Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh. James Mbatia ameonyesha mfano wa kuigwa katika kusaidia shughuli ya uokoaji wa waathirika wa jengo lililoanguka jijini Dar es Salaam tarehe 29.32013. Hayo yameelezwa na walioshuhudia jinsi kiongozi huyo wa upinzani alivyokuwa hodari katika kutumia ujuzi wake kulinufaisha taifa katika janga hili.
Hatua hii ni tofauti na mwenyeti wa chadema Freeman Mbowe ambaye alichokifanya ni kwenda kwenye mitandao ya kijamii kulifanyia kejeli janga hili kubwa kwa taifa.
Kamera za waandishi wa habari zilifanikiwa kupata picha kadhaa za jinsi mh. Mbatia alivyoonyesha umuhimu wa kuweka siasa pembeni katika majanga na kutoa kipaumbele kwenye kuisaidia jamii kuwa salama kwanza.
Hongera mh. Mbatia, hongera NCCR kwa kuwa na mwenyekiti shupavu.
View attachment 88608
Mh. Mbatia akitoa maelekezo ya hatua muhimu za kuchukua kuokoa waathirika.
View attachment 88607
Rais Kikwete akimshukuru na kumpongeza mh. Mbatia kwa mchango wake mkubwa kwenye kuokoa waathirika.
View attachment 88609
Wananchi wakimshukuru mh. Mbatia kwa msaada mkubwa alioutoa kuokoa waathirika.