Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Status
Not open for further replies.
hapa ndiyo sehemu watanzania walipokosea..
ilibidi wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vyingi vyama vyote vingeondolewa na kuanzishwa upya ili
kuleta usawa!!
haya makauli mabovu ya nimezaliwa nikaikuta CCM yasingekuwepo.
Udhaifu ulianzia hapo mgawanyo haukuwepo thats why CCM inajiona ni chama halali kuliko vyama vingine!!
BTW tunawahesabia tuu......
kwa chama kipi sasa kitakachoweza kuichukua hii nchi zaidi ya ccm?
Nalog off
 
Kuna njia nyingi za kutoka na nzuri zaidi hebu wajiulize kina hao zitto walioko juu kwasasa walitoka kwakuwasingia wengine mambo ya uzushi?
Ndio matatizo ya kukosa ubunifu mwenzao kajijenga kisiasa kupitia misimamo yake hata kama anamapungufu yake na weakness zake. Lakini his strongest side is what made him what he is today.

Msimamo wa Zitto juu ya matumizi ya hela za umma na ubadhirifu na usimamizi wake leo unaweza kumfanya apewe hata muda wa kusikilizwa na viongozi wa sector yake nchi kubwa. Tusione picha tu kupewa appointment na yule mama mwenyekiti wa PAC UK na yeye Zitto sio kiongozi wa serikali. Hivyo kumpa ushauri ujue ameuelewa msimamo wake na anamueshimu sana kimtazamo wanawatu wakuwaambia huyo mtu ni wa aina gani and if she is worth her time. Ndio kusema hata uwanja wa kimataifa ana heshimika kwa kile anachoamini.

Nimetoa mfano wa chipsi hapo awali, sasa hivyo vibanda almost ninety percent vipo karibu na madimbwi na njia za vumbi mvua ikinyesha ujue wateja wanajitafutia madhara ya kipundi pindu na malaria kutokana na hali ya mazingira na isiponyesha minyoo maana vumbi nje nje. Ujawahi kusikia hata siku moja kiongozi wa chama kivuli kwenye afya wa chama chochote akikemea serikali kuzembea ku inforce laws of safe food services, maana wagonjwa wanategemea kutibiwa bure. Hizi ni hazard zinazo epukika na vyombo husika vipo.

Ukijaa kwenye sanaa watoto wana aribika na mamiss, sijui fiesta zisizoisha na kudandia utamaduni wa kigeni, ujaona waziri kivuli akitaka kuona enough of exploitation kwa watoto wetu matokeo yake vilaza walioacha shule wanaenda affect mpaka fikra za wanafunzi wa chuo na kuongeza upumbavu wa vijana wa kesho, yeye sanasana anataka kushindana na fiesta kuongeza tatizo.

Kila nyanja aikosolewi, wakati tunaona vile zitto anavyopigana na serikali sasa inajaribu kujirekebisha japo kwa asilimia ndogo. Na hilo ndio linamfanya hata na wazungu wamuheshimu kwa huwezo wake wakumilika kutokana na nafasi hivyo kumualiaka alika maana Zitto mwenyewe si wa vile katika maswala anayo simamia hoja zake upwaya wakati mwengine lakini huwezi kuuliza kuhusu nia yake that is enough to earn him world respect.

Hao wengine badala na wao kupambana na sehemu zingine ambazo ni mawaziri au wanaona zipo hovyo kutwa ni Zitto, kwakuwa wanaona nyota yake inasogea. Maisha si bahati nasibu ni jitihada jamaa kafika alipo kwa sababu ya kile anachoamini sasa uoga wa vilaza kama mbowe na Dr. Slaa ndio tatizo na hawa watoto wenye njaaa waliowazunguka kwa kutafuta fursa. Wakati kuna mambo mengi sana wangeweza pigana nayo na wao wakapata sifa zao kwenye jamii maana matatizo ni mengi sana. CDM ni majanga na njaa na wivu za wanachama wao ziko wazi tu maana kupata nafasi kunatokana na kupendwa na bosi wako na si huwezo ndio maana mwenye huwezo kama Zitto ni tatizo kwa wenye SACCOS kwa sasa.
 
326091_orig.jpg

some people can see what I can't see. watafikia maamuzi muhimu na mazuri, I hope!
 
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, Josephine Mushumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa? Mungekaa Kimya?

Binafsi nina matatizo na mwenendo wa Zitto, lakini katika hali ya kawaida uongozi wa chadema mmechemsha, badala ya kujibu hoja mnaleta risiti zinazomhusu Zitto sasa hizo risiti tuzifanyeje?

Ninachotaka kuona ni maamuzi yasiyo na double standard. Yaani hiki chama kimekuwa cha ajabu sana yani kwa mfano wapo vijana kama Yericko Nyerere anatoa matamko utafikiri chadema ni chama cha shangazi yake (naongea kama wanachama wanavyosema huku mitaani) na haoni madhara ya anayoyaandika humu.

Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!

Kampe Babaako masaa 24.
Jifunze kuwa na adabu ..eboh..
 
Dr. Slaa na Mh Mbowe kama kazi imewashinda, achene kuliko kitudhalilisha wa Tanganyika. Lema na Zitto wote lazima waitwe na wapowe kadi ya njano ASAP
 
Vijana wa CCM huu ni mwaka wenu wa kutaabika, mtakufa kwa kukosa usingizi kisa CDM wakati CDM ni mwendo mdundo mbona mtakoma kulinga, vibaraka wote chali. Halo halo mbona raha.
 
Mleta mada hujawa objective. Ningekuona una maana sana kama ungejaribu kuleta bandiko ukifocus kwenye reality. Unaposema Lema amemkosea naibu katibu mkuu bila kusema naibu katibu mkuu amewakosea wanachama wengine akiwamo Lema unaondoa kabisa maana nzuri uliyokusudia kwenye andishi lako hili.

Binafsi tangu mwanzo sijawahi na sitawahi kuja kuunga mkono malumbano ya kipuuzi ya namna hii. Kinachoumia ni chama. Chama hiki kuna watu wamekifia, kuna watu wamekaa rumande/gerezani kwa chama hiki. Kuna watu wametoa fedha zao halali kwa ajili ya chama hiki. Kujivua nguo hadharani kwa style ile ni kudemoralize nguvu kubwa ya sisi tilio baki. Ni ku water down nguvu ya damu iliyomwagika kwa kukipigania chama.

Mshindi katika vita hii atakuwa mi CCM. Chama ambacho wengine hatutaki hata kukisikia japo kwa sekunde hata moja.

Kwa ufupi Zitto na Lema wana 'dhambi' zinazofanana.

Nimefarijika baada ya kuambiwa Uongozi wa juu umeingilia kati. Nadhani hata Yericko Nyerere atakuwa ametaarifiwa aache mpango wake alionao.


Bila kujali nani kakosea wapi, viongozi wa chama kinachotegemea kuchukua dola kuanza kutoleana shutuma hadharani ni tatizo kubwa. naamini kuna namna ya kufanya ili haya mambo yaishe. Blame game inapoanza kwa kawaida inaashiria uvumilivu umekwisha na hii ni hatari sana kwa ustawi wa CHADEMA.
 
Vijana wengi wanaoshinda hapa JF wakimshambulia bado ni wachanga sana katika ulimwengu wa Siasa.Nina uhakika hata ukiwauliza sasa hivi haya mnayoyafanya yanmharibia Zitto?Kwa vyovyote vile kwasababu ya ufahamu wao mdogo wa masuala ya kisiasa na tabia za binadamu kwa ujumla jibu lao litakuwa NDIYO.

Tujikumbushe Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka August/2007 hadi June/2008 ambapo Hillary Rodham Clinton na Barack Hussein Obama walikuwa wanawania ticket ya Ugombea Urais kupitia Democrat Party.Obama alianza vizuri sana kwa kunyakuwa States za Nevada na Michigan,State ya 3: ilikuwa New Hampshire na Obama alikuwa anamuongoza Clinton kwa 2-1 opinion polls,Wakati wa Campaign hapo NH alitoa kauli flani ambayo Political pundits & women waliitafsiri kama sexist remarks against Clinton,Siku ya Uchaguzi Obama aliikosa ile State kwasababu Women walimpa Clinton sympathy votes ilibidi Obama ajipange upya kuhofia hasira za women zingemharibia zaidi.Zitto ni mfano wa Bi Clinton hizi siasa zenu zinamjenga zaidi kuliko kumharibi
 
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, Josephine Mushumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa? Mungekaa Kimya?

Binafsi nina matatizo na mwenendo wa Zitto, lakini katika hali ya kawaida uongozi wa chadema mmechemsha, badala ya kujibu hoja mnaleta risiti zinazomhusu Zitto sasa hizo risiti tuzifanyeje?

Ninachotaka kuona ni maamuzi yasiyo na double standard. Yaani hiki chama kimekuwa cha ajabu sana yani kwa mfano wapo vijana kama Yericko Nyerere anatoa matamko utafikiri chadema ni chama cha shangazi yake (naongea kama wanachama wanavyosema huku mitaani) na haoni madhara ya anayoyaandika humu.

Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!

Mtahangaika sana kukichafua cdm ,hamtaweza kwani jf sio sanduku la kura,kama mnatumwa na ccm,hamjafanikiwa
 
Mtahangaika sana kukichafua cdm ,hamtaweza kwani jf sio sanduku la kura,kama mnatumwa na ccm,hamjafanikiwa

chadema sio mbowe, slaa au mtu yeyote ni fikra za wapenda mabadiliko. hata Hawa viongozi hawatakuwepo chadema bado kitaendelea mbele
 
Mkuu mbona unataka nipaliwe hii Kinana baridi ninayoshushia nyama choma yangu? Hapa lazima tamko la Mkuu wa Itikadi na uenezi litatolewa tuu. zumbemkuu, ulishaona wapi mdumange unapigwa Mlalo lakini wanaokatika wako Mazinde? Ndiyo tuliyoyaona humu. Wanachadema wanabishana kwa hoja zao juu ya misimamo yao lakini ukihesabu thread za ushauri na malalamiko kuwa jambo hilo sio jema au kutoa utetezi, 80% ni wale Buku 7 & co
hahaha mkuu taratibu, nashangaa mtu anaishi huko Ngua halafu anacheza dumange la shauri linalopigwa mbaramo, loh! ngoja nkapate boha langu mie.
 
We endelea kukesha na Chadema badala ya kupigania maslahi ya Waislamu....Unaitetea ccm ambayo inakuua......

Katiba ndo hiyooo tunaipata, Mahakama ya Kadhi hakuna, OIC tupa kuleee, sijui upuuzi gani wa uamsho tupa kuleeee......

Umebaki tu hapa na Chadema kila siku....

Unazidi kuudhirishia umma wa Watanzania kwanini hauwezi kuwapa chadema kuongoza nchi.

Ni kundi la wahuni kama wewe, hauna tofauti na Mbowe na Slaa.
 
We endelea kukesha na Chadema badala ya kupigania maslahi ya Waislamu....Unaitetea ccm ambayo inakuua......

Katiba ndo hiyooo tunaipata, Mahakama ya Kadhi hakuna, OIC tupa kuleee, sijui upuuzi gani wa uamsho tupa kuleeee......

Umebaki tu hapa na Chadema kila siku....

........Mkuu tedo ungetumia kiboko ila hii missile ni nzito sana!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom