Mazuri ya Edward Lowassa

Mkuu Gamba la Nyoka..kama kiongozi anashindwa kazi kwa nini asiwe let go?

hii ni good idea nakubaliana nayo, ila tatizo ni moja mwenye uwezo wa kumfukuza mkuu wa wilaya ni raisi peke yake, waziri mkuu anaweza tu kumshauri raisi. lakini Waziri mkuu anayo mamlaka ya kumuajibisha mkuu wa wilaya katika mambo mengine, sasa kama alivyofanya Lowasa hapo ni kuita "spade a spade",hapa hakuna cha kumuonea huruma mkuu wa wilaya, kwenda katika ziara ili kupewa information za uwongo/zisizo na substance halafu na wewe ukae tu unasikiliza wakati una power ya kukemea na kufuatilia mimi silikubali hata kidogo

unajua something is better than nothing, kukemea mbele ya wananchi viongozi wabovu halafu baada ya hapo ukafuatilia zaidi utendaji wao kwa ukaribu ni bora zaidi kuliko kufanya mambo kimya kimya.

ni lazima viongozi wetu wakumbushwe majukumu yao kwa dhahiri na siri.period
 
Kwanza naanza kuona huu utaratibu wa risala haufai. Kwa nini Waziri Mkuu asikutane na watendaji wake kwa mfano DC ama Director na kupata presentation one on one halafu ndio akauliza maswali, ku criticize na kupongeza pale inapobidi? Halafu akitoka hapo anaenda kuwa hutubia wananchi akiwa tayari ana full information kutokana na discussion aliyokuwa nayo mwanzoni?

Tunapoteza muda mwingi kwa mikutano mirefu isiyo na good outcome...kwa mfano, kama Waziri Mkuu anatembelea wilaya utakuta kwenye mkutano kuna, kwaya, ngonjera, ngoma, halafu hotuba ya DC, hotuba ya PM, etc., Kama ni siku ya katikati ya wiki basi shule kwa siku hiyo sahau..zitafungwa..also hebu fikiria muda wa kujitayarisha na ngonjera na kwaya maana mara nyingi wanao perform hizi arts mbele ya PM ni wanafunzi...Je tuko efficient kweli?
 
Whither Mwanakijiji?

CH, exactly my sentiments.Muungwana alijaribu kutoka nayo hii watu wakambana, sijui kwa misingi gani.

Lowassa sasa kamshushua mtu page ya tatu kama alikuwa ana build up minondo iko page ya sita na kuendelea :)

Ila mambo ya kutoana nishai hadharani noma, inakuwa kama mtu na watoto wake? Hata hao watoto wakifika age fulani unawapaka kiheshima vile vile.
 
kumbukumbu

DAR ES SALAAM, Oct. 4 (Xinhua) -- Tanzanian Minister for Water and Livestock Development Edward Lowassa had asked the parents in the country to provide their children with a glass of milk every day, local newspaper The African reported on Friday.

Speaking at a press conference Thursday on the eve of Oct. 4, the anniversary of the school's Milk Day celebrations, Lowassa said that Tanzanians drank an average 30 liters of milk a year.
Compared with 150 liters by people in other developing countries, this figure is too low.

Lowassa said that research had indicated that the provision of milk in schools improved attendance.

He pointed out that besides having all the necessary vitamins and in the right proportions, milk aided pupil's concentration.

It is estimated that in Africa a person drinks 40 liters of milk on average, while in Kenya and Zimbabwe, a person drinks 80 liters and 44 liters every year respectively.

Statistics also shows that many people in Tanzania can not offer their children a glass of milk a day because of the high price of milk.

In Dar es Salaam, the capital of Tanzania, 1 liter milk is about 800 shillings (80 US cents) to 1,000 shillings (1 dollars), nearly the same price as a temporary labor charge a day.
 
TUKUULIZE WEYE UNAYEAMINI HIVYO

Nakuunga mkono Mlalahoi lazima ukitoa hoja ujue una sababu una unaweza kuielezea sasa yeye aanze kututajia hayo mazuri nasi tutaangalia kama yako ya kuongezea .OK mazuri mojawapo ni kusema Bungeni kwamba Tarime watawaliwe na sheria ya Kimila na si sheria za Nchi zilizipo kisa ana chuki na Mbunge wa Tarime na wanamzuia mission zake na Barrick . Endeleza sasa
 
1. Ni handsome na pia ana mvuto kuliko MP!

2. Orator mzuri- uwezo wa kushawishi (Kiswahili lakini) ni mkubwa sana!

3. Alijitahidi ktk sector ya elimu pamoja na mapungfu yaliyopo!

4. Muumini mzuri- huwa hakosi kanisani Jumapili!

5. Amejenga shule za Waschana wa Kimasai kule Monduli!

N.k
 
Ametoa mamilioni ya pesa za dhuluma kule kanisani kwake KKT na sas watalia baada ya yeye kuondoka .
 
Lowassa pamoja na ufisadi wake

Ni mfuatiliaji wa mambo pale anapoona atapata big credit kwenye public(mfano kunapotokea natural disaster ni wa kwanza kufika kwenye eneo husika)
 
1. Ni handsome na pia ana mvuto kuliko MP!

2. Orator mzuri- uwezo wa kushawishi (Kiswahili lakini) ni mkubwa sana!

3. Alijitahidi ktk sector ya elimu pamoja na mapungfu yaliyopo!

4. Muumini mzuri- huwa hakosi kanisani Jumapili!

5. Amejenga shule za Waschana wa Kimasai kule Monduli!

N.k

Mzalendo halisi..Lowassa hajajenga shule ya wasichana Monduli (Maasae Girls Secondary School) Hii shule imejengwa na fedha ya wafadhili (makanisa ya kilutheri) kutoka Marekani. Mwanzilishi wa hii shule ni mzee mmoja hivi anaitwa David Simonson na mkewe Eunice wote wamarekani waliyelowea Tanzania, Dave alikuja kama mmisionari miaka mingi sana na anaishi Ilboru Arusha. Ila Lowassa alipata kuwa kwenye bodi ya hiyo shule miaka ya nyuma na sio sasa hivi.
 
Alisaidia kuhakikisha ule mkataba uliowekwa zamani kuzuia Watanzania kutumia maji ya ziwa victoria kwa kilimo cha umwagiliaji..
 
Nnaamini kabisa kuna mazuri aliyofanya..Je ni yapi hayo?

Oh yeah, tuyaseme kama kweli yapo; binafsi sijyaona.

Ukiskia wananchi wa kitanzania wanafurahi kwa kiongozi wao kuanguka kama ilivyotokea kwa Lowasa basi uje kuwa kiongozi huyo ana walakini mkubwa.
 
Oh yeah, tuyaseme kama kweli yapo; binafsi sijyaona.

Ukiskia wananchi wa kitanzania wanafurahi kwa kiongozi wao kuanguka kama ilivyotokea kwa Lowasa basi uje kuwa kiongozi huyo ana walakini mkubwa.

Mkuu, ukweli ni kwamba binadamu tuna hulka ya kupenda kuona mtu mwingine akianguka, tena basi mkubwa akianguka anakuwa na kishindo kikubwa na watu wengi zaidi wanafurahi. Sasa hapa kuna extremes; ukiwa mwema sana(wachache sana hawa) wengi watasikitika. lakini kama unamapangufu tena basi ya kawaida tu(hawa ndio wengi) utasikia miluzi ukianguka! Watu hupenda dramatic happenings!
Nikirudi kwenye hoja;
1. Mchapakazi kwelikweli (Uliza mtu yoyote ndani ya bongo alie wizara ya mifugo, wanamuita baba huyu kwa kuwarekebishia mambo).
2. Ni lobbyst bab kubwa, kitu ambacho kwa throat cutting competitions za sasa ni muhimu sana kwa kiongozi.
3. Mfuatiliaji mzuri wa issues.

Yote haya hayafuti madhambi yake hata kidogo! Vitu kamaa tamaa ya kujilimbikizia mali, jazba, nk.
 
Mrubana,

Mkuu karibu JF, ikiwa mwenyeji basi karibu janvini...
Umesema kuwa Lowassa alikuwa:-
1. Mchapakazi kwelikweli (Uliza mtu yoyote ndani ya bongo alie wizara ya mifugo, wanamuita baba huyu kwa kuwarekebishia mambo).
Swali langu ni kuwa Je, kuna ubora wowote ktk wizara hiyo?..mifugo ama soko nje maaanake unaposema mchapa kazi kwelikweli shurti matunda yawepo!.. unaweza kutupa data za mafanikio ya wizara hiyo..

2. Ni lobbyst bab kubwa, kitu ambacho kwa throat cutting competitions za sasa ni muhimu sana kwa kiongozi.
Swali langu ni kwamba unaposema lobbyst baabu kubwa una maana gani?.. maanake hata Pimp anaweza kuwa lobbyst babu kubwa ktk vitendo vya haramu na vinavyomdhalilisha mhusika.

3. Mfuatiliaji mzuri wa issues.
Swali langu - Again, bado tumesimama palepale kuwa hata jambazi hufuatilia sana nyendo za yule anayetaka kumdhuru...Pimp mzuri ni yule anayefuatilia fedha zake hata kama ni haramu.... what matter ni mazuri kwa Taifa letu. What good amekifanya kwa Tanzania toka ashike madaraka na pengine hnyuma unakojaribu kumpaka utuli.

Lowassa ananuka rushwa, hizo shule zenyewe kalazimisha wanakijiji kujenga na hata kufukuza baadhi ya wakuu wa kata kwa kutolazimisha watu kuhakikisha shule zimejengwa within his time limit...
uko
 
Naungana na baadhi ya waungwana hapo juu kuwa EL kuna mazuri aliyo yatenda ambayo aliya fanya kwa kulinda mitego ya ufisadi ndani ya serikali! Huyu jamaa wakati anatoa taarifa ya kujiuzulu bungeni alisema hakutendewa haki, alionewa, hakupewa nafasi ya kuhojiwa!! Jamani wana JF, mnakumbuka yafuatayo;

1. Engeneer wa Manispaa ya Temeke alifutwa kazi ghafla na kutakiwa kupelekwa mahakamani baada ya jengo mmoja kudondoka pale Keko - Hakumpa nafasi engineer ya kujieleza

2. Mkurugenzi wa wilaya moja (jina sikumbuki) alifutwa kazi ghafla baada ya taarifa kuonyesha kuna ufujaji mkubwa wa pesa - Naye huyu hakupewa nafasi ya kujitetea japo kuwa na nafasi hii hutolewa na Rais

3.Makamba ilibidi aingilie kati na kubeba mzigo wa watendaji wake kama Meya wa kinondoni Londa, na maengeneer wa manispaa ya Kinondoni baada ya EL kuwa washia moto mkali pale Shekilango kutokana na kusuasua ujenzi wa barabara ya Shekilango - Bila makamba kufanya hivyo hali ingekuwa mbaya kwa mukurugenzi na Engineer wa Manispaa na

Ndugu zangu, ''what goes around comes around'' na vitabu vitakatifu vinasema '' auaye kwa upanga hufa kwa upanga'' Rev. utanisaidia hapo!

Zaidi ya hayo, ninacho fahamu mimi huyu bwana alikuwa bingwa wa kutoa siku 10, 20, 30, 180 etc na baada ya hapo hafuatilia utekelezaji wake, kwa mfano;

1. Alitoa siku 30 kwa watendaji wa jiji la Dar kuhakikisha tatizo la traffic jams linaondolewa jijini Dar - Was this realistic wajemeni?
2. Aliunda kitu kama kamati fulani ya kufuatilia ujenzi jijini Dar, ambapo kamati hiyo pamoja na mengine ilipewa kazi ya kuangalia kama majengo yaliyopo yamejengwa kufuata sheria na mipango miji, kamati hii ilianzia Ilila na specifically K/koo - Kuna mtu anakumbuka matokeo ya kamati hiyo yalikuwa nini? Mimi sikumbuki chochote hapa!

Hii ni mifano michache tu ambayo inaonyesha jinsi huyu bwana EL alivyokuwa mtu wa kukurupuka kwenye maamuzi mengi sana!!
festog
 
Back
Top Bottom