JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Kongamano hilo la siku tatu limeshirikisha Watoto zaidi ya 3000 kutoka Parokia zote za Jimbo Kuu la Mbeya likiwa na lengo la kuwajenga katika maadili ya dini na kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao, kujitambua na kujilinda dhidi ya vitendo viovu.
Aidha, katika kongamano hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Dawati la Jinsia na Watoto na Kikosi cha usalama barabarani kitengo cha elimu kwa umma lilipata nafasi ya kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia, utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu na elimu ya matumizi sahihi ya barabara.