Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Hata Lowassa atakaporejea CCM watasema hivi hivi eti hakuwa na msaada wowote!!
Ni kawaida, mtu akihama anaonekana mbaya. Ni kama mchezaji wakati anasajiliwa atapewa majina mengi ya kumsifia ila akiachana na timu husika unasikia hakuwa na msaada kwa timu
 
Alimsaidia Lissu kushinda TLS, Masha alichaguliwa na CHADEMA kugombea ubunge EALA huo ni msaada tosha!!...Mbowe alitaka kwenda mahakamani kisa Masha kukataliwa kugombea ina maana alitaka kufungua kesi kwa mtu mzigo au mlitaka peleka mtu mzigo EALA!!?...
kura za TLS alpiga masha ee?

mbowe na sio chadema?

myb angekua mbunge angeitendea mema chadema
then hakuwa mbunge.....
"useless till make you're self useful
 
Alitaka chama kimbebe wakati yeye ndiye akibebe chama, tangu aingie CHADEMA lile jimbo lake hata udiwani tu shidaa achana na huo uwenyekiti wa serikali za mitaa - CDM huwa haibebi watu, No room for passengers.
 
Ni haya anayetoka hana kosa
Anayeachwa ndo mwenye kosa
Busara ya kuachwa ni kukaa kimya kuliko aliyekuacha umtafutie neno la kumsema
Huyo aliyekuacha asingepata chanc ya kukujibu zaid ya alichokisema wakati anakuacha linalofatia aliyetoka atakujibu kwa maneno yako kua hakuwa msaada
Tutegemee ligi ya mipasho
 
Kwa nini mlipambana sana Lissu ashinde? mpaka serikali kuingilia kutaka kuvuruga...sasa kama hauna akili za kujua influence ya chadema kwa wanasheria, nakusaidiaje sasa

si ndio nyie Mbowe anasema hamna faida?
kwani tulikuwa tunapambana lissu ashinde nafasi ya mwenyekiti wa chadema au ubunge ? tumia akili kidogo wewe. nafasi ya TLS ni professional siyo ya kisiasa.
Msaada wa Lowassa uko wazi kwa Chadema.Kila mwenye akiki timamu anauona.Ukiambiwa hebu onesha jinsi gani Masha kaisaidia Chadema utaonesha nini????. Achana na issue ya TLS, hicho si kitengo cha Chadema kama mapimbi wawiliwatatu wanavyofikiri.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

Aidha, Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.
 
aisee... ok, hakuwa na msaada. but mbona wewe mbowe ulilia sana ulipowateua na wakakataliwa Wenje na Masha kwenye bunge la Afrika mashariki? unataka kutuambia ulipendekeza watu wasio na msaada wowote?
Masha amkimbia Nyalandu, hahahahaha
 
Kauli hizi zitasababisha wanachama kuhama chamani,kwani ni dhambi kukaa na mtu asiye msaada kwako alafu ukashindwa kumfanya awe msaada kwako.

Pale anapotoka inakuwa nongwa, bahati mbaya akifariki akiwa kwako ooh ooh marehemu alikuwa msaada mkubwa sana.!!!!!!
 
Yaani mpaka atoke mtu ndo mumlipue?

Yale yale ya akina Kigwangallah kutaka TAKUKURU wamkamate Nyalandu kwa kugawa vitalu hovyo wakati wanajua viligawiwa Ikulu - sawa tu na sasa tender za bombadier as well as ujenzi wa uwanja wa Chato zilivyosimamiwa na mkuu mwenyewe. Utashangaa miaka 8 ijayo mtu kama Prof. Mbarawa anatakiwa kuchunguzwa na kuhojiwa na vyombo. Unafiki huu ndo asili ya Watanzania

Sasa mkuu hukutaka ajibiwe alichoongea ili kiwe cha kweli au?, Yeye aliandika jimkaratasi jireeeefu kuelezea kuwa chadema hakina lengo ya kushika dola sasa yeye si angesaidia kufanikisha kishike dola? hakuwa na msaada kama hakuweza kufanikisha hilo,
 
Ni kweli masha mda wote yupo Bar analewa pia kutuma msg kwa Mange Kimambi ndiyo ilikuwa kazi yake kubwa zaidi.
Sio wote wanashinda Bar ni walevi....wa pombe!!! Masha hanywi....pombe!! Anashinda Chai muda mwingi zaidi!! Acha unywanywaaa
 
Msaada wa Lowassa uko wazi kwa Chadema.Kila mwenye akiki timamu anauona.Ukiambiwa hebu onesha jinsi gani Masha kaisaidia Chadema utaonesha nini????. Achana na issue ya TLS, hicho si kitengo cha Chadema kama mapimbi wawiliwatatu wanavyofikiri.
Wewe uko na msaada gani kwani kwenye ilo chama lenu mfu? alafu kwanini mlitaka kumpa ubunge pale EA mtu asiyekuwa na mchango... kichaa cha siasa naona kitawapanda mda si mrefu.
 
uchaguzi wa TLS?? masha did well

insipiration to new members..

mbowe akae kimya, kuna siku atahama.na yy wenzake watasema alikuwa mzigo
TLS hivii ni ya CHADEMA etieee???? kwi kiw kwi....
 
Oh yeah...TLS hii ya hawa 'team Mange kasema' ni tawi la CHADEMA.

Hukuwaona walivyofurahi Lissu alipochaguliwa?

Yaani ungedhani ni ujio mpya wa Yesu jinsi walivyofurahia....wakati mwisho wa siku hakuna lolote la maana hiyo TLS inachoweza kufanya kuhusu jambo lolote lile la maana hapa nchini.
TLS ni ya chadema etiee
 
Back
Top Bottom