Ni Long story Ndugu yangu lakin kwa ufupi baada ya jaribio la Mapinduzi kushindwa 1983 Baadhi ya Watuhumiwa walitoroshwa Gerezani Ukonga na kupelekwa Kenya Kupitia Mpaka wa Horohoro na lilitumika Gari la Kubebea Mkaa kuwabeba kina Kapten Maganga
Mwl Baada ya kugundua Mpango huo ndipo akatengeneza Revenge
Baada ya Arap Moi kutikiswa ikabidi wafanye Mazungumzo na Mwl Nyerere na wakakubaliana wabadilishane Wale Wahaini ndipo kina Maganga wakadanganywa na Utawala wa Kenya kuwa wanawapeleka kuwaficha Ethiopia kwa kuwa kuna Vijana wa Nyerere Wapo mitaa ya Nairobi wanaweza kuwadaka Kumbe ni Mpango wa kwenda kuwakabidhi Dodoma si Dsm
Nyerere nae aka swap kwa kukabidhi Wahaini feki kwa Moi wakat huo tayari kina Odinga ( Wahaini halisi ) wameenda kufichwa Canada Kama wakimbiziwa Kisiasa kishawasafirisha, Moi baada ya kugundua alipoteza kabisa Interest na Tanzania na Mwl kabisa kwa kuingizwa Chaka
Tanzania haitokuja kupata Rais Mwenye akili Nyingi sana Kama Julius Kambarage Nyerere never never!