Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Hivi pale town uhindini naskia soko liliungua sijui watu wakahama? Is it true
Yea liliungua 2012 kama sikosei siku hizi ni kiwanja tu pale kimezungushwa mabati. Nilikua huko miezi kadhaa iliyopita bado hapajajengwa
 
We wa home kabisaaaa
Niliishi jirani na familia ya Mapugilo pale kiwanja mpaka. True kabisa walikiwa watata hawa ndugu sio michezo. Ila Ibu alifariki ktk tukio la ujambazi nje ya Mbeya.
 
Bujibuji hapo namba sita umenikumbusha mbali sana. Mt. Livingstone ilikuwa bomba sana misosi yao babu kubwa na dining room yao ilikuwa inavutia sana. Disco lao pia lilikuwa bomba sana sijapita mitaa hiyo kipindi sasa.
 
Sina hakika lakini, za Bhanji ziliandikwa TRANS HIGHWAY CO. LTD
Huyo Bhanji ni mchumba tu, logistics company ya zamani ni Kanji Lalji Ltd wako pale jirani na Sisimba na pia wana yard yao kubwa Sinde jirani na Idara ya maji
 
Yaani niliwahi kuwa na boyfriend wa MTC,kipindi nasoma Mwakaleli high school,lkn masikani ilikuwa Mbeya Block T. Vurugu zake nilikoma,alikuwa akinitembezea kichapo popote hata anikute tu nimekaa na mtu wa jinsia tofauti hata kama ni ndugu yangu. MTC walikuwa washenzi bwana,makondakta na madereva walikuwa wanakiona.

Iyunga boys na MTC walikuwa paka na panya likija suala la Loleza girls. Ila ilikuwa poa sana
Hahahah loleza aka Loz watoto whiteee iyunga tuliwafaidi wakati Wa pini enzi zile.

Enzi zile ukivaa suruali ya khaki na tai nyeusi wanajua we Wa iyunga full heshima Kitaa.
 
Back
Top Bottom