Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Ustadh bitebo, kuna kipindi alifikia hatua ya kuchezesha mechi za TFF ligi ya mkoa. Bila shaka atakua amefika mbali sasa hivi.
Afike mbali wapi?
Kwanza alikua wa rushwa sana
Mbili alikua mwizi balaaa na alifungwa miaka kadhaa nadhan ulikua 2000+ sikumbuki alifungwa miaka mingap
 
Mzee umenikumbusha mang'ang'a, siku moja watoto wa uswazi mabatini tukapiga mguu mpaka Uzunguni. Tukaruka ukuta nyumba moja Hivi, tukapanda mti wa mang'ang'a, tukaanza uvunaji.

Lahaula, mwenye nyumba kutuona akafungulia mbwa..... Dah, tulikimbia mbio, ruka ukuta.... Kumbe mbwa kaishia getini, sisi kituo cha kwanza Azimio.
Hyo nyumba lazima itakua kwa dr Hera
 
Mbeya home yani daa napamic sn.

Ukienda uyole enzi hizo chips 300,
Za 500 unaulizwa mpo wangapi?

Daa block T mpaka pande za Iyela.
Boss chipsi 300?watu tumeanza chips 100 ukinunua za 150 unakula wawili mpaka watatu na zinabaki
 
Pale Sangu Sekondari ...kwenye miti kulikuwa na kichaka kinaitwa kaburi la Bob Marley watu wamekula sana ganja pale....lkn leo hii baadhi yao ni watu wakubwa sana hapa chini ya jua......
Itakuwa Unamuongelea Rais Wa Congo..Kabila
 
Enzi za Kiwanja ngoma nimepiga sana soka pale,jogobasha baadaye Blacktown ya Baragumu. Derby ya snowhite na Saitama ilikuwa inajaza balaa,kuna refa alikuwa anaitwa Bitebo maarufu kwa kupigwal,pembeni kulikuwa na baa ya Memba.
Bitebo refarii maarufu sijui yuko wapi, aisee! Mkuu ule uwanja umebaki historia. Kuna mdau maarufu wa Saitama Mecky nadhani unamkumbuka pia.
 
Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
Hahahaa..mwasimba..
 
Mtc..kipindi hicho..wana resort ya kimataifa..swiming pool ya kisasa..kiwanja court nzuri ya basket ball..ukienda kilimo-uyole..ndio utapapenda kuna viwanja vya golf.basketball, long tenis.pitch ya football iliyo jengwa na wa finland..mashamba makubwa ya matunda kama pitches...ukienda MTC..daah hapo walikua na indoor moja tz hakuna sakafu ya grass kwenye court ya basketball..hapo kulikua na vijana wanapiga sana kikapu..bila kumsahau Sam mkono..soccer yupo kikapu yupo..Iyunga dah..ilo camp ni kama jesh..tatizo usela ulizid shauri ya boyz..tofaut na sangu,meta ma brothermen na master duu..The buzax kalusha sn pinny..dj Lenney Makara..hataree..yaan mby ilikua full burudani
Wasanii enz hizo..Sugu,Mac T,Prof J, Sokomatola..kuntu alikua ana jiita panga mawe..meta sec..muuza pamba dox..alikua anavaa pamba kali jioni wadau wamenunua kesho anakuja na pamba kali zaid..
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Bob G alikuwa mzee wa magendo kutoka nchi mbalimbali hasa malawi. Alikuwa na cruiser wakati kipindi hicho polisi wana hyundai. Aisee Hatari mno. Nasikia jamaa alikuwa anafukuzwa na polisi akamwagaga rambo ya shilingi mia mia pale uyole watu wakaingia barabarani polisi wakashindwa kupita.
Kuna jamaa walikua wanaiba ng'ombe hata 30 na wanawaswaga barabani wakiwa na gobole na polisi wanagwaya. I miss that Mbeya
Kuna wakati nikiwa Lute camp Tukuyu Bob G alifurumshwa na pajero la uhamiaji akiwa na cruiser yake ile ya kizamani,akakatiza,ushirika akaingia shule lutengano akapaki nyuma ya vyoo kule kipwela. Jamaa wakatutuma njiani kuwapotosha polisi, walipoondoka wakafungua nyuma..wakatupa mfuko umejaa power No1 na kiroba cha calsberg na caton ya sukari. Duh..sitaki kukumbuka kilichotokea. Baba Minga (headmaster) aliongea mpaka meno yake ya bandia yakadondoka..Duh..mbeya ile..
 
Back
Top Bottom