MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

wp_ss_20161006_0006.png
 
alaf uyo jamaa aliyevaa suruali ya khaki na shati la drafti atakuwa siyo ticha uyo,kama sio mukora kafoji cheti
 
Kwanza niseme kuwa walimu wameghafilika kidogo na kupitiliza hivyo wanapaswa kujaribu kupunguza hasira. Ila pia inashangaza kuona watu humu wanaonekana kuwa na uchungu sana na wengine kutoa lugha za kejeli na kibabe kwa walimu. Hivi kwa ninyi mnaosema angakuwa mwanao huyo ungeishia jela kwa kufanya kitu kibaya, unadhani wewe utakuwa sahihi kufanya kitu kibaya kwa walimu lakini wao hawakuwa sahihi kufanya kitu kibaya kwa mwanafunzi aliyewaudhi? Na kama ndivyo tofauti yako wewe na wao ni ipi?

Pili, shuleni kuna changamoto nyingi sana kwa walimu. Kuna wanafunzi anakosea, unataka kumuadhibu anagoma, unampeleka ofisi bado anagoma, anashika fimbo anaivunja, ukimshika shati vizuri ili umuadhibu anakukwida shingoni, nauliza kwenye mazingira hayo unafanyaje?

Tatu, wale wanaofikiri ni rahisi kufukuza mwanafunzi shule wanakosea sana. Ni kazi ngumu mno kumfukuza mwanafunzi shule haswa kwa shule za serikali. Wanafunzi wengine kwakutambua hilo wanaweza amua kumuabisha tu mwalimu vile watakavo. Isitoshe kufukuza shule sio njia bora ya kumrekebisha tabia mwanafunzi. Shule watu haweindi tu kujifunza mambo ya darasani bali ni pamoja na kujifunza na kufundishwa tabia nzuri. Hivyo tusikimbilie kusema kazi ya mwalimu ni kufundisha tu maana huwezi mfundisha mtu amabaye hana nidhamu. Sote tunatambua kuwa elimu na nidhamu zinaendana. Shule zikijikita kwenye kufukuza fukuza tu ni kina nani watabaki huko? Kuna watu leo wamekuwa na maisha mazuri na mchango mkubwa kwa taaifa lakini wakati wanasoma walikuwa wakorofi sana kiasi kwamba wangepaswa kufukuzwa shule. Hata hivyo busara za walimu kwa kuamini katika kuwadhibu ndizo zilizosaidia mpaka leo hii wamefika walikofika, na pengine wengine wamo humu. Je wangefukuzwa shule wangekuwa wapi leo? Kwahiyo huwezi kuwa kila kosa au kila mwanafunzi anapogomea adhabu au vinginevyo wewe unafukuza shule, hakuna utaratibu wa dizaini hiyo.

Nne, wazazi wengi wameshindwa kutimiza majukumu ya kulea wanao. Kazi yote ya malezi ametupiwa mwalimu, unategemea nini. Mwanafunzi mkorofi kiasi cha kupigwa na walimu kadhaa hata nyumbani lazima anashida. Wanafunzi wanafanya makosa, mzazi anaitwa afike shuleni lakini anatoa jibu jepesi kabisa "Huyo mtoto mimi ameshanishinda, ninyi amueni tu mtakavoamua" kwenye hali kama hiyo unadhani tabia ya mtoto itakuwaje. Tukiwa huku kwenye mitandao tunataka tuonekane wazazi tunaojali lakini ukweli ni kuwa wazazi wengi siku hizi wamekuwa kero kwa walimu na malezi kwao sio ishu tena. Kila mmoja hapa ajiulize anashiriki vipi kuhakikisha mwanae anapata maadili mazuri akiwa shuleni na nyumbani? Ni mara ngapi unasikia mzazi akilalamika kumshindwa mtoto ambaye pengine hata msingi hajamaliza na wengine wakiwa kidato cha kwanza au cha pili? Ni kweli inauma lakini tujiulize kwanza juu ya uwajibikaji wetu kabla ya kuwahukumu wengine.

Tano; kuhusu kufuta taratibu za kuadhibu hilo ni jambo gumu kuliko uhalisia wake. Hakuna namna kila kosa likifanyika walimu wajipange kwa mkuu wa shule kuelezea kosa, wasubiri kibali cha kuadhibu viboko vitatu kwa mwanafunzi tena wamuandike kwenye daftari. Utaratibu huu ni mgumu sana na kwa wanafunzi wameaka hii tutazalisha vijana watukutu na masifuri mengi mno. Hivyo tujaribu kuangalia na uhalisia.

Mwisho, ni kweli kuwa kitendo kile kimevuka sifa za adhabu(characteristics of punishment) na hakipaswi kuungwa mkono. Kama binadamu walimu ni vizuri kujaribu kuhimili hasira na kutokuadhiba pale ambapo mtu amekasirika. Ni watie moyo kwa kazi ngumu na nzuri mnayoifanya sio tu ya kutoa maarifa bali pia ya kulea vijana. Tukumbuke kuwa jamii hii hii inayolalamika na kutaka sheria za adhabu kufutwa ndiyo hiyo hiyo itakayo lalamika kuwa malezi yamewashinda na ndio maana mtaani wanafunzi wamekuwa wakorofi. Narudia siungi mkono adhabu kupitiliza lakini natambua namna ambavyo vijana wa leo wamekuwa wakiwapa changamoto kubwa sana walimu.
 
Aise hao walimu ni wakatili sana, isitoshe ni vijana mbona wana hasira namna hiyoo???
 
Mhhh! utafikiri kituo cha mateso ya wanajeshi wa Hitler,hata kama huyo mwanafunzi ni mjeuri si kwa kipondo hicho,duh walimu punguzeni hasira kwani hasira hasara.



Ndio hivyo tena sasa wameshatiwa mbaroni, kibarua kiko njia panda, hasira hasara; majuto ni mjukuu!!
 
Hawa waalimu waliofanya unyama huu ni wakufuatiliwa na vyombo husika,wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Ziko adhabu zakumpa mwanafunzi lakini sio waalimu wanne kwa mwanafunzi mdogo kama huyo.Na yuko Mwalimu wa kike anayeunga mkono aendeelee kuteswa mwanafunzi huyu,naye aunganishwe na hawa,inasikika sauti yake,wakati mwenzake wa kike akikataza asiendelee kuteswa.

Tusubiri vyombo vya dola vithibitishe
 
Wadau,

Clip hii sijui ni shule gani lakini yaonekana ni hapa nchini kutokana na sauti ya dada inayosikika kwenye background.

Hata kama huyo kijana amekosa vipi si angepelekwa vyombo vya sheria?

Wana tofauti gani na wale wanakijiji walioua watafiti?

Sheria ifuate mkondo wake, inaumiza sana.

=======
UPDATE:

Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.

Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.

Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.

Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.


​

HAO WAALIMU BADO HAWAJAAJIRIWA WANGEPATA AJIRA KAMILI INGEKUWAJE?KIUKWELI NI JAMBO LA KIKATILI HALIVUMILIKI
 
Video inakasirisha..kama mimi ndio huyo mwanafunzi hakika ningemtafuta ticha kwa muda wangu na lazima angeandika historia kwenye diary yake
 
Kama kutoandika homework ndo anapigwa hivi,akikutwa anatoroka si watammalizia na risasi kabisa!! mwalimu anatakiwa kudhibiti hasira zake kulea watoto ni kazi ngumu ukitanguliza hasira unaweza piga kila mtoto shuleni.
 
Hawa walimu inatakiwa wafungiwe mmoja mmoja kwenye chumba kimoja na yule Scorpion wa buguruni halafu tuone ubabe wao
 
Taarifa zingine ni kwamba huyu dogo si mwanafunzi bali mtu toka uraiani na alivaa sare za shule ili aingie shuleni hapo kwa misheni zake alizojua yeye mwenyewe.
 
Hamjafanya uchunguzi mnakurupuka huyo jamaa siyo mwanafunzi bali alivaa nguo za kianafunzi na yy akajichanganya ili arubuni videnti


Nafikiri mmeelewa
Imethibitishwa kua ni mwanafunzi sio jamaa wa mtaani

0404
 
Ni shule gani hiyo? Mzazi wa huyo mwanafunzi akiwatokea na panga hao walimu atakuwa amekosea? Hasa yule mpigaji?
kiukweli walimu hawakustaili kabisa kumpatia adhabu iyo,wachukuliwe sheria hao walimu wote
 
Sipati picha aliyeirekodi hii video saizi yupo hali gani
 
Ndio hivyo tena sasa wameshatiwa mbaroni, kibarua kiko njia panda, hasira hasara; majuto ni mjukuu!!

Mbona nimesikia walimu waliotenda hicho kitendo wamekimbia?isipokuwa walimu wote wa Mbeya day ndio wanahojiwa na polisi,kwani walimu waliotenda ni walimu wanafunzi waliokuwa field kutoka UDSM na mtuhumiwa mkuu wa hiyo kesi ambaye anatoa kipondo cha nguvu anaitwa Mwlm,Msigwa.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
So painful watu wangu..mwanafunzi anatia huruma hata kama angekuwa kafanya kosa huo si uchapaji mzuri.
Wanisamehe tu mimi naona wachukuliwe hatua za kinidham tu.
 
Sema negative effects za jeshi najua una maana JKT, usiishie tu kusema effects kwa sababu kuna positive effects pia za jeshi (JKT). Hata hivyo mimi binafsi naona ni ujuha wa hao walimu tu na si suala la kuhusisha jeshi hapo. Jeshi yaani JKT haijaanza leo, watu wengi tumepita huko nadhani labda hata wewe, lakini siyo wote wenye tabia kama hizo. Hawa walimu hawana ethics za ualimu kabisa, nadhani ndo hawa wanakwenda kusoma ualimu kwa sababu tu points za course zingine zimegoma.
Hawa wameingia na dvn one lkn
 
Back
Top Bottom