu ya swali hili ni mshangao wangu kuwa imekuwa kuwa vipi huyu Grace na Lucy ndio kuwa wabunge, considering uhusiano wao na wazee wa chama.

Jibuni jamani, vinginevyo ntaamini taarifa nlizonazo.. na pengine ntazimwaga hapa... kuwa hawa walipewa kutokana na 'vurugu' za Ndesamburo na kuwa aliweka 'masharti' mapemaaa kuwa hawa lazima wapewe. .. na hapo ndio u-family business wenyewe unapokuja! Nawapeni nafasi mnipe maelezo ya kukinaisha.. yale ya ndabita kuwa eti viligaiwa kutokana na wapi kumepatikana kura nyingi hayajaniridhisha, nimeyaona kama ni justifications .. mpaka hapo mtakapotupatia standard procedure ikoje and whether ilifuatwa au la .. na kama haikufuatwa ni kwa nini. Nimepitia website yenu sikuiona hii procedure.
 
Mwanasiasa,
'Kumbe Mtalii ndiye Chinga? Nilihisi hivyo hivyo lakini nikadhani ana pacha lake humu.
 
Jasusi: hapana sijui kama ni yeye; niliandika vile kwa kuwa hoja zawa zinafanana.
 
Ndugu Kulikoni: Pole sana kwa kuonekana tuli-ignore swali lako ambalo ni la msingi mno. Hii nafikiri ni kwa sababu kama ulivyosema mada zilichanganywa kwa hiyo kuna hoja zingine zikamezwa.

Napenda nikuongezee tu katika majibu mazuri ya Ndabita kuwa uteuzi wa wabunge wa maalumu kupitia CHADEMA unafanywa na vikao. Vikao vyenyewe ni Baraza Kuu pamoja na Kamati Kuu (soma ibara ya 6 ya katiba ya CHADEMA-ipo kwenye mtandao pia). Kila chama hupeleka majina ya wanawake 75 in priority order (1-75). Baada ya uchaguzi, kila chama kinapigiwa hesabu ya kura kilizopato na uwiano wake katika viti vya ubunge kisha kila kinagaiwa wabunge wake. Kwa mujibu wa kura za ubunge ambazo CHADEMA tulipata tulistahili viti sita. Walichofanya tume ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria na kanunu za uchanguzi ni kuchukua jina la 1 hadi la 6 katika orodha iliyopelekwa na CHADEMA.

Bahati nzuri na mbaya kwa wengine majina ya Grace na Lucy yalikuwa miongoni wa sita ya mwanzo. Kwa hivyo tume wakawatangaza kwamba ni miongoni mwa wabunge wa viti maalumu kupitia kwa CHADEMA kama ambavyo walifanya kwa Aisha Kigoda na Anna Abdala wa CCM. Kwamba Grace na Lucy wana uhusiano na Ndesamburo was just a pure coincidence kwao kama ilivyo katika mambo mengi ya kijamii.

I mean, kwamba leo George Bush ni Rais wa Marekani kama ilivyokuwa babake haimanishi kwamba basi Taifa hili kubwa duniani limekuwa la akina Bush; it was a coincidence.
 
Ahsante mwanasiasa,

Nimepitia hiyo ibara lakini naona haijazungumzia wabunge wa kuteuliwa, bali imetoa ngazi mbali mbali za vikao vya chama na nyajibu zake. Nimeona tu kuna vikao vinavyothibitisha wagombea ubunge wa majimbo.. wa kuteuliwa hawajatajwa. Pengine si kitu ambacho lazima kiwemo katika katiba.

Nashkuru umejitahidi kujibu lakini sijaridhika, nauliza zaidi. Hawa 75 mliopendekeza walipatikanaje na ni misingi gani iliyotumika kupanga hiyo priority order from 1 to 75?

Labda nitoe mfano nliouona kwa CCM na CUF. Ninavyofahamu wao huwa wanapiga kura na wanaopata kura nyingi ndio huingia. (isipokuwa kuna vikao vya juu vinavyoweza kutengua au kabadili order.. kwa sababu nzuri au mbaya). Kura za namna hii ndio zilizowaingiza akina Chifupa kupitia vijana, akina Migiro n.k.

Nimalizie tu kuwa pengine maelezo yako nisingeyahoji sana lau si hizi taarifa nlizonazo .. na baadae kuona kuwa ni wengi wenye similar concerns of the family biz issue.

By the way Grace na Lucy walikuwa 1 and 2 katika hiyo priority list au?

Kinachonifanya nione kuwa si coincodence ni hizi habari kuwa katika zile Milioni 750 zilizotangazwa na chadema kuwa ndio gharama zao za uchaguzi, takriban milioni 200 zilitolewa na Ndesamburo .. on condition that .. among other things.. Grace na Lucy wapatiwe hizi nafasi. Any comment on that?
 
KWA WAHUSIKA

Nimekuwa nikifuatilia huu mjadala, kama ilivyo kwa mada nyingine, kwa makini. Sikuwa nafahamu mengi kuhusu CHADEMA na haya madai ya "family business" yamenifikirisha. Huenda ni "coincidence", huenda ni kweli.

Mjadala huu ukanikumbusha minong'ono kuwa waheshimiwa Kabwe na Mhonga ni wachumba. Swali langu ni kwamba, KAMA NI KWELI, je kuna uhusiano wowote kati ya uteuzi wa Mhe Mhonga kuwa mbunge na uhusiano wake na Mhe Kabwe, ambaye naamini ni "kigogo" zaidi (kati yao wawili) ndani ya CHADEMA kuliko Mhe Mhonga japo wote ni wajumbe wa Kamati Kuu? Mhe Mhonga ndiye M. Said bila shaka kwenye orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu.
 
Kulikoni: Hilo la milioni 750 kwa kweli silijui kama Ndesamburo alitoa 200m on that condition. Bahati mbaya mimi ni mwanachama wa kawaida tu wa CHADEMA. Mengine kama hayo siyajui. I hope Mnyika ataibuka kukujibu hili na mengine.

Kuhusu upigaji kura, I am not sure about this as well. I will find out and come back to you. Ahsante sana kwa kutaka kujua yanayoendelea CHADEMA.
 
Mwanagenzi: Huo uchumba wa akina Zito na Mhonga sina taarifa nao. Labda ni kweli au sio kweli. Lakini ikiwa kweli nafikiri haitakuwa na uhusiano na ubunge wa Mhonga.

Ninachojua huyu binti hajaolewa na Zitto naye hajaoa na wala sio ndugu, kwa hivyo wana haki ya kuchumbiana kama wameamua hivyo. Nasi CHADEMA hatutawazuia eti kwa kuwa wote ni wabunge au ni viongozi katika CHADEMA. Ikitokea wameoana tutafunga safari tu kwenda kula pilau na kushereheka kama marafiki na kama wanaCHADEMA, itakuwa furaha kubwa!

Ni kweli pia kwamba huyo M. Said ndiye yule katika ile orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Yeye ameingia kwa wadhifa wake wa ubunge. Kwa mujibu wa Katiba yetu ukishakuwa mbunge, automatically unakuwa mjumbe wa Kamati kuu.
 
Mwanasiasa na Jasusi.

hakuna tabu kunibatiza jina la Mwamba Chinga aliyewatoa kamasi Chadema na baada ya yeye kuondoka ndio mkaja na majibu nusunusu.
mtu atakaye hoji chadema anakuwa chinga? na anayeikubali chadema anakuwa Mbowe au Mtei?
 
Unajua nyinyi Chadema you have a lot to answer maana kila siku zinakuja hoja mpya, juu ya family business, sasa haya ya Kabwe na wachubma wabunge wa Chadema yametokea wapi tena?

mimi sasa nimechoka jamani?
 
Es,

Tatizo Chadema wanatoa majibu nusu nusu na hata Mwanasiasa anayejitahidi kujibu hana majibu yote. Kuna kitu humu, nineaanza kuamini kuwa asilimia 75 ya maswali au madai ya Chinga ni sahihi.

Mtalii, rejea post yangu, nimesema inawezekana Mnyika alikuwa kwenye team ya ku consult kuhusu capacity building etc. Ukisha kuwa kwenye team basi kwa kurahisisha unaweza kujiita hivyo. BTW umeulizwa uelezee elimu inayohitajika kuwa consultant umekimbia. Nikasema kuwa huoni kuwa hizo PHD na ma profesa wa kumwaga huko serikalini ndio maana nchi haipigi hatua? wengi wao wana leta elimu ya vitabuni kwenye practice, wengi wao wamejaa urasimu........

FD
 
FD,

Nadhani tuwasaidie hawa CHADEMA jambo moja, wakajiandae vema na kuwa na agreement moja kabla ya kuja na majibu ya mmoja mmoja. Ila kwa mtu anayehoji hufaidika pale anapolihoji kundi flani au chama flani akapata mawazo ya mmoja mmoja. Hapo ndo unaweza kukijua kikundi/chama hicho kama kiko organized au ndo kanyaga twende.

Wenye kufanya mambo pamoja na kuwa na katiba moja huongea mamoja. Hakuna kubabaika! Akijibu mwanasiasa hivi, na Mnyika atajibu almost the same. Sijachambua kuona differences za wawili au wanne hawa (incl ndabita & Mh. Freeman) lakini naamini kama mwanasiasa au Mnyika (ambao wanakuwa hapa sana) wakishirikiana wanaweza kutupa data zinazoeleweka na kutufanya turidhike.

JJ, hope umenisoma mkuu... same for mwanasiasa
 
Mwanagenzi: Huo uchumba wa akina Zito na Mhonga sina taarifa nao. Labda ni kweli au sio kweli. Lakini ikiwa kweli nafikiri haitakuwa na uhusiano na ubunge wa Mhonga. Ninachojua huyu binti hajaolewa na Zitto naye hajaoa na wala sio ndugu, kwa hivyo wana haki ya kuchumbiana kama wameamua hivyo. Nasi CHADEMA hatutawazuia eti kwa kuwa wote ni wabunge au ni viongozi katika CHADEMA. Ikitokea wameoana tutafunga safari tu kwenda kula pilau na kushereheka kama marafiki na kama wanaCHADEMA, itakuwa furaha kubwa!

Ni kweli pia kwamba huyo M. Said ndiye yule katika ile orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Yeye ameingia kwa wadhifa wake wa ubunge. Kwa mujibu wa Katiba yetu ukishakuwa mbunge, automatically unakuwa mjumbe wa Kamati kuu.


Mwanasiasa bwana! Naona umekuwa mwanasiasa kama wanasiasa!

Sipingi uhalali wa uhusiano wao, kama upo. Na wala sikusudii kuwa chama chenu kiwazuie au kuwaingilia katika kutumia haki yao ya kibinadamu (right to found a family). Hasha.
Ndani ya swali langu kuna swali ambalo umeliepa (ndiyo maana nasema umekuwa kama wanasiasa ambao wanaweza kukupa maelezo, pengine marefu tu, lakini wasijibu swali), nalo ni kwamba, kama ni kweli, kwa nini unafikiri haitakuwa na uhusiano na ubunge wa mheshimiwa dada yetu?
Sina haja ya kuling'ang'ania suala hili na nisije nikaeleweka hivyo.

Angalizo Je, iwapo mtakuwa na wabunge 50 au 75, mathalani, wote watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu? Si itakuwa idadi kubwa sana kuifanya kamati iwe ya ufanisi? Au hamuamini kuwa siku moja (2010) mtakuwa na wabunge wengi kiasi kama hicho au zaidi?
 
Chadema fanyeni homework nzito mje na majibu ya kweli, badala ya siasa as usual, kumbukeni kama hamuwezi kukata mzizi wa fitina hapa forum, sijui huko mtaani itakuwaje?

Je inawezekana kuwa CCM, inayajua haya mapungufu yenu kwa siku nyingi au ndio kwanza yanafukuliwa hapa? Maana kama wanayajua siku zote basi kumbe ndio maana huwashinda kwa kura nyingi mno, halafu tunabaki tunajiuliza what happened? kumbe nyinyi ni waaarabu wa Pemba?

Kama kweli mnazo hizi skelleton zote tunazoziona hapa forum, I mean hata nguvu ya kuikemea CCM mnaipata wapi? Yaani sasa ninaanza kuamni kuwa viongozi wote bongo kuanzia CCM mpaka upinzani ni wasaniii watupu!

Sasa kama kwenda mbinguni kuliko baki ni mpaka tufe kwanza, Je Wananchi tutakimbilia kwa nani?
 
Mzee ES: Hapo sijakupata, labda uelewa wangu mdogo!

Mwanagenzi:Jibu ni hapana. Hakuna uhusiano. Muhonga aligombea kama wanachama wengi na akapitishwa na vikao na wala hakupitishwa na Zitto.

Kuhusu tukiwa na wabunge 50 au 75 itakuwaje? Labda ni-qualify statement yangu. Kuna kipengele cha uwakilishi wa wabunge katika katiba (nafikiri ni section 7.7.14) ambapo wabunge watano na wawakilishi watatu kutoka baraza la wawakilishi ndio wanaingia. Kwa sasa wabunge wote ni wanachama kwa sifa tofauti. Kwa mfano, Zitto yeye ni mjumbe kwa kuchaguliwa, ila Mhonga ameingia kuwakilisha bunge. Ahsante kwa angalizo maana limenipa nafasi ya kuweka sawa hili.

Ieleweke tu ndugu zangu hapa kuwa mimi sipo hapa kujitetea katika mapungufu yaliopo katika CHADEMA. Najaribu kuweka mambo sawa kwa kadri ninavyojua. Ninaomba sana watu wasichukue mawazo yangu kama ndio msimamo wa CHADEMA. Haya ni mawazo yangu kwa kadri niijuavyo CHADEMA. Mimi wala sina cheo katika CHADEMA kwa hivyo siwezi kutoa msimamo wa chama hiki hata kidogo. Kama kuna sehemu nimepitiliza nikaonekana kutetea bila hoja za msingi hiyo itakuwa inatokana na mapenzi na imani yangu kwa hiki chama na wala sio makusudi, na ninatanguliza kuomba msamaha kwa hilo.

Kama kuna sehemu majibu yangu yameonekana nusu nusu ni pale nitapokuwa sina facts, hapo inabidi nipapite nikitarajia mwenzangu Mnyika atateremka siku moja kuweka vitu sawa maana yeye yuko jikoni na ni kiongozi. Hoja kwamba mimi na Mnyika tukae pamoja tujadiliane haina nguvu kwa sababu hii forum tunatoa maoni binafsi na wala sio taasisi. Wala Mnyika mwenyewe hanijui mimi ni nani, ila nafikiri anajua kwamba mwanasiasa ni moja ya wanachama wa CHADEMA waliopo humu katika forum.

Naomba pia nieleweka kuwa mimi sijasema kwamba katika CHADEMA kuna purity. Ninachopinga ni hoja ambazo hazina mshiko na ambazo zimekaa ki-propaganda zaidi kuliko ukweli. Nazo ni hizi za u-family business, n.k. Nimejaribu kufafanua hili tena kwa vielelezo na takwimu hadi mzee wa utafiti (tafiti then jadili) akiingia mitini. Nimekuonesha kabisa kuwa facts hazifanani hata kidogo na ukubwa wa tuhuma zinazoelekezwa kwa CHADEMA kuhusu ukanda, ukabila na ufamilia. Sasa zaidi ya hizo facts mimi nifanye nini tena.

Hakuna kitu kigumu kukitoa akilini mwa mtu kama 'prejudices' (sina neno zuri la kiswahili). Vyama vya upinzani vilianza kwa kupandikiziwa prejudices akilini na mioni mwa watu. Prejudices zilianza na kuonesha kuwa hivi ni vyama vya fujo (vyama vyote vya upinzani), kisha ikaja na udini (CUF), then ukabila (NCCR) na sasa ukabila, ukanda na ufamilia (CHADEMA). Mimi nasema hizi zote ni conspiracy theories. Najua kwa mazingira ya indocrination iliyofanyika Tanzania, kuingia upinzani inaitaji moyo kama ilivyo kuokoka. Sisi tuliokoka (kukubali upinzani) tunajukumu la kuhubiri ukweli tu bila kupotosha. Tutakapojikwaa na kutenda dhambi, tutatubu na kurekebisha ili twende mbele katika kueneza hii injili ya upinzani. Basi ndugu zangu tusiwakatishe tamaa wale waliokwisha kujitoa kwa kuibuka na conspiracy theories.

Naomba watu sasa tugeukia kwenye sera za vyama katika mambo mbalimbali then tujadili hizi sera kama zinaweza kututoa katika matatizo yaliyosababishwa na utawala wa CCM.
 
Fikiraduni.

usomi wa form six kuwa consultant. labda kwa Udsm ujinga huo Professor Warioba wa Mzumbe haukubali wanaotaka ma consultant wa kweli waje Mzumbe university.
 
Nungwi,
Hivi consultant maana yake nini? Kama leo mimi nikiwa kijijini na nina utaalamu wa kienyeji wa miti shamba, halafu akija Daktari kutoka Ulaya, mathalan au India, anatafuta miti inayotumika katika dawa, na kwa kuwa mimi ni mtaalamu wa mitishamba, hawezi kuniajiri mimi kama consultant kwa sababu sina elimu zaidi ya form six?
 
Habari wanabodi.

Nilikuwa jela kwa hukumu niliyopewa na Admin kuchangia mada ya Mengi sikujua kama untouchable.

nimepitia mazungumzo ya Zitto Kabwe mbunge wa Chadema www.butiama.podomatic.com na amekiri kuwa mwakani atakuwa na kazi maalum ya kupambana na rushwa (nadhani ya ngono ndani ya chama) na kukifanya chama chake kuwa taasisi huo ni ushahidi tosha kabisa kuwa Chadema si chama.

Mwanasiasa wewe umesema ni mwanachama wa kawaida hivyo huna sauti ndani ya chama, wenye sauti Zitto kabwe wanakiri hamna kitu hapo.tukusikilize wewe au Zitto?

wengine pitieni kwenye blog ya Michuzi nimeona picha ya Bi Mhonga kwa kweli analipa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom