MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Nani amekuambia ni rahisi kumfukuza mwanafunzi,hakuna wa kukosa ajira,Ualimu ni ajira ya kudumu labda wengi wanaacha baada ya kupata kazi nyingine.
Kwa hiyo kama sio rahisi kumfukuza ndio wampige kama wanapiga nyoka?????

Walimu wa mwendokasi kazi sana

Imagine angefia hapo ingekuwaje?????

Kwa nini ujiharibie kwa upuuzi wa mtoto wa mtu??????

Mbona miaka yetu walimu hawakuwa wanafanya hivi???

Na alokwambia ajira ya kudumu hufukuziki ni nani???
 
No comment, huyo dogo inaonekana aliwaletea ubabe hao walimu wake, ukiangalia vizuri mwanzoni anaonekana ameshika fimbo ya mwalimu, naona wadau mnakomenti upande mmoja tu.
Mkuu nikuulize tu je angekua mwanao kakuletea huo ubabe unaousema ungempiga hivo? Kwa comment yako we ni hatari sana kuwa baba wa kambo
 
Video inakasirisha..kama mimi ndio huyo mwanafunzi hakika ningemtafuta ticha kwa muda wangu na lazima angeandika historia kwenye diary yake
Umesoma vizuri ni Mwalimu wa field na ameondoka atampata wapi.
 
1475751245123.jpg

Sijui kama ni kweli
 
Hawa walimu inatakiwa wafungiwe mmoja mmoja kwenye chumba kimoja na yule Scorpion wa buguruni halafu tuone ubabe wao
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. MWIGULU Nchemba, W MNN
 
Daah huyo mwalimu aliyerekodi video hii sijui ana hali gani

Ila jamaa mwenye sarawili ya khaki anatembeza slap za adabu utadhani anampiga mgoni aliyemfumania
 
Serikali hii haina masihara yani ukitoa jambo asubuh ndani ya masaa 24 tayari hatua zishachukulia, HII YOTE HAIJAJA TU KIRAHISI NI SAAB YA RAIS MWENYEWE HAKUNA KULALA, Ndio sabab kikinuka tu wahusika washafanya yao kuchukua hatua, SAFI SANA KAMA WAMEKAMATWA NA KUHOJIWA.
 
Nakumbuka wakati nipo high level kuna mwalimu wa nidhamu alikuwa ukimzingua na yy anakuzingua, ukijifanya unapga ngumi na basi mnaandaa ulingo, btw kuna wanafunzi wengine wanaletwa shule sababu wazazi wamechoka usumbufu wake, hapa nunda kakutana na walimu manunda
 
Hawa walimu ni wauaji kabisa hawawezi mpiga mtoto kama wanaua nyoka.Ingekua amri yangu kwanza kila mmoja angepewa wanajeshi sita wawapige kama walivyomfanyia huyo mtoto halafu ndio wapandishwe kizimbani
 
Arobaini zikifika lazima udakwe yaani watu wameanza kujirekodi wenyewe wakijua wanafanya makosa alianza police wamefuata walimu next time sijui ni nani
 
Mbona nimesikia walimu waliotenda hicho kitendo wamekimbia?isipokuwa walimu wote wa Mbeya day ndio wanahojiwa na polisi,kwani walimu waliotenda ni walimu wanafunzi waliokuwa field kutoka UDSM na mtuhumiwa mkuu wa hiyo kesi ambaye anatoa kipondo cha nguvu anaitwa Mwlm,Msigwa.



Watakamatwa tu hawana kwa kwenda, kwanza hawana pesa za kutosha, wataishia kujisalimisha mahali njaa, uchovu wa mwili na msongo wa mawazo vitakapokick in!
 
hawa waalimu ndio wale wanaopitishwa kwanza JKT wanapewa matizi mpaka wanazimia na wanagalagazwa kwenye maji?baada ya hapo ndipo wanaruhusiwa kuomba chuo?

anyway hawakufanya jambo jema,viroba,ugoro,kuvaa milegezo,ujana
 
Sema negative effects za jeshi najua una maana JKT, usiishie tu kusema effects kwa sababu kuna positive effects pia za jeshi (JKT). Hata hivyo mimi binafsi naona ni ujuha wa hao walimu tu na si suala la kuhusisha jeshi hapo. Jeshi yaani JKT haijaanza leo, watu wengi tumepita huko nadhani labda hata wewe, lakini siyo wote wenye tabia kama hizo. Hawa walimu hawana ethics za ualimu kabisa, nadhani ndo hawa wanakwenda kusoma ualimu kwa sababu tu points za course zingine zimegoma.
Umefuatilia vizuri kama ni Walimu wa field kutoka UDSM basi ni wale waliopata division one ndio wanachaguliwa kwenye Ualimu.
 
Mkuu nikuulize tu je angekua mwanao kakuletea huo ubabe unaousema ungempiga hivo? Kwa comment yako we ni hatari sana kuwa baba wa kambo

Kwanza wewe ni jipu, ngoja nikutumbue kwanza.
 
Back
Top Bottom