Mbungu Pius Chaya ahoji mkakati wa serikali kupambana na Tembo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Dk. Pius Chaya ameihoji serikali je, ni mkakati kuhakikisha inapambana na tembo ambao wamekuwa kikwanzo kwa wakulima wa korosho jimboni hapo?

Amesema katika jimbo hilo kuna kilimo cha korosho block farm lakini tembo hao wamekuwa wakiwasumbua sana wakulima hali hiyo hupelekea kulima kilimo kisichokuwa na tija.

Akijibu swali hilo Novemba 8, 2023 bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Luka Kitandula amesema kilimo hiko kimeanzishwa kwenye eneo la ushoroba hivyo wanapambana na changamoto ya wanyama ambao wamekuwa wakitumia maeneo hayo kutoka kwenye hifadhi na kwenda kuvamia maeneo ya wananchi.
 
Back
Top Bottom