Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Utaratibu wenu wa kutangaza mapato niliupenda sana, lakini ghafla mkaacha. Nini kiliwakuta ghafla mkasitisha? Wanamchi tuna hamu na hako ka utaratibu..! Rudisheni basi, au mtupe sababu ni nini?
Ukiongopa sana mwisho wa siku ni aibu.
 
Zilikuwepo, sasa kwanini media zisitangaze mpaka waitiwe press conference? Kwanini wasidakue data na kuandika magazetini?
Kwanini msilaumu media, mlaumu serikali?
Jibu swali kwanini sasa hivi TRA hawaitishi press kutangazia wananchi mapato ya mwezi ?. Usizunguke zunguke kama mtu ambaye haelewi swali kwenye mtihani.
 
Kuna tofauti gani? Data si zipo mkasome? Mimi naona kama mnalalamika na kuja na sababu zisizo na msingi wowote ule. Nendeni mkazisome halafu tujulishane badala ya kuja na sababu zisizo na mbele wala nyuma.
Ziko wapi hizo data?Hakuna Data zozote
 
Kuna tofauti gani? Data si zipo mkasome? Mimi naona kama mnalalamika na kuja na sababu zisizo na msingi wowote ule. Nendeni mkazisome halafu tujulishane badala ya kuja na sababu zisizo na mbele wala nyuma[/QUOTE Sasa Mimi Niko kijijini ntazisomea wapi? Mbona unakuja na majibu rahisi utafikiri hukuwahi kugusa umande
 
Ziko wapi hizo data?Hakuna Data zozote
Sharia ndio mdudu gani?
Data zipo, sema uelewa wako ni mdogo subiri magazeti labda yatakuelewesha. Sharia/sharia who gives a fk?
Keyboard yangu ina auto-correct kwa hiyo ukiandika neon sheria ina-detect na kubadilisha kuwa sharia kwa sababu ni neno maarufu. Wengi huelewa hili, sema naona teknolojia imekupitia kando. No wonder huzioni hizo data.
 
Zilikuwepo, sasa kwanini media zisitangaze mpaka waitiwe press conference? Kwanini wasidakue data na kuandika magazetini?
Kwanini msilaumu media, mlaumu serikali?
Watawalazimisha wenye mamlaka?
 
Benki kuu na TRA wanatangaza mapato kwenye website yao. Nendeni mkasome acheni uvivu.

Ukiingia kwenye website ya TRA huoni mahali penye makusanyo ya mwezi ya nchi nzima kaka. Hapo ni kwamba mwanzoni ilikuwa ni kick toka malimbikizo. Sasa hivi biashara zimedondoka na mapato yameshuka ile mbaya.
 
Back
Top Bottom