Mbowe awazuia BAVICHA kwenda Dodoma

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Amesema kuwa CCM iachwe ifanye mkutano wake, na wao watatumia mikondo yote ya sheria iliyo nchini na nje ya nchi kupigania haki za vyama vya siasa.

Pia amezungumzia suala la vijana waliokamatwa na polisi kuwa wana haki ya kupewa dhamana kwani sheria ipo wazi juu ya hilo, huku akisisitiza kuwa hawaogopi kulala ndani.

AZAM TWO TV
 
Hapa kuna kitu, haiwezekani jana EL leo Mbowe. Kutaka ccm ifanye mkutano wake kwa amani kutakuwa na manufaa kwa cdm kuliko kuuzuia au kuuvuruga.

Ghafla tu hawa cdm kubadilika hivi si bure, hata kama wanajulikana kwa maamuzi yao ya kubadili gia angani lakini ni vema mkajiuliza ni manufaa gani cdm watakayopata kutokana na kile ccm watakacho kifanya Dodoma? Au wananufaika vipi kwa kubadili msimamo wao?
 
Swali la muhimu ni nani yupo nyuma ya kutaka kusababisha vurugu?
Hivi Magufuli aliposema tuache siasa tulimuelewaje?
Kwa nini kauli ya Rais iliyokuwa inatengeneza harmony kwa wanasiasa ilipotoshwa kwa makusudi?

Hivi ni kweli kuna mtu anataka tuendelee na siasa za kiuanaharakati au kama vile tuko kwenye kampeni badala ya kujenga nchi?

Ukawa imeshikilia majiji muhimu
..hii ikiwa ni step muhimu kuelekea Ikulu kwa nini wasijikite kwenye maendeleo makubwa katika hayo majiji ili tuone utofauti wao na CCM?

Magufuli aliachana na siasa kwa kukubali uchaguzi wa meya ufanyike Dar na atakayepata apate kwa nini UKAWA hawaliheshimu hili?
Magufuli amesisitiza kuwa tuache siasa tufanye kazi na ifukapo 2020 watanzania watuhukumu kwa haki.

Ukawa ilikuwa inalia na ufisadi na leo hii Magufuli anapambana nao ...kwa nini ukawa wanakuwa ni obstacle?
Kuna hoja nyeti sana za kuibana serikali ya Magufuli mfano Kwenye Afya elimu ajira n.k kwa nini sisikiii uhamasishaji wa maandamano kuhusu haya maswala ya kitaifa??

Ni nani huyu anayejaribu kuwapoteza vijana na kuwaondoa kwenye mstari wa fikra na badala yake anawaimbisha nyimbo mbaya kama kasuku??
 
Waambie CCM waibane hiyo serikali ya UKAWA waachie wenyewe
Serikali ifanye kazi na wanasiasa wafanye siasa maana ndio kazi yao
Hayo majiji waliyoshinda viranja kila siku wanatoa matamko hao mameya watafanyeje kazi?
 
Wakati Lowasa anauziwa chadema na kugombea urais alikuwa na uzoefu na chadema kwa masaa mangapi ??

Ya chadema yamewashinda ,ya ccm mtayaweza wapi??.

Magufuli amekuwa mbunge na waziri kupitia ccm kwa miaka 20 !! Alafu wewe kibavicha kutoka ufipa unakuja kitumbo mbele kudai hana uzoefu na chama!!

Shame on you
Magufuli ashawahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi CCM?
 
Amesema kuwa CCM iachwe ifanye mkutano wake, na wao watatumia mikondo yote ya sheria iliyo nchini na nje ya nchi kupigania haki za vyama vya siasa.

Pia amezungumzia suala la vijana waliokamatwa na polisi kuwa wana haki ya kupewa dhamana kwani sheria ipo wazi juu ya hilo, huku akisisitiza kuwa hawaogopi kulala ndani.

AZAM TWO TV
Nakubaliana na Mbowe, Polisi sio watu wa huruma, watawaua vijana. Kuna njia zingine za kudai haki hiyo, hazijashindikana. Try those first!
 
Back
Top Bottom