Ni katika kuchangia hotuba ya mali asili na utalii!amesema vyombo vya usalama na viongozi waandamizi wa chama na serikali ni wahusika wakuu!amesema kilo moja ya meno ya tembo inauzwa kati ya dola 3500 mpaka 4500 hali inayohatarisha usalama wa tembo hapa nchini!
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Aikaeli Mbowe,akichangia hotuba ya ya Wizara ya Mali asili na Utalii amesema kwamba ili kuweza kumaliza Swala la Uharamia wa Tembo wanaoelekea kuisha ndani ya miaka saba kwa ajili ya Kuuwa ni vema Wabunge watunge sheria juu Wale wote wanaojihusisha na biashara hii ya Meno ya Tembo.
Alisema pia kwamba Wanaojihusisha na Biashara ya meno ya Tembo nchini ni Mtandao Mkubwa na inawahusisha Viongozi wa Serikali na Viongozi wa chama chenye Serikali pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya Usalama.
Alisisitiza sana kua kama serikali inaogopa kuwashugulikia Wahujumu hao wa Tembo ni bora ianzishwe Sheria ya Kunyonga hata kama wanaharakati wa haki za binadamu watasema Serikali ya Tanzania inarudisha Sheria ya Kunyonga badala ya kuondoa ni bora waseme kuliko kuendelea kunyamaza huku Temno wakiwa wanaisha.
Nawakilisha.