Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

halafu baadaye huyo Masha akajitoa katika kugombea huo urais usio na athari yoyote ya maana nchini
naona hujielewi. unasema huo urais wa TLS haukuwa na athari yoyote kwa nchi, una hoja gani kudhani masha aliisaidia chadema? mambo yasiyo na athari yoyote kwa nchi yanakuwaje sifa kwa huyo masha?
 
acha kudesa maswali, ndio maana unaambiwa hauna faida kwa chadema, mtu mwenyewe unaitwa mwalla
hahahahahaaaa ahahaaa!!!😀😀😀 vipi katayako mmepata diwani mpyaaaa😵

 
Msaada wa Lowassa uko wazi kwa Chadema.Kila mwenye akiki timamu anauona.Ukiambiwa hebu onesha jinsi gani Masha kaisaidia Chadema utaonesha nini????. Achana na issue ya TLS, hicho si kitengo cha Chadema kama mapimbi wawiliwatatu wanavyofikiri.
Labda msaada wa pesa ...lakini amekuta chama imara na tayari kutwaa dola .....kwanini hakwenda ACT wala NCCR?
 
In short Mbowe anakubaliana na Dr Slaa kuwa hawakuwa Asset bali Liability ....hii ya Masha cha mtoto ....soon linakuja bomu lingine ....
Ni vyema ukafunguwa ofisi ya unajimu ukapiga pesa, bado hatujampata mbadala wa Sheikh Yahya.

Je unaweza pia kututabilia unakufa lini?
 
Wewe uko na msaada gani kwani kwenye ilo chama lenu mfu? alafu kwanini mlitaka kumpa ubunge pale EA mtu asiyekuwa na mchango... kichaa cha siasa naona kitawapanda mda si mrefu.
Kwani Juliana Shonza amefanya lipi la maana ccm hadi kuzawadiwa ubunge na unaibu waziri?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema aliyekuwa mwanachama wao ndugu Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya chama chao tokea alipojiunga akitokea CCM.

Chanzo: Gazeti la Nipashe!

My take:
"Sizitaki mbichi hizi", Sungura akagumia
===============

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

Aidha, Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.

Ni kweli Masha alikuwa kama anasubiria kitu..... alikuwa siku zote akionekana kama wanachelewesha
 
Siku zote imani yangu kwa habari iliyokuja kwa njia ya magazeti huwa ndogo sana.

Labda mtoa mada unaweza kuwa na voice note ama video ya hayo maneno ya Mbowe ili nipate cha kujadili!?
 
Kamanda vipi enzi za Segerea na Makongoro? ....hivi kipindi tunawaka humu baada ya uchaguzi 2010 tungeambiwa ni kamanda mtarajiwa si tungezimia?
Mimi sijawahi kuwa Chadema na si mtumwa wa vyama, adui yangu ni ccm tu.

Mtu anayejitakasa kutoka huko sina tatizo naye, labda kama hujui siasa ni nini omba ufundishwe.

Leo Mbowe akitangaza kujiunga na ccm Magufuli atatangaza siku ya mapumziko kitaifa kwa sababu hizi ndio political milage.
 
Back
Top Bottom