Mbatia ameonyesha mfano wa kuigwa...

Mbatia ameonyesha mfano wa kuigwa...

Kwa maoni mliyochangia wenzangu huyu mleta uzi atalaani kwa nini alianzisha huu uzi na kamwe hawezi kujibu hoja hata moja. nashukuru mmempa stahili yake.
 
Nadhani ungekuwa na hoja km ungesema hivi: 'sera ya ccm ni kuua raia wake kwa njia mbalimbali kisha kujitokeza haraka kwenye eneo la tukio huku wakiwa wameandaa wapiga picha za video ili waonekane wanajali kwenye TV'. Tatizo lao ni kwamba serikali iliyo chini ya ccm ndiyo imesababisha madhara yote haya kwa kuyaachia mambo yaende hovyo hovyo ilimradi wao wamekula rushwa inatosha. Hivi unadhani km kungekuwa na usimamizi mzuri wa ujenzi hiyo ajali ingetokea? Au ndo unataka kusema ni mapenzi ya mungu? Majengo mangapi yameanguka temeke, sinza na sasa kariakoo ndani ya utawala wa JK, amechukua hatua gani? Unajua kesi za wahusika zilikufaje? Je tume ya Lowassa na mapendekezo yake ya 2008 ilifanyiwa nini? serikali hii hii ya ccm ilijifunza chochote? Je ilirekebisha kasoro au iliona vyema raia wasio na hatia waendelee kufa, huku kazi yao ni kutoa salaam za pole na kauli zisizotekelezwa za kuwa wahusika wote watashughulikiwa? Sasa chadema unataka wawe wanakimbia kimbia kwenda kwenye misiba km JK badala ya kutafuta suluhisho la matatizo ya majanga yanayozuilika? Unataka hata km hawapo karibu na eneo la tukio wakimbie kimbie ilimradi tu wapigwe picha za magazeti na TV? Mbona huulizi Pinda alikuwa wapi jana? Mbona Nape, mwigulu na Kinana hatukuwaona hapo? mbona hawakutokea? Unadhani wote walioshiriki kuokoa hawakuwemo wanachadema? Hili ndiyo tatizo la siasa zetu za kutafuta sifa na siyo 'utendaji' madhubuti.
Ndugu wana JF na watanzania nimefuatilia misiba mikubwa km kuzama kwa meli. Pia sijona chama cha CHADEMA; Kipindi cha uokozi ; ushauri wangu CHADEMA tuma mwakilishi katika jengo lilioanguka posta ili imani ya wapenzi wa chama iongezeke;

Mbowe na slaa onyesha mfano kama Mbatia kipindi cha uokoz
 
Matatizo ya Tanzania mengi ni ukosefu wa UZALENDO............haya mengi mbwembwe tu
 
Mbatia amekomaa kisiasa na ndio maana kama kiongozi wa chama alifika kwenye tukio kuungana na wananchi .
Wengine wamekaa nyumbani wanasubiri kesho watoe TAMKO na kuitisha maandamano nchi nzima.
Wao ni kama kufa kufaana, yaani wengine wakipatwa na majanga wanatumia kama mtaji wa kujipatia umaarufu wa kisiasa
Viongozi wa kweli ni wale waliofika kwenye eneo la tukio, sio kurusha comments kwenye face book
When you are good , You are good! No wonder why Mheshimiwa Rais alimteua mbunge wa viti maalum, ni kwa sababu aliona kipaji cha huyu bwana
Upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali, upinzani ni kuwaonyesha wananchi kuwa utawafanyia zaidi ya yanayofanywa na serikali ya sasa au kuyaboresha.

Ubongo kama ungekuwa unavaa nguo basi wa kwako uko uchi! Mbatia yuko pale zaidi kama mtaalamu wa disaster management kuliko kama mwanasiasa.....Dr Sarungi alikuwa anafika katika matukio kama haya nkama mtaalamu wa mifupa....sio kila kitu ni siasa ! NIKUJUZE TU KUWA hata JK hakupaswa kuweko pale twice katika stage za awali ajali hii kwa kuwa uwepo wake una desrupt rescuing processes!
 
I think we are missing the big picture here. Mwenye jukumu la kushughulikia maafa nchini ni serikali. Yalipotokea mafuriko ya Katrina New Orleans ni serikali ya Bush ndiyo ilikuwa na dhamana ya kushughulikia maafa hayo, na ililaumiwa ipasavyo kwa kushindwa kuokoa maisha ya watu katika muda muafaka. Mafuriko yaliyotokea New York na New Jersey wiki mbili kabla ya uchaguzi wa mwaka jana Obama aliwajibika ipasavyo. Akishirikiana na gavana wa New Jersey alitoa ahadi kuwa serikali itahakikisha kuwa wahanga wanapewa msaada haraka. Hivyo ndivyo wenzetu wanavyofanya. Wanayo system in place na si kutegemea msaada wa mtu mmoja mmoja kama Mbatia na kumwona shujaa wakati system yetu ni a total failure. Hii si mara ya kwanza kwa jengo kuporomoka Dar-es- Salaam na ninaamini haitakuwa ya mwisho. Tumejifunza nini kutokana na jengo lililoanguka Chang'ombe? Nothing. Tumeweka in place utaratibu gani wa kushughulikia maafa kama hayo? Nothing. Kwa hiyo hii ya kumsifia Mbatia ni kutaka kupotosha lengo kuwa hatuna utaratibu wowote wa kushughulikia au kuzuia maafa kama haya nchini mwetu.
You have a point dude!!!!!
 
Mleta mada ulitaka nani waje pale kutoa msaada.?
Mpaka ghorofa inajengwa inafika floor ya 14 hakuna ukaguzi wowote ule hii nchi ina kiongozi kweli?

Kuendekeza ujinga na unafiki ni kitu kibaya sana.
 
Hii nchi ni ya ajabu sana, yaani watu na akili zao (sijui kama hizo akili zipo), wanakaa kusubiri majanga yatokee ili wapate nafasi ya kwenda kuuza sura na kupiga picha za kuonesha kwenye vyombo vya habari?. Huyo rais wa nchi aliyewahi mbio kwenye tukio akiambatana na mke wake alitoa msaada gani zaidi ya kubaki kushangaa kama wananchi wengine. Kuanza kutoa lawama na kunyoosha vidole kwa mtu mmoja mmoja wakati hili janga ni la taifa huo ni ujinga na kukosa uelewa.

Tunafahamu wazi kuwa kitengo cha maafa kipo na kinasimamiwa na Waziri Mkuu. Rais au Waziri Mkuu mwenyewe awaeleze Watanzania hicho kitengo kinafanya kazi gani wakati haya majanga sio mara ya kwanza kutokea hapa Tanzania. Imefika wakati sasa Serikali ikiri wazi kuwa imeshindwa kutimiza wajibu kwa raia wa Tanzania; watu wanakufa kwa mambo yanayoepukika kabisa lakini cha kushangaza viongozi wanabaki kukimbilia kwenda kuhani na kutoa pole kwa wafiwa pasipo kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo.
 
Mbatia amekomaa kisiasa na ndio maana kama kiongozi wa chama alifika kwenye tukio kuungana na wananchi .
Wengine wamekaa nyumbani wanasubiri kesho watoe TAMKO na kuitisha maandamano nchi nzima.
Wao ni kama kufa kufaana, yaani wengine wakipatwa na majanga wanatumia kama mtaji wa kujipatia umaarufu wa kisiasa
Viongozi wa kweli ni wale waliofika kwenye eneo la tukio, sio kurusha comments kwenye face book
When you are good , You are good! No wonder why Mheshimiwa Rais alimteua mbunge wa viti maalum, ni kwa sababu aliona kipaji cha huyu bwana
Upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali, upinzani ni kuwaonyesha wananchi kuwa utawafanyia zaidi ya yanayofanywa na serikali ya sasa au kuyaboresha.

VP WE ULIFIKA ENEO LA TUKIO NA UKATOA MSAADA?COZ NAWE NI KIONGOZI WA SIASA.AU UMEPISHANA NAYO?

  • :censored:

  • A%20S%2039.gif

Mbona maelezo yako hayatoi taarifa sahihi kama picha ulizoweka zinavyoeleza. unasema ameshiriki kikamilifu ktk kuokoa waanga wa ajali hiyo,huku picha zikionesha anashiriki kikamilifu kusalimia wato. ACHANA NA KUTAFUTA CHEAP POPULARITY.
 
Wewe ubongo wako naona umeoza kwa sababu ya kupewa vya bure!! Kweli unataka kutuaminisha kwa nguvu kuwa hao vibaraka wenzako kama Mbatia na Kikwete wanaosubiri ajali zitokee tena kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu ni bora kuliko wale wanaopiga kelele kuzizuia!? Huendauna ugonjwa mbaya sana unakusumbua....

Nadhani unachotakiwa kufanya kwanza ni kujifunza maana ya KUZUIA. Janga likishatokea hapo kipaumbele sio kuzuia ila kwanza ni kuokoa waathirika na kuwapa msaada wanaostahili.

Ni kituko kuona mtu anayetaka kuwa kiongozi wa kitaifa anaona janga limetokea, hata waathirika hawajatolewa kwenye kifusi yeye "ANAPIGA KELELE ZA KUZUIA". Sasa hapo anataka kuzuia nini wakati chini wa kifusi kuna watu wako hai wanangoja waokoaji wafanye bidii itakayoamua kama watatoka wakiwa wazima au wafu!

Tatizo lenu chadema IMEWALAGHAI kiasi kwamba hamna tena uwezo wa kufikiri zaidi ya kufuata upepo unaopulizwa na Mbowe na Dr. Slaa (chini ya amri ya Mzee Edwin Mtei). Ndio maana mnaona mtu aliyesema kuwapa pole wafiwa hakuna umuhimu amefanya la maana kuliko yule aliyekimbia kwenye tukio kusaidia waathirika...
 
Hayo ni mawazo ya ki-mbulula kwa ma-mbulula kama wewe. Huwezi kuwasha moto nyumba halafu inapowake eti unakimbilia kuokoa!
 
I think we are missing the big picture here. Mwenye jukumu la kushughulikia maafa nchini ni serikali. Yalipotokea mafuriko ya Katrina New Orleans ni serikali ya Bush ndiyo ilikuwa na dhamana ya kushughulikia maafa hayo, na ililaumiwa ipasavyo kwa kushindwa kuokoa maisha ya watu katika muda muafaka. Mafuriko yaliyotokea New York na New Jersey wiki mbili kabla ya uchaguzi wa mwaka jana Obama aliwajibika ipasavyo. Akishirikiana na gavana wa New Jersey alitoa ahadi kuwa serikali itahakikisha kuwa wahanga wanapewa msaada haraka. Hivyo ndivyo wenzetu wanavyofanya. Wanayo system in place na si kutegemea msaada wa mtu mmoja mmoja kama Mbatia na kumwona shujaa wakati system yetu ni a total failure. Hii si mara ya kwanza kwa jengo kuporomoka Dar-es- Salaam na ninaamini haitakuwa ya mwisho. Tumejifunza nini kutokana na jengo lililoanguka Chang'ombe? Nothing. Tumeweka in place utaratibu gani wa kushughulikia maafa kama hayo? Nothing. Kwa hiyo hii ya kumsifia Mbatia ni kutaka kupotosha lengo kuwa hatuna utaratibu wowote wa kushughulikia au kuzuia maafa kama haya nchini mwetu.

Kudos Mkuu. Tuache mambo ya personality cult tuongelee kuunda chombo cha kushughulikia maafa. Huyo Mbatia peke yake hawezi kufanya kitu.
 
Wewe ni mwandishi kidampa na mchumia tumbo tu. Huna lolote na mawazo yako yanaongozwa na tumbo lako

Vijana wengi wa chadema wakikosa hoja huwa wanaishia hapahapa ulipoishia wewe. tumeshawazoea walaghaiwa...
 
Mbatia amekomaa kisiasa na ndio maana kama kiongozi wa chama alifika kwenye tukio kuungana na wananchi .
Wengine wamekaa nyumbani wanasubiri kesho watoe TAMKO na kuitisha maandamano nchi nzima.
Wao ni kama kufa kufaana, yaani wengine wakipatwa na majanga wanatumia kama mtaji wa kujipatia umaarufu wa kisiasa
Viongozi wa kweli ni wale waliofika kwenye eneo la tukio, sio kurusha comments kwenye face book
When you are good , You are good! No wonder why Mheshimiwa Rais alimteua mbunge wa viti maalum, ni kwa sababu aliona kipaji cha huyu bwana
Upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali, upinzani ni kuwaonyesha wananchi kuwa utawafanyia zaidi ya yanayofanywa na serikali ya sasa au kuyaboresha.

Uko biased sana kimawazo, bado mchanga sana katika uchangiaji na uelewa wa maisha.
 
Kichwa chako hakina hoja wewe. Tumbo lako ndio lina hoja!!!!

Kwako wewe mlaghaiwa unaona Mbowe aliyesema kuwapa pole wafiwa sio muhimu amefanya la maana sana kuliko Mbatia aliyekimbilia kwenye tukio kusaidia waathirika, na mpaka sasa Mbatia hajatoa kauli yoyote ya kisiasa.
 
Nadhani unachotakiwa kufanya kwanza ni kujifunza maana ya KUZUIA. Janga likishatokea hapo kipaumbele sio kuzuia ila kwanza ni kuokoa waathirika na kuwapa msaada wanaostahili.

Ni kituko kuona mtu anayetaka kuwa kiongozi wa kitaifa anaona janga limetokea, hata waathirika hawajatolewa kwenye kifusi yeye "ANAPIGA KELELE ZA KUZUIA". Sasa hapo anataka kuzuia nini wakati chini wa kifusi kuna watu wako hai wanangoja waokoaji wafanye bidii itakayoamua kama watatoka wakiwa wazima au wafu!

Tatizo lenu chadema IMEWALAGHAI kiasi kwamba hamna tena uwezo wa kufikiri zaidi ya kufuata upepo unaopulizwa na Mbowe na Dr. Slaa (chini ya amri ya Mzee Edwin Mtei). Ndio maana mnaona mtu aliyesema kuwapa pole wafiwa hakuna umuhimu amefanya la maana kuliko yule aliyekimbia kwenye tukio kusaidia waathirika...
Nilipoona heading na attacment za picha, nilidhani mbatia alikuwa busy akibeba waathirika, kumbe mfano wenyewe wa kuigwa ni wa kusalimiana na watu?
 
Back
Top Bottom