MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Naomba email ya Prof Ndalichako au Simbachawene haraka sana. Hii ni zaidi ya Iddi Amini Dada!!!!!!!!!!!!!
 
too much..wanampiga utadhani ni mwizi....mkulu hebu litolee tamko na hili.
 
Pamoja na kazi ya kuboresha utendaji serikalini na kuondoa ufisadi; Haya mambo JPM inabidi ayafanyie kazi ili kujenga jamii bora. Watoto kupigwa , kunyanyaswa majumbani, wanawake kuteswa, kupigwa...ujinga ujinga kama wa Mvumi, Dodoma; lazima tujenge jamii bora yenye kuheshimiana...sasa hiyo video ni adhabu au ukoloni, mwanafunzi anashughulikiwa utafikiri scorpion wa buguruni
 
Hii ni miongoni mwa video mbaya kabisa kuziona, hatua kazi za kisheria lazima zichukuliwe na hiyo shule iwekwe wazi watu waanze kuisusia. Hiyo shule yote ni jipu kuanzia mwalimu mkuu mpaka mwalimu ''muuaji''

Huwezi kumpiga mtoto wa watu namna ile tena akiwa hana uwezo wowote wa kujilinda ... ni unyanyasaji wa hali ya juu kabisa.

Kuanzia leo nimepanga kutovumilia kipigo chochote cha mwalimu kwa ''Mwanangu'', nitakachomwambia kuanzia leo ni kwamba endapo ataguswa tu kwa kosa lolote aje anieleze nikalianzishe ... upuuzi kabisa huu.

Waalimu 4 kwa ka-mwanafunzi mmoja!!!!Nooooooooo
 
Daaah hata kama ni adhabu hii hapana hawa walimu wachukuliwe hatua za kisheria haikubaliki mwanafunzi kupigwa namna hii
 
Ukatili wa hali ya juu. huku si kumrekebisha mwanafunzi bali kumumiza kwa kukusudia; tazama anavyogaragazwa.. tazama anavyokanyagwa mkono.. tazama hayo makofi yenye nguvu ya kuweza kujeruhi ngoma ya sikio, taya, meno, ulimi... Kweli huku ndo kumrekebisha mwanafunzi???? Mheshimiwa Profesa Ndalichako mama yetu mpendwa tutumbulie jipu hili
Dogo ni mkaidi na akishazingua anaenda kutamba kwa wenzake,hii kitu ni lazima ili ajue kwamba akileta uhuni anazinguliwa kihuni.Saafi sana walimu,saaafiiiii kabisaaaaa
 
Ni halali

Halali kwa upande upi..!? Kuna adhabu ya namna hii kwa mwanafunzi kaka..!? Hata kama kaua..! Si mumpeleke kwenye vyombo vya sheria..!? Kuna Juvie mkuu.. au kama kawashida mumfukuze tu..! Ili asiwape hasira..! Kuadhibu mtoto wakati uko na hasira namna hii sio sahihi hata kidogo..! Kama angekua mwanao unakuta anapigwa namna iyo kama nyoka ungejiskiaje..!? Ukiangalia kwa udadisi utajua kwamba huyu aliekua anapiga kama anaua anaconda hana uhusiano mzuri na wenzie(walimu) na ndio maana hata kuna alie rekodi na kuipeleka viral..! Na ninahisi ni huyu aliekua anaomba dogo asamehewe..! Na hata apo unaona kuna wenzake wa kiume wanamwambia amuache..! Hii sidhani kama ni sahihi asee..!
 
Mimi nafkiri TCRA wakishirikiana na jeshi la polisi wanaweza kuijua simu iliyosambaza na iliyorekodo kupitia imei na laini ya simu. Hivyo basi ni vyema hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao walimu wote waliohusika hapo.
 
Walimu pia ni wazazi kwa upande mwingine ila hapo nahisi kuna tatizo la zaidi ya kitaauma na huyo mwanafunzi.
Walimu bado vijana waodogo kwenye hiyo clip nahisi hawana hata uzao katika hii dunia so wanampiga huyo kijana kama wapo mtaani tu au kwenye uwanja pale shabiki wa simba alipoingia upande wa mashabiki wa Yanga.
Sheria zichukue mkondo wake kwa hawa walimu ili iwefundishio kwa walimu wengine .Adhabu kwa wanafunzi zimeainishwa kwenye vifungu vya sheria na jinsi kutoa hizo adhabu imeelezwa sasa sio kwa mtindo huu.
Hakuna sifa ya mwalimu mzuri wa kuadhibu bali mwalimu anayefaulisha vizuri kwenye taaluma yake.
 
Back
Top Bottom