MB DOG: Diamond Platnumz amenidhulumu wimbo wa Mapenzi Kitu Gani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1689275265491.png
"Google wimbo huu wa Mapenzi Kitu gani au ingia YouTube halafu ataona. Nenda kwenye more Information utaona jina la Msanii aliyeimba wimbo huu imeandikwa jina la #DiamondPlatnumz. Ubunifu kama huo lakini nikitaka kuutumia napigwa stop. Unapotaka kuutumia kwa ajili ya maisha ya familia ili nipate kitu chochote siwezi"

"Na wakati natunga huu wimbo mwaka 2008. Diamond alikuwa bado Sana kwenye Muziki. Nina ushahidi wote kuhusu huu wimbo tangu sikubya kwanza naandika mashairi. Producer alikuwa Man Water. Nilijaribu kuzungumza na management yake lakini nilikosa nafasi. Nilikwenda COSOTA namshukuru Madam Doreen alipambana kwa nafasi yake. Walifuatilia mwaka mzima bila mafanikio yoyote. Kuna kiongozi mmoja Serikalini aliniita nikajua nitapata haki yangu lakini nikaambia niachane na paste niangalie future"

"Nikiusikia huu wimbo unalia huwa nakaa chini nafikiria hata maisha yangu ya kawaida na nyumbani ninavyopambana na familia yangu halafu Mimi siwezi kuiba, kukaba ambacho Mungu amenibariki ni kufanya kitu na kufanya watu waweze kupata burudani.

"Niseme ukweli Ngoma zangu kuanzia Latifa kwenye platform hizi sijawahi kupata pesa. Hakuna audio yangu yoyote ambayo sina leseni zote zimelipia ushuru. Wasanii wengi wa Bongo wanadhulumika lakini haki zao za msingi hawazipati" @mbdogg_Master
1689275318961.png
 
"Na wakati natunga huu wimbo mwaka 2008. Diamond alikuwa bado Sana kwenye Muziki. Nina ushahidi wote kuhusu huu wimbo tangu sikubya kwanza naandika mashairi. Producer alikuwa Man Water. Nilijaribu kuzungumza na management yake lakini nilikosa nafasi. Nilikwenda COSOTA namshukuru Madam Doreen alipambana kwa nafasi yake. Walifuatilia mwaka mzima bila mafanikio yoyote. Kuna kiongozi mmoja Serikalini aliniita nikajua nitapata haki yangu lakini nikaambia niachane na paste niangalie future"
Mmmh mwamba kaanza kudata au, mbona huu wimbo upo kwenye album ya "si uliniambia" na hii album ilitoka around 2005 au 2006. Yeye anasema aliutunga 2008😁
images (9) - 2023-07-14T054634.781.jpeg
 
Ina maana Diamond kaupost huo wimbo kwenye ukurasa wake au youtube channel anapiga pesa au? Afu hiyo channel ya utube mbona sio ya Diamond huyo MB Dog kaanza kuvuta nini?

Yeye alie na huyo zerokay18 ndo kaupost wimbo huo
Wakishavurugwa wanatafuta ndio mchawi
 
Wasinii wa zamani bhana pesa walipata wakachezea walifikiri labda watafanya mziki mpaka uzeeni na kubaki kwenye chati wao nikuponda raha tu.

Sasa hivi wanaibuka kutokea kwenye mashimo kila mmoja kwa wakati wake,nao wakitoka huko target yao ni Diamond..
 
Yaani hapo iko hivi:

Kuna YouTuber anajiita zerokay18 ame upload wimbo wa Mapenzi kitu gani wa msanii MB Doggy hafu yeye kaandika muimbaji ni Diamond Platnumz.

Kwahiyo kwenye makosa hapo ni zerokay18 na Diamond hafaidiki kitu hapo.
Hee
 
Yes jamaa yupo sahihi alichokosea ni kumtaja Diamond directly maana Diamond hausiki anaehusika ni huyo WINGA anaejiita zerokay18 mwenye njaa alieudandia wimbo wa watu bila idhini na wapo wengi tu wanapost nyimbo za watu YouTube sio huyo tu
✍️
 
Back
Top Bottom