Von zelewisky
Senior Member
- Apr 26, 2013
- 183
- 50
Wakati kikao cha bunge kikielekea ukingoni asubuhi ya leo,kiongozi wa kambi ya upinzani aliomba apewe muongozo na m/kiti kuhusu wabunge waliokua kwenye orodha ya wachangiaji waleo kutokuchangia,na wabunge hao ni wa ccm.,na hivyo muda ukabaki zaidi ya saa zima bila matumizi. Akauliza uwezekano wa nafasi hizo kupewa wapinzani kuzitumia pale zinapotokea. Ghafla,kwa kimbelembele, mh.waziri lukuvi akanyanyuka na kumjibu mheshiwa mbowe kuwa ,wabunge hao hawajachangia leo kutokana na kuamua wenyewe katika vipaumbele walivojiwekea. Hawajaona kama ni muhimu kuchangia mjadala waleo. Lakini baadaye mh.m/kiti jenista,akitoa muongozo wake,alitoa maelezo yaliyokinzana na lukuvi. Sasa hapa kuna maswali nimejiuliza. 1.je hao wabunge wa ccm ambao walikua kwenye list na hawajachangia ni kina nani? (Isijekua walikua na hoja tofauti na chama hivyo kunampango ulioratibiwa ili wasizungumze) 2. Jazba,na kimbelembele cha mh.lukuvi kukurupuka kujibu swala lisilomuhusu tena kwa majibu yasiyosahihi ilizababishwa na nini?(what is the motiv behind?).