Mbowe hakupaswa kuwapa taarifa kuwa kuna bomu jingine analipua kuhusu gesi! manake magamba watajaribu kuziba kama walivyojaribu kuziba Escrow japo pale bomba lililopasuka lilikuwa kubwa na walishindwa! ninashangaa majizi yanawajibishwa kwa awamu ila chenji hayaambiwi kurudisha na watanzania wanasikitisha manake wamekata tamaa na sasa mali zao zinaibiwa kama shamba la bibi hawana kauli tena, manake siwasikii tena kudai mafisadi warudishe zile pesa za umma walizokwapua Escrow! bado nakumbuka ufisadi zilizopita na nasikitika zimefukiwa japo natamani kina LISSU wafufue tena yale madudu! nimesoma mahali wakimtaja mwandishi wa article Alta Vista 1 akidai kuwa sasa ni zamu ya watoto wa viongozi kutawala bongo eti 15% ya uongozi wa bongo kwa sasa ni watoto wa viongozi na asilimia inaweza kufika mia wabongo wakiendelea kulala usingizi wa pono!! ule uchifu aliofuta nyerere umerudi bongo kistaili! jamani natamani sana uraia wa nchi ingine!sitamani kabisa kurudi bongo japo visa inaniishia!