Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Mbona mapato ya kila mwezi hatusomewi?

Too much politik!

Wangeweza kutangaza bila siasa na mbwembwe wala kusingekuwa na maswali.
 
Sasa hivi wamebaki kutangaza yale mapato ya kinyang'anyi kupitia askari wa usalama barabarani.
 
Nasikia wale watumishi vyeti vilivyogongana pia hawapati mshahara. Kuna mtumishi kaja kunikopa na ana familia, hii serikali vipi?
 
Sasa watangaze nini wkti hali sio hali naskia makusanyo kwa mwezi ni 110trilioni sawa na thamani ya kontena 277 za makinikia
 
Kobello kama una uhakika, si ulete link hapa tuone tulichokusanya
 
TRA vipi...mmekata pumzi au? Halafu nasikia siku hizi mnavizia watu kama vile wale Traffic wa Tochi
TRA siku hizi mnabambikiza kodi eti?
 
Wanasaka hela Kwa nguvu ili wagomboe bombadier ile!

Ova
 
Siku hizi wameongeza vitengo vya ukusanyaji kodi, Traffic polisi nao wamekuwa ni kitengo ndani ya TRA cha ukusanyaji kodi kupitia faini za barabarani.. W/end hii tu nadhani kwa Dar hapa watakuwa wamepata sio chini ya bilioni moja..
 
Siku hizi tunasomewa tu takwimu za polisi Dar Es salaam wamefanikiwa kuwapora/kuwanyang'anya madereva na wamiliki wa magari kiasi gani kwa wiki, kwa sas polisi Dsm wanakusanya (Kwa njia isiyo halali) mapato makubwa kuliko TRA.
 
Huku kwetu Rwanda mapato ni siri ya serikali. Cha UMUHIM wananchi wapate huduma

Kumbe Tanzania mlikuwa mnasomewa,?
 
Mods naomba msiunganishe uzi huu na mwingine.

Kuna mambo mengi mazuri yanayoanzishwa lakini ghafla yanazimika.

Tumeshuhudia kampeni za usafi mwisho wa mwezi, usafiri bure kwa waalimu Dar, kupanda miti Dar na mazoezi yanayoongozwa na makamu wa rais Samia Suluhu.

Je, TRA kusoma mapato ilikuwa mojawapo ya 'kiki' hizi za kuanza na kuzima?

Swala la TRA kutusomea mapato na matumizi lilikuwa linatupa mwanga, japo hali ilikuwa ngumu kitaa lakini ukisikia fedha zimeelekezwa kwenye ujenzi wa airport Chato na hostel za Magufuli nyingine kwenye fly over atleast moyo unafarijika kuwa hatujapigwa.

Lakini ghafla.... hakuna taarifa ya mapato na matumizi, wasiwasi unawapata raia maana bajeti iliyopitishwa bungeni haifuatwi sasa hela zinakwenda wapi.

Au ndo hizo biashara zisizoeleweka kati ya TZ na North Korea?

Je, TRA kufungua branch Rwanda kuna kilichoongezeka au tunabeba mzigo wa kuwasaidia warwanda.

Wito: Tusomeeni mapato na matumizi labda italeta faraja katika kipindi hiki kigumu.
 
Mwenzako aliulizia mshahara juzi na akasema serikali imefilisika.
Hizi threads tumeshazizoea hapa jamvini
 
Mkuu mapato ya serikali ya kila mwezi ni makubwa mnooo..
Ndio maana wameona hakuna umuhimu wa kutangaza tena.
Ona mwenyewe utekelezaji wa mambo mengi nje ya Bajeti mfano kununua Madiwani na Wabunge wa upinzani, kununua ndege kwa malipo ya Cash, kuhonga wabunge 10mil, maana yake mapato yanayokusanywa ni makubwa.
 
Back
Top Bottom