Mbeya: Nilikumbana na Mauza Uza ya Wachawi

Mbeya: Nilikumbana na Mauza Uza ya Wachawi

de Gunner

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
11,366
Reaction score
22,551
Katika mikoa niliyo tembea hapa Tz mbeya ni kiboko...

Ndo maana kuna makanisa mengi sana, wale jamaa ni wachawi vibaya mno.

Baada ya kumaliza chuo nilienda mbeya kujitafta hiyoo ilikuwa mnamo 2021... Nilikuwa na marafiki zangu huko. Tulipata mchongo private sector.

Tukapanga vyumba sehemu moja. Mwenye nyumba alikuwa mtu poa sana. Ila kimbembe ni wale majirani wa karibu na ile nyumba.

Walikuwa wanamazoea sana. Sasa mimi ni mtu flani ambae niko reseverd sana, huwa sipendi mazoea na watu unless yaani tuwe tunafahamiana na tumezoeana. Sipendi umbeya, sipendi kuongelea watu vibaya. Sipendi majungu.

So pale wale marafiki zangu ndo Wali tokea kuzoeana sana na wale majirani. Mimi upande wangu ilikuwa salamu tu, maybe stori mbili tatu... Ila ile kujua a sana haikuwa kipaombele changu.

Haya bwana, mimi huwa sina shida na watu kabisa, ila kwa ile jinsi tu nilivyo walidhani ya kuwa najiona sana. Wakadhani mimi mbinafsi(at least nadhani ndo walidhani hivyo)

So tumeendelea kuishi wale jamaa Wakawa so invested na wale majirani yaani mtu anakuwa kama Mwana familia kabisa wa watu asiowajua...

Long story short wale jamaa hawakufanikiwa kubaki kwenye kampuni maana hawakuwa serious. Walienda bata basi wa karudi zao makwao wakaniacha mimi... Ila cha kushangaza nikiwa majirani wakadhani mimi nimewachongea jamaa zangu wafukuzwe... Hiyo haitoshi wakawa wanawapigia simu wananisemea vibaya eti najiona na sina ushirikiano nao, wakati hakuna siku nimewahi kukwazana na mtu pale mtaani na hata kama kuna shida huwa nafix kama na uwezo..

Basi bwana, baadae mambo yakanikali sawa nmshahara ukapanda nikaanza kuenjoy, maisha ya kawa mazuri mpaka nikaanza kutafta kiwanja.. Badala ya kupoteza muda kutembea nikanunua boxer ya usafiri. Nikaanza kutafta pia frame japo na mimi nianze kuwekeza kwenye biashara.

Ila sasa wakuu, kimbembe kilikuja kunikumba... Yaani that year mshahara umepanda nilianza kuona mauza uza kwanza kazini mpka mtaani.

Kazini boss hanielewei, Daah kuna demu wa chuo nilikua nakula mara akaanza mauza uza, haya mara nikute magetoni mtu kamwaga ugali mlangoni... Aisee na nilikuwa nimeshalipa miezi 6. Wale majirani walikuwa hatari... Mimi huwa napenda watoto, lazima ni kukutana na dogo lazima ni Mwache na hela jero kawaida tuu. Ila kuzoeana na watu ilikuawa taabu..

Kinacho nifanya nisizoeane na watu ni kuwa kuna mapito maishani ambayo yame nifanya nisiwe open kwa watu ni sio wajua... (even the devil was once an angel)

Ebwanaa eeh ilifikia hatua maisha haya kuwa na amani kabisa... Kuanzia kazini mpka mtaani. Kuna siku siku niliugua kidogo nife kabisa... Alaf haukuwa na mtu demu wangu kashaniblock alaf watu napatana nao hasa makazini walikuwa wakiishi mbali na nilipo kuwa naishi.. Kugongea majirani hakuna anaeitikia wakati wao kila day mtu akiwa na shida mm sishindwi kuwasaidia

Basi bwana, mauza uza haya kuisha... Kuna siku aisee nimefika kazini kuna kazi niliachiwa na boss ilikuwa ya muhimu sana... Wadau sijui hata nielezeje sikuwa na kumbukumbu hata kazi inafanywaje na huku nimefanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka mzima.. Nilidata yaani ni kama ubongo ulikuwa empty set... Kila nilijaribu ku recall sikumbuki.

Hapo ndo nilitambua kuna juju hapa. Nilitambua kabisa hii kuna mtu ananichezea... Niliaga kwa boss sijisikii fresh nikaenda hospital hapo sielewi nini hata kimetokea.. Kila nikiwa a mpaka leo Nashindwa kuelewa.

Aisee nilionge na bibi yangu nikamwelezea the whole thing.. A kasema huenda ni mimi na uchovu wangu tu.. Nikamwambia this is enough narudi home..

Sikuaga, si kumwambia mtu yeyote kazini, nika badili laini. Nilivyo fika home nilikesha nalia kwa kusali maana niliona hakuna namna mtu ata elewa nacho pitia.. Nilisali rozali mara sijui ngapi..

Wakuu omba yasikukute, wachawi wapo ndugu zangu na hapo ndo kilikuja kutambua ya kuwa lazima uwe na Mungu ndani yako, lazima uwe na imani ya kuwa Mungu ndo muweza wa yote.

Nilikuwa nasali mpaka natetemeka aisee. It was hell. Ila baada ya kama mwezi hivi nilirudi katika hali ya kawaida. Na hapo ndio niliekuja kujua Mungu yupo.

Zamani nilikuwa athiest mzuri kuwaonya wafia dini wajinga, ila baada ya ile incident Nilijua kabisa kuna Mungu sio huyo tunayehubiriwa makanisani bali yule aliye ndani yetu. Mimi sio mtu wa Kukesha kanisani ila nina imani kubwa sana.

Sajasema mbeya sio Sehemu nzuri, la hasha ila kwa yalivyo nikuta kule sitosahau maishani.

Kingine nilijifunza kutokuwa na umimi sana, sometimes watu hawapendi mtu wa namna hiyoo ingawa huenda mtu maisha ndo yanamshepu kuwa hivyo

Nani alisha wahi kupitia mauza uza ya namna hii?
 
Ukienda ugenini kaa kimaster mkuu, ule usemi mpe mchawi akulelee mtoto wako nadhani haukuelewa mapema, hao wanauliokua unawakataq ndio wangekua guardian angels kwakukusanua , ukute landlord ndio mwanga
 
Kutopenda umbea haimaanishi usichangamane na jamii inayokuzunguka hasa kwenye mambo ya msingi, kama misiba, sherehe, shughuli shirikishi mtaani etc. Ukihusika huko lazima mtajuana, mtaongea, na jamii itapata fursa ya kukuelewa tabia yako hta kama ni mkimya wa asili.

Ukimya wa bila majivuno ni tofauti sana na ukimya wenye kiburi na majivuno, na mtu yeyote mzima anaelewa tofauti yake mkuu. Je hukua karibu na majirani zako wote? Tafakari huenda kuna sehemu uliteleza mkuu, mara nyingi jamii ni mwalimu mzuri.
 
Ukienda ugenini kaa kimaster mkuu, ule usemi mpe mchawi akulelee mtoto wako nadhani haukuelewa mapema, hao wanauliokua unawakataq ndio wangekua guardian angels kwakukusanua , ukute landlord ndio mwanga
Mkuu hata sielewi aisee ila kwa mauza uza yale sirudii kuishi tena mbeya. Sometimes nilihisi wadau walosepa walifanya madawa kishirikina na wale majirani... It was hectic
 
Kutopenda umbea haimaanishi usichangamane na jamii inayokuzunguka hasa kwenye mambo ya msingi, kama misiba, sherehe, shughuli shirikishi mtaani etc. Ukihusika huko lazima mtajuana, mtaongea, na jamii itapata fursa ya kukuelewa tabia yako hta kama ni mkimya wa asili.

Ukimya wa bila majivuno ni tofauti sana na ukimya wenye kiburi na majivuno, na mtu yeyote mzima anaelewa tofauti yake mkuu. Je hukua karibu na majirani zako wote? Tafakari huenda kuna sehemu uliteleza mkuu, mara nyingi jamii ni mwalimu mzuri.
Hasa hasa ilikuwa ni salamu nilikuwa kama kupiga stori mmekutana tu nje ile asubuhi ila ule ukaribu wa kukaribishana ndani sikuwa nayo kabisa na hata nikikaribishwa nilikuwa naenda kama kuzuga tuu. Actually walionekana ni watu wanapenda kuzungumzia maisha ya watu wengine sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom