Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Kwamba bajeti iliyopo haifuatwi.

Niambie, mishahara hailipwi? Au haikua kwenye bajeti?
Niambie, kuna mwanafunzi kacheleweshewa boom? Au pia haikua kwenye budget.

Ujenzi wa reli haukua kwenye bajeti?

Halmashauri gani haijapata gawio lake?

Elimu bure imekwama?

Au umewasikia wakina Lema Nawewe ukaamua kupita na maneno yao.?
 
Hivi yale makontena yaliyokuwa yakikamatwa kwamba yamekwepa kodi wahusika wake walufikishwaga mahakamani?
 
Sijuwi kwa sasa ccm inaunua madiwani na wabunge wa upinzani kwa bei gani. TRA isome na bajeti ya kununua madiwani. Yaani badala ya kuelekeza fedha kwenye miradi ya maendeleo wao wanaelekeza kwenye manunuzi ya binadamu na play maker wa hii game ni polepole
 
Mara raisi kayakamata 3000, mara waziri mkuu kayakamata 2900, yaani nchi hii
 
Mwenzako aliulizia mshahara juzi na akasema serikali imefilisika.
Hizi threads tumeshazizoea hapa jamvini
Ccm iache kuwanyanyasa watanzania. Bila ccm hili taifa lingekuwa mbali sana kimaendeleo lakini kwa chuki na roho mbaya ya ccm wananchi wamezidi kuwa masikini sana
 
Mods naomba msiunganishe uzi huu na mwingine.
Kuna mambo mengi mazuri yanayoanzishwa lakini ghafla yanazimika. Tumeshuhudia kampeni za usafi mwisho wa mwezi, usafiri bure kwa waalimu Dar, kupanda miti Dar na mazoezi yanayoongozwa na makamu wa rais Samia Suluhu.
Je, TRA kusoma mapato ilikuwa mojawapo ya 'kiki' hizi za kuanza na kuzima?
Swala la TRA kutusomea mapato na matumizi lilikuwa linatupa mwanga, japo hali ilikuwa ngumu kitaa lakini ukisikia fedha zimeelekezwa kwenye ujenzi wa airport Chato na hostel za Magufuli nyingine kwenye fly over atleast moyo unafarijika kuwa hatujapigwa.
Lakini ghafla.... hakuna taarifa ya mapato na matumizi, wasiwasi unawapata raia maana bajeti iliyopitishwa bungeni haifuatwi sasa hela zinakwenda wapi. Au ndo hizo biashara zisizoeleweka kati ya TZ na North Korea?
Je, TRA kufungua branch Rwanda kuna kilichoongezeka au tunabeba mzigo wa kuwasaidia warwanda.
Wito:tusomeeni mapato na matumizi labda italeta faraja katika kipindi hiki kigumu.
Wengi hapa walikuwa wanalalamikia hayo mapato kutolewa kila mwezi; Walikuwa wanasema ni ya uongo an wengine walisema ayawasaidii chochote!
 
Back
Top Bottom