Mbowe unakosea sana kumpangia Rais Samia ratiba zake

Lete ya kwako ambayo ni sahihi
Hao “mabeberu” huwa hawatulazimishi kuwagawia bure rasilimali zetu. Ni viongozi wa serikali ya CCM hupenda kuandaa na kusaini mikataba ya kifisadi na “mabeberu”, period. “Beberu” akidai mkataba safi usio na ufisadi ananyimwa fursa na kutangaziwa kila aina ya mipasho.
Wapinzani wakidai mikataba ijadiliwe bungeni wanashambuliwa kwamba hizo ni “siri za nchi”. Kufichua ufisadi ni usaliti kwa taifa; eti unalivua nguo taifa! Ndio sababu hadi leo CHADEMA inatambulika na serikali na manazi wake kama “public enemy number one”. Mwendazake alitaka kuiangamiza na viongozi wake literally.
Huu ujinga wa kudai “mabeberu” wanataka kutuibia ni aibu kubwa sana ya awamu ya 5. Hata corona: eti nayo ni njama za mabeberu kutaka kutuibia rasilimali zetu; wtf! Hakuna mkoloni anayemshikia bunduki mtu siku hizi. Mnajipeleka wenyewe na propoza zenu za kiwizi halafu mnadai mmebakwa! Mbona nchi makini zinasaini mikataba ya maana sana?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yani mbowe naye amekosa hekima kiasi hiki kama lisu tu? Unataka umpangie rais wakati wa kukutana naye ili iweje?
Chadema limeshakuwa genge la wahuni tu wasiokuwa na hekima wala busara.
 
Kwahyo umesusa au...yaan mbowe huna tofaut na toto la mwisho.kaz kulia tu maama maama...sasa unamsusia mkuu wa nchi .una akil wew..

Yaan tangu mumuonheleee marehem vbaya sina hurimaa na nyie hata kama mko sahih..ntawaponda tuu .kama mbwai na iwe mbwai
 
Yeye mwenyewe akina Halima Mdee walishapeleka barua yao ya rufaa kwake miezi sasa 6 imepita ameikalia! Hana akili, akome kumtisha rais wetu. Na tunamshauri rais wetu aitupilie mbali kabisa hiyo barua ya Mbowe na kuichoma moto. Tuone atakachofanya huyo mhuni na faru john zake. This is isurbodination of the highest order to our president. Yaani hawa wahuni wanaamini upinzani ni mapambano ya mabavu.
 
Kwahyo umesusa au...yaan mbowe huna tofaut na toto la mwisho.kaz kulia tu maama maama...sasa unamsusia mkuu wa nchi .una akil wew..

Yaan tangu mumuonheleee marehem vbaya sina hurimaa na nyie hata kama mko sahih..ntawaponda tuu .kama mbwai na iwe mbwai
Sasa si umfate huyo marehemu huko aliko
 
Hii bahati haiwezi kujirudia tena....Nendeni "Ikulu" za Canada au Ubelgiji!
2414618_24gvpqh.jpg
 
Muda wa kwenda kugawa rasilimali zetu Kenya anao, kwanini wa kukutana na jemedari Mbowe kujenga umoja wa kitaifa, which is far better, hana!!?
Umoja wa kitaifa mnatakaga nini ,kwa mfano mpewe uwaziri au ,maana nchi iko pamoja tu wala haijawahi Kuwa hivyo mna yotaka
 
Kuwa mpuuzi nacho ni kipaji, hivi mtu unapuuziaje demokrasia?
Upuuzi ni kipaji.
 
Mnapohoji matumizi mabaya ya fedha za umma, unaofanywa na viongozi wa Serikali, mfanye hivyo hivyo kwa matumizi ya Ruzuku, kodi yetu.

Hivi kwa nini mnamwogopa Mbowe? Km alilewa chakari akadondoka, hadi leo kimya, kama vile hilo tukio halikuwepo, na hata yeye, mhusika, halizungumzii kabisa.
Hili tukio Kama sio watu kumshupalia mbowe nina uhakika ,mbowe na wapemba zake wangesingizia serikali
 
Leo mbowe akiwa mkoani Morogoro amesema walimuandikia barua kuomba kukutana na Rais Samia ila hadi leo hajakutana nao.

Anasema anaona tu anakutana na makundi mengine ila wao hataki kukutana nao, hivyo hawatasubiri mwaka kukutana na Raisi na ipo siku atawatafuta.

Hadi haoaa itoshe kusema chadema ni chama ambacho hakipo makini, ni vipi unaweza kumpangia Raisi ratiba zake?

Kama sasa hivi kabanwa atakutanaje na nyie? Mbowe ameenda mbali na kumtisha Rais eti ipo siku atatutafuta. Asipokutafuta utamfanya nini?

Walio karibu na mwenyekiti wampumzishe kidogo maana ni Kama Kuna kitu hakipo sawa kwenye medula.

#mamasamia kanyaga twende# kazi iendelee#

View attachment 1813320View attachment 1813322
Wacha hiyo mioyo yao iendelee kuvuja damu hadi ikauke tuone.
 
Nakubakiana na wewe kuwa kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi siyo hisani, ni kwa mujibu wa sheria. Lakini Rais kukutana na viongozi wa vyama hivyo si sehemu ya sheria hiyo. Hizo ni busara za kiongozi husika.

Hivyo si busara kumlazimisha na kumwamrisha rais akutane na viongozi hao kwa namna wanavyotaka wao. Kama walishamwomba kukutana naye kwanini wasiwe na subira? Atawaita kwa wakati utakaokuwa muafaka kulingana na ratiba zake.

Mpaka sasa bado anapanga safu ya wasaidizi wake katika ngazi mbalimbali. Na ndio kwanza ana miezi 2 tangu awe rais, tumeshaanza kuleta nongwa. Tujifunze kuwa na subira ndugu zangu. Subira yavuta heri.

Kwani vyama vingi ni hisani yake kama ni hisani yake walishaambiwa wavifute
 
Haraka ya nini? Mtu hata miezi mitatu hajafikisha akiwa Rais…

Au yeye Mbowe alitaka Rais akutane naye siku hiyo hiyo aliyoomba kukutana naye?

Utadhani kuna sheria inayoelekeza kwamba hilo lifanyike ndani ya siku kadhaa tangu ombi la kufanya hivyo kupokelewa!
 
Kwa hiyo anamtisha mama ili aogopwe, sisi tutasimama na mama yetu Samia hakuna wa kumtisha.
 
Back
Top Bottom