Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
Kumbe wewe ni wa Mbeya.....ndio maana Kuna ugoloka fulani
 
Nikajua unamzungumzia dr BERN ambaye alikuwa anafanya kazi rufaa naye alioa Mzungu
 
Nilichomoka longtime kitambo miaka kumi na tano sijarudi huko .....by the way utambulisho ndio hilo rass jeff kapita....hiyo timu ya forest nimecheza na akina robyo mwasalemba,hamis chepe chepelino.....maja,zungu,abuu kasanga
etc,etc ...niambie ww unatokea angle ipi ......ama ww ni mtoto wa mzee nani nitakuelewa
Mimi Sajo, hao madogo walikuwa bado wanacheza chandimu wakati mimi nacheza Rockers United.Dogo wangu aliitwa Prince Lugax rapa wa mwanzo mwanzo kampani ya kina Sugu
 
Pia kulikuwa na huyu jamaa Banyambala Kaka, alikuwa na coaster za kyela, mwanzoni miaka ya 2000 alikuwa anaendesha mke wake coaster moja hv. Pia kulikuwa na magari ya Buffalo alikuwa anamiliki mama Jane, huyu mama alisifika sana kwa uchawi na hata kifo chake kilikuwa cha kutatanisha.
 
Nliondoka mbeya nikiwa mdogo sana...km 4-5 yrs...huyo jombi tulikuwa tunakaa jirani...alikuwa akitokea watoto wote mbio...nakumbuka alikuwa na Nissan patrol km sikosei...nakumbuka hatukuwa mbali sana na shule ya mwenge,kulikuwa na hotel inaitwa mbeku,sikumbuki ni uwanja gani ila huo uwanja walikuwa wanautumia sana waubiri akina Moses klola...tulikuwa na tabia ya kula miti ya mahindi mabichi...kama miwa tunaita migagi......nakumbuka kulikuwa na maziwa flan hv ya mgando yamepakiwa katika pakiti zenye rangi ya kaki na kijani yamekaa umbo la pyramid..kuna matunda flani yanaitwa songwe(sikumbuki vizuri) ila nimekumbuka mbali sana sana...especially marehemu mama angu...dah wakati umeenda wapi?
 
Hapo sasa! Namkumbuka sana!
Shule yetu ilikuwa ikipangwa ki madaraja, ilikuwa namba moja, ndio inafuata Sisimba. Hao akina Itiji, Majengo, Mbata (Shule aliyosoma Mwambusi wa Yanga) zote zilikuwa madaraja ya chini!
Mapumziko, SOMBRERO HOTEL kununua Bagia, au kwa MWADADA kununua ndizi na MAKATAPERA, pale karibu na duka la yule Muhindi KIGHILI!!
dah hapa mkuu ndo umenkumbusha mzee mwadada anatoa makatapera kalobe na itende anapeleka mpaka sokomatola kwa miguu dah R.I.P mzee mwadada
 
Back
Top Bottom