Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Hawa ndio walikuwaga wababe enzi hizo......Daudi Masoke .....Janken....huyu jamaa alipigwa risasi na askari pale Mafiati .....alikimbia akaenda kufia Makunguru......wane star alikuwa mruka sarakasi tu hakuwaga mbabe though watu walikuwa wakimuogopa wakizani anajua kung fuu....Mwasimba mzee wa kubeba chuma enzi hizo....Kidos the killer ....Imma Kisogo wa forest ....pia kulikuwa na wakorofi kama akina Jagwa, Regge Man,Samadoh Jah mtoto wa makinda mby .....kundi la waswaken........bia yangu ya kwanza kunywa ...nimekunywa bar moja long time kitambo.....inaitwa vamponji....anyway tuache tu......
 
siku moja tulienda kucheza boli Rungwe sec basi kulikua na mawe ya kufa mtu dah ile match inaisha aisee walituvunjia vioo bus let, ila kweli Rungwe mlikua mnavuta sana bangi aisee.

Kama ile ajali ya kuanguka miti inayozunguka uanja wa Sokoine aisee nilinusurika nilikosa siti sikupanda, kuna mshkaji ni mlemavu hadi leo................

Mbeya bwana dah nina miaka mingi sijaish Mby ya wasafwa, wanyiha, wanyakyusa, wandali, mwagona mwe
 
Hawa ndio walikuwaga wababe enzi hizo......Daudi Masoke .....Janken....huyu jamaa alipigwa risasi na askari pale Mafiati .....alikimbia akaenda kufia Makunguru......wane star alikuwa mruka sarakasi tu hakuwaga mbabe though watu walikuwa wakimuogopa wakizani anajua kung fuu....Mwasimba mzee wa kubeba chuma enzi hizo....Kidos the killer ....Imma Kisogo wa forest ....pia kulikuwa na wakorofi kama akina Jagwa, Regge Man,Samadoh Jah mtoto wa makinda mby .....kundi la waswaken........bia yangu ya kwanza kunywa ...nimekunywa bar moja long time kitambo.....inaitwa vamponji....anyway tuache tu......
Umenikumbusha sana hawa walisumbua sana walikua wanafanyia machinjioni monde
sheta au mwasimba
kidos
Julius kajoleka
lutengano
huyu mwasimba alisumbua sana mpaka serikari ikamuajili kwaajili ya kutuliza ghasia machinjioni hapo
julius kajoleka alikua mtumishi misuli maalufu tz alishafanikiwa kufika south Africa kwa kutunisha misuri baadae wazungu w alikuja kumtafuta akacheze filamu hollwood baba yake akamkataza akamwambia ukienda huko hutaludi na kweli hakwenda na alikua na uwezo mkubwa wa kula nyama kilo nne mlo mmoja wanawake alikua hadumu nao
 
Cpwaa..Daz J..Isanga family..BizeBabu..Robo Corp..Ras Richy..Luggy..Adili..Buzax..Murady..Kambasonic..Mwalugaja..Yesu na Shetani
Kama unamfahmu biz bab ....hushindwi kumfahau rass jeff kapita....sisi ndio tulikuwa tuna run Mby wakati huo.....chapa sana vibao akina adili ....na kina leni makaya...long long time....
 
HII NDIO ILIKUWA MBEYA BWANA

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi, kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie Mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa Kiswele..engine nyuma, Dar - Mby faster, Mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya Ukweli,usisahau Mv Saratoga, Tunyande bus service, Zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa km 5 hivi, wachafu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. kiwanja ngoma, hapa Soka lilipigwa bwana, timu yangu ya Mtaa Snow White chini ya Key, kina Baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya Flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry Kichaa alikuwa na alergy na watu weupe, akikuotea atakukimbizaa na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa km Makao makuu ya vichaa walikuwa kibao

5.Pale Bomani palikuwa na Mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna,nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

6. Kipindi hicho Disco lilikuwa Mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa Wasape na Sugu- 2 Proud, hipop ilinoga bwana.

7. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi Wa Sinema pale opposite na Ofisi za Posta Town, Muvy ya Hatya ilifunika sana enzi zile.

8. Miaka ile bwana mvua ilikuwa inapiga km gharika,sometimes ilikuwa inamwagwa barafu km ulaya,mlima Loleza ulikuwa ukifunikwa theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina Shake.

9. Siku ya Jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa,mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale Mifugo,nyuma ya Kanisa la Roman,mkishamaliza kuogesha mnaanza kugombanisha Mbwa,mbwa Wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na Wa kienyeji ikiaminika wananguvu balaa.

10. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali,watoto walikuwa wanatoka maeneo kadhaa ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi,mang'ang'a,mafyulizi,mapohora,mapera nk.

11. Mwanjelwa.enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii, mitumba viwango,raba Kali,msela ukitupia vya doksi umemaliza.

12.Enzi zile ukisoma Sisimba na Azimio unafunika,Shule ya International ilikuwa Umoja primary school, waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa

13. Kuruka ukuta Wa Uwanja Wa Sokoine au kuingia uwanjani kupitia Bomba la maji ya mvua wakati Wa mechi ilikuwa ujanja balaa.

14. Ukisikia Shule za Sekondari Iyunga, Sangu, Loleza, Mbeya Day zilikuwa na kila aina ya sifa.Sangu kulikuwa na vichwa lazima uvitambue wababe km Simply na Kambosonic waliogopwa.

15. UMISETA sasa, dah, achaa..hapa Lutengano hapa Mwakaleli, boli lilitandazwa,kikinuka uwanjani ilikuwa km vita,makwanja na fimbo hujui vilipotokea,ukizubaa utakula mkono balaa

16. Kuna mdada walikuwa hatari alikuwa anatembeza kichapo kwa wanaume balaa walikuwa anatokea ilemi alifahamika kwa jina la Jeni.

17 Kuna jamaa alikuwa mtata sana mtaa Wa mafiati, makunguru, juakali alifahamika kwa jina la Daudi Masoke. Walikuwa balaa alikuwa anaiba Nyumba nzima hadi kitanda ulicholalia.

18. Ukisia mtaani Dunda, Kwendi, Shaban wanatembea mtaani wanaume wote kimya walikuwa hawaoni shida kukupiga dispiss ya tumbo. Wakitaka kupora walikuwa hawapati shida wanakuzunguka baada ya muda unaporwa ukipiga kelele hakuna Wa kukusaidia maana hadi wazazi wao walikuwa wanawaogopa.

19. Ukisikia obamka yaani ilikuwa full kwa watoto Wa mafiati, sinde, ilemi, isanga, ilolo ni sehemu ya kuchomea viazi mtoto walikuwa radhi asile nyumbani aende njelii kuokota viazi ili akachome obamka.

20. Uswahili tabu fresh food iligeuzwa jina na kuitwa Chakula barafu kiss vyakula vinahifadhiwa kwenye friiza. Expire date ya chakula hasa maziwa ilikuwa furaha kwa watoto Wa uswahili. Zaidi panaitwa city pub/century plaza.

21. Doxi waliwauzia wanyia blauzi na kuwaambia mashati. Ndio kisasi kikarudishwa unyiani na kuwaambia wamachinga Wa nguo Tumugoge tumuleshe...(tumuue tumuache).

NAIKUMBUKA MBEYA YA ZAMANI..
Kuna mabasi mengine kama Majira, Sasa kazi, Mgangaluma yalikuwepo
 
naskia ile barabara ya kutoka Rift valley kwenda chunya ina lami, na lile soko la Isanga limefutwa,hv uwanja ngoma upo bado?
a6c73e94f7cf88fde7738355946e1da0.jpg
 
Back
Top Bottom