Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma

Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma

La msingi undumila kuwili wa jeshi la polisi umewekwa hadharani na uhusiano wao na chamadola umethibitishwa kimazingira. Lakini si-dhani kama tumeona mwisho wa hili vitimbwi vya polisi vitaendelea tu mpaka hapo mahakama itakapoamua vinginevyo.
lengo lilikuwa ni bavicha kwenda kuzuia mkutano, je wamefanikiwa?? hayo ya polisi weka kando kwanza
 
Naona nguruwe pori wamefunguliwa wanapokezana
 
lengo lilikuwa ni bavicha kwenda kuzuia mkutano, je wamefanikiwa?? hayo ya polisi weka kando kwanza
Sidhani kama hata wao wenyewe waliamini kuwa hilo lingewezekana-mkutano wa CCM ungelindwa kwa gharama yeyote ile lakini walikuwa tayari kwenda kuonyesha polisi na CCM wanavyoendesha mambo ya nchi hii. Polisi walipo-ona wameshikwa pabaya wakatoa tamko la kuilinda CCM huku wakisema mikutano ya ndani inaruhusiwa, hivyo yale yaliyotokea Dodoma, Iringa, Moshi na Morogoro "hayatatokea tena". Lakini la kuambiwa changanya na zako-hapo anaelindwa ni CCM. Ya polisi huwezi kuyaweka kando kwani ndio mkono wa CCM kudhibiti wengine na ili kujitakasa unaona wametoa tamko ambalo bado lina mitego kwa UKAWA.
 
Amesema kuwa CCM iachwe ifanye mkutano wake, na wao watatumia mikondo yote ya sheria iliyo nchini na nje ya nchi kupigania haki za vyama vya siasa.

Pia amezungumzia suala la vijana waliokamatwa na polisi kuwa wana haki ya kupewa dhamana kwani sheria ipo wazi juu ya hilo, huku akisisitiza kuwa hawaogopi kulala ndani.

AZAM TWO TV

mwenye chama na mkuu alishatoa general statement jana na kusema biashara ya maandamano imepitwa na wakati. cut that crap chama kime graduate sasa. sio chama cha uanaharakati tena. Mbowe lazima atii maelekezo au amri. haya tulitegemea kwa Mbowe na wengine to follow likewise
 
bavicha mmemsikia mkuu wenu? msikanyage dom..at your own risk..
 
Hivi maneno kama haya angetamka Zitto hawa wanaitwa nyumbu wangemuitaje?
CDM ni ccm kichaka.
Never blv this party again..labda yule aliyenunua hiki chama akiondoka.
 
Ukiona ngoma nzito ni vyema kuufyata mkia.
Ni làzima wafyate mkia, walijaribu Bavicha kupima kina cha Mani juzi, wakajikuta wako viongozi peke yao hakuna aloyewaunga mkono, wameishia kunyea debe. Hakuna namna in lazima watafute njia ya kitokea!!
 
Hapa lazima tuseme. Mbowe ameonesha ukomavu mzuri wa kisiasa nikiwa kama mpenda mageuzi mwenye fikra huru huwa napenda kuyatizama mambo katika hasi na chanya.
Binafsi nilipingana na maamuzi ya kwenda dodoma . hayakuwa na tija kwa chama na wanachama wake.lakini kwa sasa CDM imekuwa na baadhi ya Viongozi vijana wa hovyo sana ambao hawafikirii mbali.

Lakini ni hawa hawa ambao baadaye hubadilika na kuwa wapinzani wa watu wenye kuamua mambo kwa kutizama pros and cons. Hakukuwa na uwezekano wa kuzuia mkutano mkuu wa CCM HATA KIDOGO. watu wengi wangepigwa mabomu na kuvunjwa miguu na pengine kuangukiwa na kitu chenye ncha kali. Wazaz wangelalamika chama kinaua na kuharibu watoto wao.

Nlimtizama mkuu yule wa polisi mkoa/kanda akizungumza. Alijawa na chuki,ghadhabu na aina flan ya kisasi. Angeumiza vijana wengi sana na kuwafunga.lakini mwishowe mkutano wa ccm ungefanyika kwa amani kabisa.

Chama kama chama kisingekuwa na faida yoyote ndani na nje ya nchi kwa machafuko yale.na hawa vijana wanaotoa matamko je wnapata muda wa kutafakari?lowassa anaonesha aina ya siasa ambazo zinafanyika mataifa yaliyokuwa kisiasa. Nataman na ccm wangeonesha ukomavu wao pia katika hili. Siasa chafu mara nying hupelekea machafuko kwa nchi husika.

Bado naiasa serikali yoyote inayokuwepo madarakani. Kuna kipindi polisi na majeshi hushindwa. Tumeona mifano ya misri,syria na kwingineko.

Tusifike huko. Huu ni wakati wa cdm kutengeneza akina john mnyika wengne. Heko mbowe.
 
sasa hawa BAA YA VICHAA hawana mlezi mshauri au nini kweli huko ukoo Wa kambare
 
sasa hawa BAA YA VICHAA hawana mlezi mshauri au nini kweli huko ukoo Wa kambare
Ujumbe wao umeshafika. Lengo ilikuwa kuikumbusha serikali na polisi kushughulisha ubongo kidogo kabla na si baada ya kuamua mambo.
 
Usiache na akili ikazure. Tuliza akili watu wenye uelewa watachangia wewe usiye na uelewa uliyezoea lugha za hovyo una aina ya threads zenu. Nikusahihishe. Siyo kambare- KAMBALE

sasa hawa BAA YA VICHAA hawana mlezi mshauri au nini kweli huko ukoo Wa kambare
 
Hiyo ilikuwa ni strategy ya kufikisha ujumbe na kuibua mjadala juu ya double standard za Policcm. Hilo limefanikiwa.
 
Back
Top Bottom