Rais Samia amekubali ombi la kukutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,797
12,239
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. John Mnyika ametoa taarifa kuwa Rais Samia amekubali ombi la Mh Mbowe kukutana naye katika tarehe itakayopangwa baadaye.

Naomba kuwapa taarifa rasmi kuwa tarehe 20 Aprili 2021 tulipokea majibu ya barua ya Mh. Mwenyekiti @freemanmbowetz ya kuomba kukutana na Mh. Rais @SuluhuSamia . Rais amekubali kukutana kushauriana na @ChademaTz . Tunasubiri kujulishwa tarehe ya kukutana.
Screenshot_20210425-154926.png

Sawa tunaimani Mbowe ataenda na nondo zilizoshiba kwa maslahi mapana ya Demokrasia
Haa wapi... tetesi ni kwamba wameambiwa kupeleka hoja zao kupitia kwa Shibuda na msajili wa Vyama ,kwanza wazikague kama zinatosha... hahahahaaaa kaazi iendelee.
 
Haa wapi... tetesi ni kwamba wameambiwa kupeleka hoja zao kupitia kwa Shibuda na msajili wa Vyama ,kwanza wazikague kama zinatosha... hahahahaaaa kaazi iendelee.
Wapeleke kopi tu, orijino wabakinazo mwishoni si lazima watakutana hapo ndio tutajua kama Mama ana nia ya dhati au la.

Uzuri kurukakaruka huwa si dawa ya urimbo
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. John Mnyika ametoa taarifa kuwa Rais Samia amekubali ombi la Mh Mbowe kukutana naye katika tarehe itakayopangwa baadaye.

Huu ni ushindi kwa Watanzania wote dhidi ya ukandamizaji tuliouona kwenye Awamu ya 5 ya Mwendazake.

Mwendazake alikuwa anatamani hata kubadili Katiba kwenye Ibara ya vyama vya Siasa ili visiwepo kabisa. Mwendazake alikuwa anawashambulia kwa risasi kama alivyomfanyia Tundu Lissu au kama alivyobomoa Bilicanas hotel and casino.

Ushauri:
Vyama vya upinzani viitumie fursa hii kwa hekima na busara na siyo kuonyesha kiburi kwa kuwa tu Rais SSH anatoka kwenye Chama kilicho kandamiza upinzani. Tusiiharibu fursa hii kwa ajili ya kuleta mazingira ya Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom