MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

No comment, huyo dogo inaonekana aliwaletea ubabe hao walimu wake, ukiangalia vizuri mwanzoni anaonekana ameshika fimbo ya mwalimu, naona wadau mnakomenti upande mmoja tu.
Pamoja na hayo ndugu, lakini still it doenst justify "mtoto" kupigwa hivyo mana huyo bado mtoto, kama mwanafunzi kagoma adhabu na alifanya kosa kubwa kuna njia zingine, kama kumuita mzazi wake, aelezwe tatizo, au kusimamishwa shule, wengine wanapewaga hadi adhabu za kulima au kufanya usafi either wa vyoo au kufagia uwanja wa shule peke yako hata mwezi mzima, lakini sio KIPIGO hicho, sasa hayo mabao tena ya uso angewafia je? au hata kuzirai au kutokwa damu mdomoni na puani? hapana kwa kweli au kama kawashinda sana basi mfukuzeni shule akahangaike na wazazi wake lakini sio kumpiga hivyo, yani naandika huku machozi yananitoka aisee hapana
 
kuna mwanafunzi aliwai kimpiga mwalimu wa kike mitama ya nguvu muda mwingine wanafunzinao niwakorofi hasa wakijua viboko haviruhusiwi basi nikuangalia move za utupu kwenye smrtfn zao minathani kuliko upate kesi ni bora kumuacha tu maana ukichukua hatua za kinithamu pia tabu
 
Kama alileta ubabe si wamrudishe nyumbani,kuliko adhabu wanayompatia,hivi bahati mbaya huyu mtoto akapoteza maisha yake,picha itakuwaje?
Unaweza kumwambia arudi nyumbani akakwambia siendi na adhabu sifanyi.kuna mmoja nilimwambia akanyoe ndevu kesho yake ulikuwa mtihani wa necta,nikamwambia vinginevyo hutaingia kwenye mtihani akajidai mbishi,kesho yake yeye na mwenzake wakaja wamenyoa viduku hata balotel cha mtoto,tulipowakamata mimi na bosi wangu mmoja,tulitembeza bakora na tukakwangua zile nywele,kila ukipeleka wembe unatoka na ngozi,hawa madogo waliumia mnooo,walifanya pepa wakikiwa wamefunikwa vichwa.Mmoja akamuita baba yake,na baba yake alishachoka ujinga wake ikaishia hapo.Mmoja alikula four mwenzake zero.
 
Hii haikubaliki hata kidogo. ni matumaini yangu wahusika watachukua hatua kabla wazazi hawajachukua sheria mkononi.
 
No comment, huyo dogo inaonekana aliwaletea ubabe hao walimu wake, ukiangalia vizuri mwanzoni anaonekana ameshika fimbo ya mwalimu, naona wadau mnakomenti upande mmoja tu.
Wewe ni mwalimu nini? Bora unyamaze tusije tukamaliza hasira zetu kwako
 
Video hii inaonyesha walimu wakitoa adhabu kwa mwanafunzi kwa mtindo ambao haujaelekezwa kutumika, mwanafunzi anapaswa kupewa adhabu kwa kuchapwa mikononi au matakoni, sasa hapa walimu zaidi ya watatu wanamuadhibu mwanafunzi kwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili.

Hili si jambo linalofaa hata kidogo na likiachwa hivi kuna maafa yatatokea siku moja katika shule zetu ama kwa kuuawa wanafunzi kwa vipigo ama kwa wanafunzi kutopenda kwenda shule kwa kuhofia adhabu za mtindo huu.

Hata kama mwanafunzi kagomea adhabu si kwa nguvu hii inayotumika nafikiri akigoma nikumchukulia hatua zinazofuata sio kumfanyia shambulio la kudhulu mwili namna hii.

Wadau wa elimu litazameni hili
 
tar 5/10 kila mwaka ni siku ya walimu, haya ndio wanatakiwa wayazungumze
 
Wakuu katika pitapita zangu huko kwenye makundi ya WhatsApp nimekutana na video inayowaonyesha Waalimu wakimuadhibu kijana wa kiume katika njia ya kikatili sana.

Kiukweli aina hii ya adhabu si sawa ndugu waalimu kuna wazazi wengine mtaishia kugawana majengo ya serikali wewe mwalimu unaelekea hospitali na mzazi anaelekea kituo cha polisi.

​

Hakuna anaempenda mwanafunzi kama mwalimu. ... naamini wanajua wachokifanya... wanafunzi wengine hata police hawawawezi. ..
 
So what?! Kwahiyo, sheria na utaratibu ukishika fimbo ya mwalimu ndio unatakiwa upigwe kwa style ile?! Nyie watu hebu anzeni kwanza kuzaa ndio mjue uchungu wa kulea na kusomesha ... Hiyo style ya upigaji haina justification hata kama mwanafunzi alimtukana mwalimu matusi ya nguoni

Upo utaratibu wa adhabu ikiwemo kusimamishwa shule/kufukuzwa ama kupelekwa Mahakamani. Kumpiga mwanafunzi namna ile kunafanya watu waanze kujiuliza kuhusu mpigaji kama ana akili timamu.

Tunahitaji kujua jina na huyo mwalimu na shule yake tuende tukamjazie inzi kwa kusimama na mabango kupinga ukatili huu.


Huyo ni mmojawapo wa hao walimu. Huwezi kutetea ujinga kama huo kama na yeye siyo wenye tabia kama hizo.
 
Wengi wanakurupuka tuuu,na ndo maana mitoto ya siku hizi haina adabu,unakakuta kabinti ka shule kanaongea na simu mambo ya kingonongonooo,na kamekaa kingonongono tuuu kisa hawa walezi wanaocomment humu.Vivulana vinajifanya vitemiiii na kuwadharau walimu kisa baba yake ana ka passo na pick up.kama ni mimi nakunyoosha kama nyoka na niliwahi fanya hivo kwa dogo mmoja hivi shule moja Mbez huko.Alipoleta ujuaji nilimfukuzisha shule jumla,Sipendagi ujinga mieee
Mfukuze shule inatosha siyo kumpiga namna hiyo.
Bora ukamuacha akaenda kufundishwa na dunia kuliko mwalimu kufanya kitendo kama hicho, mpaka hapo utakuwa siyo mwalimu timamu.
 
Back
Top Bottom