Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,292
"Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA. Yawezekana, wewe na washauri wako hamjaelewa maumivu tuliyopitia kwa miaka 5 ya mtangulizi wako!! Na ndiyo sababu tulikuomba sana utusikilize mapema!! Kauli hii leo inatulaza na machozi!! Very very sad!!"-Freeman Mbowe

Mbowe.JPG

 
Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Masheikh wa UAMSHO wanakula biriani mtaani kwa sababu ya huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Mbowe amefutiwa kesi yake na kurudishiwa milioni zake 300 kwa sababu ya huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Kwani MDUDE NA WENZAKE wangeendelea kukaa RUMANDE kingebadilika KIPI huku mitaani ?!!!!!!


#ChademaWameanzaKubeep
 
Kule Misri kuna RAIS aiitwaye EL SISI....huyo asingechezewa na hawa akina MBOWE.....

EL SISI amewaweza nduguze MUSLIM BROTHERHOOD....Leo akina MBOWE NA TUNDU LISSU wanamshambulia mh.Rais Samia Suluhu kiasi hiki ?!!!! Khaaaaa 🤣🤣🤣🤣

REST IN PEACE OUR BELOVED JOHN POMBE MAGUFULI ,AMEN!!!

#KaziInaendelea
#StaunchSupporterOfSSH
 
Hawa maccm Warioba na Butiku wanaoujua umuhimu mkubwa wa Katiba mpya mbona wanaifagilia katiba mpya? Wacha ujinga wa kutaka kuendeleza UCHAFUZI wa kura.

Na Mbowe na Chadema kudai uchaguzi huru na wa haki hawambabaishi yoyote yule bali ni haki yao ya kikatiba kupinga uminywaji wa haki na uhuru wa Watanzania kuchagua Viongozi tuwatakao badala ya hawa wanaopitishwa kwa mtutu wa bunduki na ile tume FAKE ya UPORAJI wa kura.

Kwa hiyo MBOWE akisema HAPANA ndio anawasemea WATANZANIA WOTE?...
 
"Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA. Yawezekana, wewe na washauri wako hamjaelewa maumivu tuliyopitia kwa miaka 5 ya mtangulizi wako!! Na ndiyo sababu tulikuomba sana utusikilize mapema!! Kauli hii leo inatulaza na machozi!! Very very sad!!"-Freeman Mbowe
Alisha waambia mkosoeni, ila iwe kiistarabu, ninyi hamjamkosoa, ni lazima atengeneze mazingira ya kuwapima kama mlimuelewa, si kwamba amewa ban, she knows what she is doing, she listens to what you say and respond in public
 
Acha kuandika ujinga wewe! Eti ametoka kwa huruma ya mama wakati hukumu inasema kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumtia hatiani. Kwanini unaandika uongo kiasi hili kama vile wengine hatukusikia hukumu husika?

Na nani aliyekudanganya huruma ya mama ndiyo iliwatoa masheikh wa uamsho!? Uwe unasikiliza kwa makini badala ya kuja hapa na kupindisha ukweli husika.


Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan...
 
Acha kuandika ujinga wewe! Eti ametoka kwa huruma ya mama wakati hukumu inasema kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumtia hatiani. Kwanini unaandika uongo kiasi hili kama vile wengine hatukusikia hukumu husika? Na nani aliyekudanganya huruma ya mama ndiyo iliwatoa masheikh wa uamsho!? Uwe unasikiliza kwa makini badala ya kuja hapa na kupindisha ukweli husika.
Sawa.....

Mbona huko kukosekana kwa USHAHIDI WA KUWATIA HATIANI hakukuwepo kabla ya kuapishwa kwa mh.SSH?!!!!

Wale masheikh wa UAMSHO wako ndani toka enzi ya Rais Kikwete....kwa hiyo huo ushahidi haukupatikana kipindi chake....kipindi cha JPM mpaka kipindi hiki NDIO MAHAKAMA inakosa huo ushahidi ?!!! 🤣🤣

Mkuu unakataa kabisa kuwa hakuna POLITICAL WILL nyuma ya kukosekana huo ushahidi?!!!

Duuuh
 
Kwa hiyo kwa akili yako fupi Samia ndiye aliyegundua kwamba hakukuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa? Samia tangu lini amekuwa lawyer? Na huo upelelezi kaufanya lini hadi lini ili kuhitimisha kwamba watuhumiwa hawana hatia!?

Political will kwenye kesi za kubambikia watu? Ulitaka aendelee kutumia mahakama kuminya haki za Watanzania ambao hawana hatia yoyote? Kumbuka HAKI siku zote huinua Taifa na dhuluma na udhalimu huangamiza Taifa.

Sawa.....

Mbona huko kukosekana kwa USHAHIDI WA KUWATIA HATIANI hakukuwepo kabla ya kuapishwa kwa mh.SSH?!...
 
Kwa hiyo kwa akili yako fupi Samia ndiye aliyegundua kwamba hakukuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa? Samia tangu lini amekuwa lawyer? Na huo upelelezi kaufanya lini hadi lini ili kuhitimisha kwamba watuhumiwa hawana hatia...
Wewe mwenye akili ndefu hujanifafanulia KINAGAUBAGA ya kwamba ni kwanini MARAIS WAWILI WAMEPITA bila ya mabadiliko YOYOTE kwa hao UAMSHO mpaka kipindi hiki?

Unataka kusema kuwa SERIKALI hii ilipata presha kubwa ya kushughulikia KESI YA UAMSHO?!!! khaaaaa

Utanipinga tu kuwa hakuna POLITICAL WILL bali ni mahakama tu....ila ukweli uko BAYANA.
 
Back
Top Bottom