Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma

Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma

Swali la muhimu ni nani yupo nyuma ya kutaka kusababisha vurugu?

Hivi Magufuli aliposema tuache siasa tulimuelewaje?

Kwa nini kauli ya Rais iliyokuwa inatengeneza harmony kwa wanasiasa ilipotoshwa kwa makusudi?

Hivi ni kweli kuna mtu anataka tuendelee na siasa za kiuanaharakati au kama vile tuko kwenye kampeni badala ya kujenga nchi?

Ukawa imeshikilia majiji muhimu
..hii ikiwa ni step muhimu kuelekea Ikulu kwa nini wasijikite kwenye maendeleo makubwa katika hayo majiji ili tuone utofauti wao na CCM?

Magufuli aliachana na siasa kwa kukubali uchaguzi wa meya ufanyike Dar na atakayepata apate kwa nini UKAWA hawaliheshimu hili?

Magufuli amesisitiza kuwa tuache siasa tufanye kazi na ifukapo 2020 watanzania watuhukumu kwa haki.

Ukawa ilikuwa inalia na ufisadi na leo hii Magufuli anapambana nao ...kwa nini ukawa wanakuwa ni obstacle?

Kuna hoja nyeti sana za kuibana serikali ya Magufuli mfano Kwenye Afya elimu ajira n.k kwa nini sisikiii uhamasishaji wa maandamano kuhusu haya maswala ya kitaifa??

Ni nani huyu anayejaribu kuwapoteza vijana na kuwaondoa kwenye mstari wa fikra na badala yake anawaimbisha nyimbo mbaya kama kasuku??
Nimeipenda hoja yako bure kwa sababu umemnukuu Magufuli na si rais. Hicho ndicho UKAWA hatutaki maamuzi ya nchi yetu sote yotoke kwa mtu mmoja asiyeheshimu taasisi ya urais.
 
Mwenye chama Lowasa aliongea Jana kuwa mambo ya maandamano na migomo waache ni tabia ya uanaharakati.

Kwa hiyo Mbowe Leo ametekeleza amri ya Mwenye chama
Hakiyanani kuna watu wana akili ndogo, daaaah
 
Nilikuwa nasubiria kwa hamu kuona vijana wa ufipa wakipokea kichapo kutoka jeshi la polisi..sijui wangemlaumu nani..ila ingewatia akili na uwezo wa kuchanganua jema na baya.
 
Amesema kuwa CCM iachwe ifanye mkutano wake, na wao watatumia mikondo yote ya sheria iliyo nchini na nje ya nchi kupigania haki za vyama vya siasa.

Pia amezungumzia suala la vijana waliokamatwa na polisi kuwa wana haki ya kupewa dhamana kwani sheria ipo wazi juu ya hilo, huku akisisitiza kuwa hawaogopi kulala ndani.

AZAM TWO TV
Ukiona ngoma nzito ni vyema kuufyata mkia.
 
Swali la muhimu ni nani yupo nyuma ya kutaka kusababisha vurugu?

Hivi Magufuli aliposema tuache siasa tulimuelewaje?

Kwa nini kauli ya Rais iliyokuwa inatengeneza harmony kwa wanasiasa ilipotoshwa kwa makusudi?

Hivi ni kweli kuna mtu anataka tuendelee na siasa za kiuanaharakati au kama vile tuko kwenye kampeni badala ya kujenga nchi?

Ukawa imeshikilia majiji muhimu
..hii ikiwa ni step muhimu kuelekea Ikulu kwa nini wasijikite kwenye maendeleo makubwa katika hayo majiji ili tuone utofauti wao na CCM?

Magufuli aliachana na siasa kwa kukubali uchaguzi wa meya ufanyike Dar na atakayepata apate kwa nini UKAWA hawaliheshimu hili?

Magufuli amesisitiza kuwa tuache siasa tufanye kazi na ifukapo 2020 watanzania watuhukumu kwa haki.

Ukawa ilikuwa inalia na ufisadi na leo hii Magufuli anapambana nao ...kwa nini ukawa wanakuwa ni obstacle?

Kuna hoja nyeti sana za kuibana serikali ya Magufuli mfano Kwenye Afya elimu ajira n.k kwa nini sisikiii uhamasishaji wa maandamano kuhusu haya maswala ya kitaifa??

Ni nani huyu anayejaribu kuwapoteza vijana na kuwaondoa kwenye mstari wa fikra na badala yake anawaimbisha nyimbo mbaya kama kasuku??

Sijaelewa hapo kwenye bold,au mie ndiye sielewi maana ya "siasa"?Nijuavyo mimi hata uchaguzi ni siasa!
 
Wakati Lowasa anauziwa chadema na kugombea urais alikuwa na uzoefu na chadema kwa masaa mangapi ??

Ya chadema yamewashinda ,ya ccm mtayaweza wapi??.

Magufuli amekuwa mbunge na waziri kupitia ccm kwa miaka 20 !! Alafu wewe kibavicha kutoka ufipa unakuja kitumbo mbele kudai hana uzoefu na chama!!

Shame on you
Ukithibitisha kama lowassa alinunua chadema , najitoa jf sasa hivi , lakini ukishindwa kuthibitisha , mimi na watu wangu tutahakikisha unapigwa ban ya milele kuingia jf , uongo wa kishamba kama huu haukubaliki popote pale .
 
Wakati Lowasa anauziwa chadema na kugombea urais alikuwa na uzoefu na chadema kwa masaa mangapi ??

Ya chadema yamewashinda ,ya ccm mtayaweza wapi??.

Magufuli amekuwa mbunge na waziri kupitia ccm kwa miaka 20 !! Alafu wewe kibavicha kutoka ufipa unakuja kitumbo mbele kudai hana uzoefu na chama!!

Shame on you
Kwani aliwahi hata kuwa balozi wa 10*10?
 
Lowassa hakupenda vijana waende huko kwa sababu ni hoja iliyoyotengenezwa UBUNGO.

Jamaa hayupo vizuri kichwani ndo maana mwenye chama amekataa.
 
mbowe kaogopa!! huwez kushindana na dola
La msingi undumila kuwili wa jeshi la polisi umewekwa hadharani na uhusiano wao na chamadola umethibitishwa kimazingira. Lakini si-dhani kama tumeona mwisho wa hili vitimbwi vya polisi vitaendelea tu mpaka hapo mahakama itakapoamua vinginevyo.
 
Back
Top Bottom