MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Mkuu wa kaya anakasirishwa sana na div "0" sasa nyie mnaotokwa na "POVU" eti kijana kaonewa "Tukutane mahakamani" maana inaonekana huyo kijana mnamrubuni nyie....!
 
huwa nawaheshimu walimu na huwa siwaheshimu walimu kabisa hasa baada ya kumaliza elimu
 
Mnataka nikomenti ili kuwafurahisha nyie ? Acheni mihemko kama mmetekenywa kila mtu anahaki ya kusema anaojiskia kusema, hakuna sehemu nimeunga mkono adhabu ilotolewa, sipo upande wa hao walimu au wa huyo mwanafunzi, so acheni personal attack zenu, kama hamjapenda nilovocomment piteni kimya tu kuliko kuniletea mihemko yenu hapa.
CC
[HASHTAG]#Safari[/HASHTAG] safi
[HASHTAG]#Mwelewa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Prondo[/HASHTAG]
Na wengine
 
Kama ni kweli siyo igizo, aliyepiga hiyo "video clip" na kuisambaza na asiipeleke kwenye vyombo vya sheria, ana kesi ya kujibu
 
huyo mwanafunzi alimlawiti mwenzie?!?..mbona kipigo ni cha hatari sana?
 
Kama ni kweli siyo igizo, aliyepiga hiyo "video clip" na kuisambaza na asiipeleke kwenye vyombo vya sheria, ana kesi ya kujibu
kuna tetesi eti ni kijana aliyevaa nguo za shule na kwenda kuwarubuni wanafunzi ndipo waalimu wakamshtukia! ebu tuendelee kufuatilia tujue mwisho wa sakata hili
 
serikali ipo busy kuhamia dodoma kila kitu kinakwenda ovyo.. mara scropion kamtoa mtu macho, mara tarfiki kalamba hela kwa mzungu, huku mkuu wa gereza kala hela ya madawati,kule ndege zimebuma... ni shidaa tupu
 
Wanafunzi wa siku hizi some times wanahitaji adhabu kama hizi. Maana wamejaa kiburi kiasi cha kipiga hata na kujeruhi waalimu.
 
Huyo Teacher aliyekuwa anampa kelbu aka nakozi za uso mfululizo atakuwa ana stress za kupigika kimaisha,nakozi kama zile unaweza kuja kupata madakesi (Murder case).
 
Dogo nae mzembe kweli inamaana hakua hata na bikari au kiwembe? basi hata kalamu zile za cello au speedo amzamishie mmoja wao hapo mbona wangesanda.Sema hiki kizazi cha msoga, fesibuku na smatisimu ujasiri huo akuna ndio mana amekubaliana na hio hali. Pole yake.
 
Polisi wanaumiza hivi hivi mmenyamaza. Haki za binadamu nani ana haki Tanzania? State ya kila mtu kushughulikia mwenzie
 
RSO Mbeya amethibitisha kuwa tukio ni la Mbeya Day Secondary.
MKUU wa Wilaya wanalishughulikia hivi sasa na Waziri Mkuu ametaka maelezo kwa Rc
asnte sana wakamatwe haraka hawa walimu wahuni wakubwa
 
Unaweza kumwambia arudi nyumbani akakwambia siendi na adhabu sifanyi.kuna mmoja nilimwambia akanyoe ndevu kesho yake ulikuwa mtihani wa necta,nikamwambia vinginevyo hutaingia kwenye mtihani akajidai mbishi,kesho yake yeye na mwenzake wakaja wamenyoa viduku hata balotel cha mtoto,tulipowakamata mimi na bosi wangu mmoja,tulitembeza bakora na tukakwangua zile nywele,kila ukipeleka wembe unatoka na ngozi,hawa madogo waliumia mnooo,walifanya pepa wakikiwa wamefunikwa vichwa.Mmoja akamuita baba yake,na baba yake alishachoka ujinga wake ikaishia hapo.Mmoja alikula four mwenzake zero.

Kwa hiyo kama mwalimu unajisifia kwa hili?!! Shame on you! Sishangai watoto kuchukia shule!
 
Kama ni kweli siyo igizo, aliyepiga hiyo "video clip" na kuisambaza na asiipeleke kwenye vyombo vya sheria, ana kesi ya kujibu
Sasa watakuwa hata hawasambazi, wewe badala ya kumshukuru kuirecord tu unaanza kumshambulia
 
Peleka polisi kuna jela za watoto...
Lakini huwezi kunipigia mtoto kiasi hiki...

Juzi nilisikia kuna mwalimu kapewa kipigo hadi kufa...
Story ilikuwa inaelezwa nusu nusu...lakini kuna taarifa kuwa huyo mwalimu walikuwa anawageuza watoto wa kiume kama option ya kutowaadhibu...ukikosa anakwambia chagua...fimbo au nikugeuze...
Afu wanafunzi wenyewe wa sekondari...walimtolea uvivu wamempiga ...kalazwa sijui Bugando...mwisho kafa...niliposikia story kamili nikasema afe tu

nilipotazama video hii,nikafikiria labda huyu mwanafunzi kamlawiti mwenzake...
 
yaani angekuwa mwangu huyu cjui huyu mwalimu anayemzaba vbao ningefanya je, yaani nilvyoumia anavyomchapa vbao nahc muda huu ningekuwa nyuma ya nondo haki ya mungu ningemfanya kitu mbaya watanzania wote mmngenichukia nimeumia sana kwa kweli.
 
Wanafunzi wengine wakorofi sana,ni kina scorpion wajao.....mfano hapo ameambiwa lala chini ila anagoma angekuwa humble wala wasingemshambulia,na ingekuwa ni mwl mmoja bila shaka wangepigana
Kulikuwa hakuna sababu ya kumpiga, kakataa kuchapwa arudishwe kwao aje na mzazi, mzazi akikataa abaki na mwanae, mitoto kibao ipo mitaani yenye tabia mbaya, na yeye wangemwacha akaongeze idadi huko mitaani.
 
Kwa taarifa kutoka chanzo cha uhakika ni kwamba tukio hilo ni kweli limetokea Mbeya Day Sec
Kulikuwa na ubishani kati ya Mwalimu wa field na mwanafunzi hali iliyopelekea kushikana na hatimae mwanafunzi kumjeruhi mwalimu mdomoni kwa ngumi
Hali hiyo ilipelekea walimu wengine wa field kumbeba mzobemzobe mwanafunzi huyo na kumpleka chumba cha Staff na kumsulubu
Hakukuwapo walimu wenyeji na hao walimu wenyewe walijirekodi na kurusha tukio mitandaoni kama vile kuonyesha kitendo chao cha kukomeshea
Walimu hao walimaliza field Ijumaa na kurejea makwao
Pole kwa walimu wa Mbeya Sec shule yenu imechafuliwa
 
Back
Top Bottom