Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,128
- 8,058
Hapa JF kuna watu wana maneno yanayochoma kama mkuki, hata hivyo bado kuna watu wanaobaki kuwa na mioyo ya upendo, subira na busara hata wakirushiwa mikuki ya dhihaka na kejeli. Mmoja wa watu hao ni Lucas Mwashambwa — mtu ambaye licha ya kupingwa vikali, kushambuliwa hoja zake, na kukosolewa mara kwa mara, bado haachi kuwaona wakosoaji wake kuwa ni "ndugu zake"
Ni rahisi sana kuwapenda wanaokupenda, kuwasifu wanaokusifia, na kutoa tabasamu kwa wale wanaokupongeza. Lakini inahitaji moyo uliojaa neema, imani na unyenyekevu mkubwa kuendelea kuwaita wanaokubeza kuwa ni “ndugu.” Hiki ndicho kinachomtofautisha Lucas Mwashambwa na wengi wetu. Anaishi kama Maandiko yanavyotufundisha tuishi.
Yesu alisema:
“Lakini nawaambieni nyinyi mnaonisikiliza, wapendeni maadui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni. Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.."(Luka 6:27-28)
Akaongeza tena:
“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.." (Luka 6:32)
Lucas Mwashambwa kwa kuendelea kuwaita “ndugu zangu Watanzania” wale wanaomshambulia, anatimiza kwa vitendo maagizo matakatifu ya Yesu. Ndio sababu nasema huyu ni mfano bora wa kuigwa, kwa sababu anajua kuuenzi utu hata pale ambapo wengine wanamnenea mabaya. Lucas Mwashambwa anatambua wazi kwamba tofauti za mawazo hazipaswi kufuta undugu wetu wa kibinadamu.
Lucas Mwashambwa, ametufundisha kwa vitendo kwamba mtu anaweza kutetea mtazamo wake bila chuki. Anaweza kupingwa bila kulipiza kisasi, na anaweza kuendelea kuona thamani ya wale wanaomtusi , kwa sababu ndani yake, anawaona kuwa ni ndugu zake.
Nimeona niandike uzi huu kwa sababu Biblia inanihimiza kufanya hivyo katika kitabu cha Wafilipi 4:8.
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yapendezayo, yo yote yenye sifa njema, ukiwapo wema wo wote, na sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."