Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 1,354
- 1,869
Mkuu; Umenena vyema lakini pia ujue kuna wakati hata kuwa na Elimu hakuna tija sana juu ya mahusiano esp. kwa walio ndani ya ndoa. Ingia kwenye ndoa uone ndoano zilizopo. Ni majanga.Watu hua wanadharau wasomi na Elimu, lakini kuna uhusiano mkubwa sana kati ya matukio ya ajabu ajabu na Elimu ndogo. Ni nadra sana, narudia tena ni nadra sana kwa wasomi wa Elimu angalau ya Chuo kusikia wanafanya matukio ya namna hii. Lakini pia kuna uhusiano mkubwa sana kati ya hali duni ya kimaisha na matukio ya ajabu ajabu. Sijawahi kusikia mtu mwenye ukwasi anaanguka majini, kupandisha mashetani ama anaenda kushinda kwa Mwamposa ili aombewe apate rizki bila kufanya kazi. Umaskini, ufukara, hali duni za kimaisha, kipato duni na kukosa elimu hivi vitu vinaleta msongo wa mawazo (stress) na kupelekea watu kufanya matukio ya ajabu ajabu kama haya. Katika hali ya kawaida huwezi kua unafikiria kuua ua ama kuuana uana tu kama ndo solution ya matatizo yako na mwenzako
Inatokea kero kwa mwenza wako na akishauriwa, akionywa, akikatazwa na hata "akipapaswa/akifinywa" kidogo haelewi amekaza fuvu. Inafika mahali mwanaume anasema ni afadhali ya jana -ya leo ni kali mno.
Sasa kama mwanaume hana akili ya kujiongeza au akifikiria kuja kugawana pasu kwa pasu ilhali kasota kupata mali na huyo mke , lakini mke ndo huyo tena amekengeuka analeta za kuleta .....ukijazia na kaulevi kidogo ndo yanapojitokeza majanga kama hayo. Usishangae nyuma ya tukio hilo akawepo mwanamke.(wanawake wanasalitiana sana)
Ni ukweli usiopingika kwamba huyo njemba (mume) amejipalia mkaa kwani huenda hukumu kali ikampasa na hakuna anayeunga mkono kitendo chake.