Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
Mkuu umenichekesha sana...!
 
Japokuwa sio mzawa wa Mbeya ila nilienjoy sana wakati huo nasoma Southern Highland. Kuna wahuni Sido waliniibia pesa yangu wakati nimeenda kudaka nguo asubuhi. Mbeya taam sana Mamajoni, Hali ya hewa(airport ya zamani), Isengo, Pambogo, Block T, Soweto, Ilomba, Maendeleo hizo zote zilikuwa pande zetu
 
Mkuu kumbe tumesoma shule moja na darasa moja halafu ulikuwa rafiki yangu wa karibu sana, unamkumbuka Joseph ndimbo?, tulikuwa darasa moja na hamidu na amidu
Hapo sasa! Namkumbuka sana!
Shule yetu ilikuwa ikipangwa ki madaraja, ilikuwa namba moja, ndio inafuata Sisimba. Hao akina Itiji, Majengo, Mbata (Shule aliyosoma Mwambusi wa Yanga) zote zilikuwa madaraja ya chini!
Mapumziko, SOMBRERO HOTEL kununua Bagia, au kwa MWADADA kununua ndizi na MAKATAPERA, pale karibu na duka la yule Muhindi KIGHILI!!
 
Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
Hahhahaha kuna Dada mmoja Nae alikuwa na matatizo ya Akili Dox pale walikuwa wanamuita Tabu kila mwaka anazalishwa.
mbeya kitambo
 
Baba David pia
David alikuwa mpole sana,akilipiga dude utamuona macho yanakuwa madogo halafu mabichi.Radio ya gari imefungwa kwenye kitanda,cassette ni Bob Marley, Lucky dube, Gregory Isaac, Alfa Blondie. Sunday akitoka kuuza mchicha na Mponjo akija zinachangwa tayari kwa matumizi
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Bob G alikuwa mzee wa magendo kutoka nchi mbalimbali hasa malawi. Alikuwa na cruiser wakati kipindi hicho polisi wana hyundai. Aisee Hatari mno. Nasikia jamaa alikuwa anafukuzwa na polisi akamwagaga rambo ya shilingi mia mia pale uyole watu wakaingia barabarani polisi wakashindwa kupita.
Kuna jamaa walikua wanaiba ng'ombe hata 30 na wanawaswaga barabani wakiwa na gobole na polisi wanagwaya. I miss that Mbeya
Bob G jirani yetu...alishafariki
 
Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
Aliitwa MWASIMBA,KITONSA,BABU AU SHETANI.
 
Cpwaa..Daz J..Isanga family..BizeBabu..Robo Corp..Ras Richy..Luggy..Adili..Buzax..Murady..Kambasonic..Mwalugaja..Yesu na Shetani
IPP-Isanga Peoples Party,Mwalugaja unamaanisha Laurent?alisoma Olevel kipoke wenye kiwira motel?
 
Walikuwa wanakaa mitaa ya kishua jirani na kwa mehrab,mzee malakasuka alikuwa na kampuni inaitwa GHANA BUILDING CONTRACTORS.Walikuwa na hela na walitugonga sana tu.
Waliwagonga?? Unamaanisha walikuwa wanawa***** wanawake??
 
Back
Top Bottom