Alim-over shine boss wake ugomvi ukahamia kwa wake zao

Alim-over shine boss wake ugomvi ukahamia kwa wake zao

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
13,019
Reaction score
14,947
Hili jambo nimelikumbuka,,,,
Hapo zamani za kale kulikuwa na miradi mbalimbali iliyokuwa chini ya serikali.,,,kama vile NAFCO...

kwa kifupi sijui ilikuwaje kuna jamaa akawa General Manager kwenye moja ya mashamba makubwa pahala...lakini kichwani ni kama vile "Trump''kwa sasa....

Pengine huyu jamaa "Jeuri ya Chama" ndio ilimbeba( zama za Chama kushika hatamu) .....hakuna ajuaye.....

Siku isiyokuwa na jina wakaja wageni kutoka mataifa ya dunia ya kwanza....ilikuwa ni kichekesho kisichokuwa na kifani....jamaa kujieleza ilikuwa ni taabu,,,lakini kiungwana msaidizi wake,,,alikuwa anaokoa jahazi mara kwa mara ....

Ugeni ulikaa pale mashambani kama wiki moja hivi kwa hiyo ilikuwa ni ziara kubwa sana, ...manake hata Waziri wa Kilimo wa nyakati hizo naye alikuwepo katika msafara huo.

NYakati za jioni wageni na maboss walikuwa wanajumuika katika 'Club' ya hapo mashambani...sasa yule bwana meneja alikuwa anakula kale "Keupe"...lahaula...vituko juu ya vituko matusi,kutukana n.k.

Ikifika asubuhi ziara inaendelea mashambani bwana meneja haonekani...kakamatwa na "hangover"...msaidizi wake ndio anaokoa jahazi na kujaribu kuficha aibu....(waziri alishaona mapeema) lakini kiungwana akamezea tu,

Mzaidizi angalau lugha ilikuwa inapanda kwa hiyo aliimudu ziara mpaka siku ya mwisho.

Siku wageni wanaondoka, walimpongeza sana yule msaidizi..makofi yakapigwa wafanyakazi wakamshangilia...lakini yule bwana meneja walimshukuru tu kiungwana...na ikawa baridi bila makofi.

Wageni wakaondoka ,,,wenyeji wakabaki...vikaanza vijembe...kati ya familia ya bwana meneja na msaidizi wake....wake zao wakaanza kuchambana kwa kutumia radio kaseti wanafungulia taarabu kwa sauti za juu....

Maneno yakasambaa mpaka mashamba ya jirani na vijijini......

SWALI
Hivi yale mashamba ya NAFCO yalikufaje kufaje?? manake walikuwa wanavuna usipime.
 
Back
Top Bottom